Wasamehe mkuu haya maisha tu, bora hao walimu kuliko sisi tusioijua kesho yetu.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣waacheni walimu ni watu muhimu sana hapa nchini.
 
Wewe sio Mwalimu, walimu wenye degree wanaanza na 822,000k
 
Hoja yako ni dhaifu, ungesema mfanya usafi wa BOT, NSSF ningekuelewa wafanyakazi wa bank wana hela gani? Wale ni wahesabu Hela maisha Yao ni ya kawaida tu, advantage Yao nasikia mikopo Yao Haina riba
 
Na kuna watu wa kozi zingine wanakimbilia kusomea Ualimu
 
Serikali waoneeni huruma walimu wanaishi kwa mateso sana, na hizi mvua nyumba zao zinajaa Maji maana zishachoka zinavuja tu, nyumba mbovu kama mabanda ya nguruwe.

Kuna mwalimu nimempa hifadhi kwangu akae Kwa mda maana nyumba zao zinavuja sana, naongea nyumba za serikali ambazo walimu wanakaa. Walimu kwenye hii nchi ni jehanamu tosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…