Maisha ya mwalimu yanakuwa magumu kwa sababu ndio mfanyakazi anayefanya kazi mbili kwa wakati mmoja za ofisini ie. Kuandaa somo na field ie. Darasani hapohapo mshahara huohuo avae, ale, asafiri, alipie watoto ada na kama hana nyumba alipe pango asaidie ndugu kama anao n.k. Si kama kada nyingine angalau unaweza iba au kula rushwa kwa mwalimu huna cha kuiba zaidi ya chaki labda vitabu. Serikali iliangalie na hili pia. Ukiona mwl kajenga ujue ni mkopo ana kigari jua ni cha mkopo tena na kupigwa juu.
 
Sio ccm ni utandawazi umesababisha hayo kada nyingi zinatoa wafanyakazi zamani IT, Computer science, Account na course nyingine zilikua hazina watu wengi vyuoni
 
*Hao walimu wale nyasi, sisi tupo bize kununua ndege yetu sisi viongozi hapa bungeni.
Si tumekubaliana kula kwa urefu wa kamba au mmesahau?*
"Hakika inaumiza sana, lakini watanzania tumezidisha upole. Swala kama hili utasikia tumwachie Mungu, ni kweli lakini tunapaswa kuweka juhudi kwanza."
 
Hawa watu Kuna mda huwa nawaza nasema sio kitu cha kawaida, yani hawana posho yoyote ile katikati ya mwenzi na mshahara wenyewe ni mdogo ivi wanaishijeee?

Mbaya zaidi wamekuwa watumwa kwenye kazi zao. Ni watu wa ndio tuu ndio mana Kila mtu mitaani anasema bora niwe bodaboda kuliko kuwa mwalimu, that means ualimu unadharaulika kwasababu hata maisha yao wanajamii tunayaona

Sasa ajabu ni kuwa, huwezi kukuta mwalimu anadai Haki yake, yani hata ukiwaambia Kuna mitihani ya mock njooni msaishe bure wote wanakubar eti wanaogopa kufukuzwa kazi ilihali inabidi wapewe posho πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mwisho ni kuwa wamekuwa wanawaibia Chama flani kura kipindi cha uchaguzi, Chama hicho hicho ndio kinawadharau hawa maticha.

 
Hawa watu Kuna mda huwa nawaza nasema sio kitu cha kawaida, yani hawana posho yoyote ile katikati ya mwenzi na mshahara wenyewe ni mdogo ivi wanaishije...
Siyo kweli watu wanakimbia uticha ,vijan maelfu kwa mamia wanatafuta kazi hyo kwa tochi na hawaxioni
Jana nimeambiwa rfk wangu amenunua gari mpya
 
Mbona maticha wana maisha mazur kushinda wengi tu mtaan wana miliki nyumba magari viwanja ndani ya mda mfupi tu kwa tz hii ukimiliki gari na nyumba si ushamaliza mana kuwaza kuwa na makampuni n wachche tu ss walim wengi wana maisha mazur tu acha zako na ww
 
Jidanganye
 
Uko sawa sana ndugu Mpwayungu. Nahisi wote wanaokupinga siyo walimu, na kama ni walimu basi niseme mficha uchi hazai.

Ni ukweli kabisa ulicho kiandika ndivyo uhalisia ulivyo. Ila unyonge huu wa walimu kuwa watiifu hata kudhurumiwa na serikali imekuwa faida kwa serikali kutimiza mambo kwa malipo finyu. Kwani siku hizi mitihani mingi ya mock walimu hulipwa nauri tu!

Kwa asiye amini afanye tafiti atakuja na dhuruma lukuki zinazo wakuta walimu.

Walimu wengi wanatia huruma kutokana na kutegemea mshahara tu.

Kusema wajiongeze si kweli kwani maafisa wanawataka kuondoka kazini saa kumi na mbili jioni eti kwa kuwa wazazi wanatoa chakula watoto wale mchana na hivyo kuwalazimisha walimu kuwepo kazini kutwa nzima bila kujali masaa ya kazi kuisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…