Maoni na Msimamo wa Baraza la Katiba la Wasanii

Maoni na Msimamo wa Baraza la Katiba la Wasanii

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Wiki hii kuliitishwa Baraza la Katiba la Wasanii ili kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo kwa ajili ya Rasimu ya Katiba Mpya.
Baraza lilifanyika ofisi za BASATA zilizopo Ilala Dar es Salaam.

MSIMAMO WA BARAZA...

Pamoja na mambo mengine Baraza la Katiba la Wasanii liliafikiana kuweka msimamo mmoja kama ifuatavyo.

  1. Utamaduni uingizwe kwenye Katiba kwani ni unabeba maana pana tena ya utambulisho wa Taifa. Hivyo BARAZA limependekeza vifungu vya kuongeza na vingine viondolewe kwa minajili ya kuulinda, kuuenzi na kuuendeleza UTAMADUNI wetu. Mapendekezo hayo yameainisha maeneo ya kuongeza ambapo ni Utangulizi, Yaliyomo, Haki na Wajibu (Bill of Rights), Mahakama na sura zinginezo.. (nikipata nakala ya dodoso nita-update hii post)
  2. Mfumo wa serikali uwe mmoja na siyo tatu wala mbili. Baraza limeona kuna faida kubwa kama Muungano wa sasa utakuwa "TRANSFORMED" na si kuwa DIVIDED kama wanasiasa wanavyohubiri. Masuala makubwa ambayo yanatuunganisha ni UTAMADUNI, ELIMU, UCHUMI na ULINZI. Kwenye dodoso na mapendekezo ya Baraza kumeelezwa kwa kina kuhusu yote hayo pamoja na hasara za kuwa na serikali tatu.
  3. BARAZA limeona kuwa RASIMU iliyopo imetekwa na Wanasiasa na wanaharakati wenye mlengo wa Kisiasa hivyo KUWABURUZA Watanzania katika misimamo na malengo ya kisiasa wakati wa kutoa maoni yao.

Pia BARAZA limegundua kwamba TUME ya KATIBA ina maslahi kwenye Rasimu iliyopo kutokana na mtindo wanaoutumia wa kuitetea (Defend) rasimu badala ya kuiwasilisha kwa wananchi waichambue. Hivyo imeshauriwa kwamba Watanzania watoe maoni yao kwa UHURU na maoni yao yaheshimiwe badala ya kulazimisha misimamo ya wanaoisimamia sasa.

ZeMarcopolo,

..hata mimi nadhani wasikilizwe.

..haswa pendekezo lao la SERIKALI MOJA.

Hahahahahahahaa

Wewe JokaKuu kumbe MCHOKOZI.

Waache wasanii watoe maoni, wengine pia watoe maoni - lakini mpaka mwisho kama Taifa tunaihitaji kuwa na KATIBA MOJA. Si sahihi kila mtu kutegemea kwamba kila alichopendekezwa kitaingizwa kwenye katiba.
 
Wamesahau

1. Katiba ikataze uvaaji wa suruali chini ya makalio.

2. Katiba ikataze Filamu na Tamthilia zinazohamasisha ngono. (Uvaaji nusu uchi).

3. N.k
 
wiki hii kuliitishwa baraza la katiba la wasanii ili kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo kwa ajili ya rasimu ya katiba mpya.
baraza lilifanyika ofisi za basata zilizopo ilala dar es salaam.

msimamo wa baraza...

pamoja na mambo mengine baraza la katiba la wasanii liliafikiana kuweka msimamo mmoja kama ifuatavyo.

  1. utamaduni uingizwe kwenye katiba kwani ni unabeba maana pana tena ya utambulisho wa taifa. Hivyo baraza limependekeza vifungu vya kuongeza na vingine viondolewe kwa minajili ya kuulinda, kuuenzi na kuuendeleza utamaduni wetu. Mapendekezo hayo yameainisha maeneo ya kuongeza ambapo ni utangulizi, yaliyomo, haki na wajibu (bill of rights), mahakama na sura zinginezo.. (nikipata nakala ya dodoso nita-update hii post)
  2. mfumo wa serikali uwe mmoja na siyo tatu wala mbili. Baraza limeona kuna faida kubwa kama muungano wa sasa utakuwa "transformed" na si kuwa divided kama wanasiasa wanavyohubiri. Masuala makubwa ambayo yanatuunganisha ni utamaduni, elimu, uchumi na ulinzi. Kwenye dodoso na mapendekezo ya baraza kumeelezwa kwa kina kuhusu yote hayo pamoja na hasara za kuwa na serikali tatu.
  3. baraza limeona kuwa rasimu iliyopo imetekwa na wanasiasa na wanaharakati wenye mlengo wa kisiasa hivyo kuwaburuza watanzania katika misimamo na malengo ya kisiasa wakati wa kutoa maoni yao.

pia baraza limegundua kwamba tume ya katiba ina maslahi kwenye rasimu iliyopo kutokana na mtindo wanaoutumia wa kuitetea (defend) rasimu badala ya kuiwasilisha kwa wananchi waichambue. Hivyo imeshauriwa kwamba watanzania watoe maoni yao kwa uhuru na maoni yao yaheshimiwe badala ya kulazimisha misimamo ya wanaoisimamia sasa.

nina maswali machache katika maoni haya.
1. Je hata masogange naye anataka haki za kisanii ili asafiri south africa
2. Yule msanii wa comedy wa chanel 5 anaye piga picha za ngono na dada zetu nae anataka atambuliwe kikatiba?
3. Je haya maoni yanawainclude hata bongo movie? Kama majibu ni postive basi kweli maoni haya ya wasanii ningekuwa mimi msanii wala nisinge jisumbua na rasimu maana bongo movie ni ukahaba mtupu
4. Mlikutana bar gani kujadili maoni haya au kayaandika lulu.
5. Je ni kweli kuwa utamaduni mnao utaka wasanii mmewajumuisha wale wasanii wa customary areas au mmekaa wa mjini tu.
6. Je mfefikiria suala la kuvaa mlegezo, kuchonga kope na kuvaa vimin au pedo ni utamaduni wetu?
7. Je mbona mashindano ya big brother hamjayaweka katika maoni haya hamjui kuwa ndo mnapata majina maana kuna wengine wametoka juzi tu huko kufnya uchafu.
8. Je kunyoa viduku ni utamaduni wetu au wa mchezaji shabalala wa africa kusini
9 je cha arusha cjakiona hapo au cha dodoma kwani si utamaduni wenu.
10. Starehe, pombe, na michakato majimboni mbona kimya jamani wasanii.
 
maoni yanendana na watoa maon maana naona haruf za kuber na ngnja kwenye huo msimam wao!!!!

Na dudu baya alikwepo!!!??.

teh teh teh
 
Naiona taswira fulani katika hicho kinachoitwa Baraza la Katiba la Wasanii,

Mda ukifika mtaona rangi yake halisi,

Watanzania kuweni makini sana katika hivi vinavyojiita "makundi maalumu", vingine ni makundi maalumu kweli kweli kwakuwa yanawakilisha wahuni wawili ama watatu wenye agenda pana zaidi,

Nawaasa ndugu zangu, kuweni na macho manne kila ukionapo kitu kinachojiita "kinawakilisha watu flani"

Ukistaajabu ya CCM utayaona ya Januari Makamba
 
Hahahahahahahaa

Wewe JokaKuu kumbe MCHOKOZI.

Waache wasanii watoe maoni, wengine pia watoe maoni - lakini mpaka mwisho kama Taifa tunaihitaji kuwa na KATIBA MOJA. Si sahihi kila mtu kutegemea kwamba kila alichopendekezwa kitaingizwa kwenye katiba.
ZeMarcopolo,

..kama watu wanaogopa GHARAMA basi serikali moja, tena ndogo, ndiyo solution.

..pia ukisoma historia ya Znz, wakati wa chaguzi kabla ya uhuru bandia wa 1963, utaona kwamba majimbo ya uchaguzi Pemba na Unguja yalikuwa hayafiki 40.

..sasa hebu jiulize leo Znz wana wawakilishi na wabunge wangapi? binafsi nadhani "utitiri" wa wanasiasa huko Znz nao ni tatizo kubwa.
 
Last edited by a moderator:
maoni yanendana na watoa maon maana naona haruf za kuber na ngnja kwenye huo msimam wao!!!!

Na dudu baya alikwepo!!!??.

Teh teh teh
aisee umenichekesha sana tena sana ngoja nikpate pepc then ntarudi humu dah!
 
zemarcopolo,

..kama watu wanaogopa gharama basi serikali moja, tena ndogo, ndiyo solution.

..pia ukisoma historia ya znz, wakati wa chaguzi kabla ya uhuru bandia wa 1963, utaona kwamba majimbo ya uchaguzi pemba na unguja yalikuwa hayafiki 40.

..sasa hebu jiulize leo znz wana wawakilishi na wabunge wangapi? Binafsi nadhani "utitiri" wa wanasiasa huko znz nao ni tatizo kubwa.
akili kama za expert broker hizi au za viroba eti nae kaongea point c muda mref utamtaja dr slaa hapa huchelewi
 
nina maswali machache katika maoni haya.
1. Je hata masogange naye anataka haki za kisanii ili asafiri south africa
2. Yule msanii wa comedy wa chanel 5 anaye piga picha za ngono na dada zetu nae anataka atambuliwe kikatiba?
3. Je haya maoni yanawainclude hata bongo movie? Kama majibu ni postive basi kweli maoni haya ya wasanii ningekuwa mimi msanii wala nisinge jisumbua na rasimu maana bongo movie ni ukahaba mtupu
4. Mlikutana bar gani kujadili maoni haya au kayaandika lulu.
5. Je ni kweli kuwa utamaduni mnao utaka wasanii mmewajumuisha wale wasanii wa customary areas au mmekaa wa mjini tu.
6. Je mfefikiria suala la kuvaa mlegezo, kuchonga kope na kuvaa vimin au pedo ni utamaduni wetu?
7. Je mbona mashindano ya big brother hamjayaweka katika maoni haya hamjui kuwa ndo mnapata majina maana kuna wengine wametoka juzi tu huko kufnya uchafu.
8. Je kunyoa viduku ni utamaduni wetu au wa mchezaji shabalala wa africa kusini
9 je cha arusha cjakiona hapo au cha dodoma kwani si utamaduni wenu.
10. Starehe, pombe, na michakato majimboni mbona kimya jamani wasanii.
Unyanyapaa ni tabia iliyojikita kwenye fahamu za Watanzania wengi.

Hoja zako ama maswali yako yote hayajalenga kutafakari hoja zilizoainishwa hapo juu.

Ni kweli wapo wasanii ambao tabia, mwenendo na hulka zao haziendani na Utamaduni wetu. Lakini wapo wengi pia ambao ni mfano wa kuigwa ktk jamii.

Je tabia ya wanasiasa ndiyo ya kupigwa mfano kwenye jamii kwamba tuwaamini kutuletea KATIBA waitakayo?

Wasanii wamewaza huru na wametoa maoni yao. Ila mkuu unaruhusiwa kuweka mapendekezo yako kuhusu sanaa na utamaduni.
 
maoni yanendana na watoa maon maana naona haruf za kuber na ngnja kwenye huo msimam wao!!!!

Na dudu baya alikwepo!!!??.

teh teh teh
Kuber na ganja havikuwepo kwenye mada na hivyo vitu hutumiwa na watu kama wewe.
Tulijadili Rasimu ya Katiba.
 
ZeMarcopolo,

..kama watu wanaogopa GHARAMA basi serikali moja, tena ndogo, ndiyo solution.

..pia ukisoma historia ya Znz, wakati wa chaguzi kabla ya uhuru bandia wa 1963, utaona kwamba majimbo ya uchaguzi Pemba na Unguja yalikuwa hayafiki 40.

..sasa hebu jiulize leo Znz wana wawakilishi na wabunge wangapi? binafsi nadhani "utitiri" wa wanasiasa huko Znz nao ni tatizo kubwa.

Mechanism ya kukiua cheo cha Rais wa Zanzibar ndio kikwazo.

Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye haoni kwamba serikali moja ndio the way to go, but the question is HOW TO START. Yaani ni sawa na mtu anayeona kabisa kuwa ili aende kazini comfortably anahitaji kununua gari lakini kipato hakiruhusu. Serikali moja ni sahihi, but how do you remove the government of Zaznibar? Any suggestions?
 
Naiona taswira fulani katika hicho kinachoitwa Baraza la Katiba la Wasanii,

Mda ukifika mtaona rangi yake halisi,

Watanzania kuweni makini sana katika hivi vinavyojiita "makundi maalumu", vingine ni makundi maalumu kweli kweli kwakuwa yanawakilisha wahuni wawili ama watatu wenye agenda pana zaidi,

Nawaasa ndugu zangu, kuweni na macho manne kila ukionapo kitu kinachojiita "kinawakilisha watu flani"

Ukistaajabu ya CCM utayaona ya Januari Makamba
Mkuu,
hilo unaloliwaza ndilo tumeliwaza siku zote. Tumetoa maoni yetu kwa uhuru na tutayawasilisha kwa Tume.

Hofu yako inatokana na athari za sumu inayomwagwa na wanasiasa ambayo hata wewe umeathirika nayo. Hayo makundi mnayopambana nayo kila siku kwenye pilika zenu za kisiasa SISI hayatuhusu na wala hatutumiki. Bahati nzuri kwenye BARAZA kulikuwepo na wawakilishi wa sekta zote za sanaa ambao wengi ni waadilifu na wamechangia kwa sehemu kubwa mabadiliko ya sekta ya sanaa na utamaduni.

Be informed kwamba haya mabaraza yatakoma kufikia tarehe 31 Agosti. Hautakaa kusikia tena Baraza la Wasanii la Katiba
 
unyanyapaa ni tabia iliyojikita kwenye fahamu za watanzania wengi.

Hoja zako ama maswali yako yote hayajalenga kutafakari hoja zilizoainishwa hapo juu.

Ni kweli wapo wasanii ambao tabia, mwenendo na hulka zao haziendani na utamaduni wetu. Lakini wapo wengi pia ambao ni mfano wa kuigwa ktk jamii.

Je tabia ya wanasiasa ndiyo ya kupigwa mfano kwenye jamii kwamba tuwaamini kutuletea katiba waitakayo?

Wasanii wamewaza huru na wametoa maoni yao. Ila mkuu unaruhusiwa kuweka mapendekezo yako kuhusu sanaa na utamaduni.
kwa kifupi maoni yenu ni ya kitoto na kisanii kabisa yamekaa kilulu lulu tu au kwa akili ya kawaida tu bila kwenda shule huwezi sema serikali moja so what.what is the basis, what is the objective.
Nakushauri kalete maoni mengine. Haya hatuyataki ni ya kisanii sana
 
Mechanism ya kukiua cheo cha Rais wa Zanzibar ndio kikwazo.

Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye haoni kwamba serikali moja ndio the way to go, but the question is HOW TO START. Yaani ni sawa na mtu anayeona kabisa kuwa ili aende kazini comfortably anahitaji kununua gari lakini kipato hakiruhusu. Serikali moja ni sahihi, but how do you remove the government of Zaznibar? Any suggestions?
Ndugu,
Tukiachana na HOFU na UOGA hilo linawezekana.
Wasanii wamependekeza Serikali moja na Mabunge mawili. Yaani Senate na Congress.

Serikali tatu ni kuua Muungano. Ni hatari sana kwa Usalama wa nchi.
 
mkuu,
hilo unaloliwaza ndilo tumeliwaza siku zote. Tumetoa maoni yetu kwa uhuru na tutayawasilisha kwa tume.

Hofu yako inatokana na athari za sumu inayomwagwa na wanasiasa ambayo hata wewe umeathirika nayo. Hayo makundi mnayopambana nayo kila siku kwenye pilika zenu za kisiasa sisi hayatuhusu na wala hatutumiki. Bahati nzuri kwenye baraza kulikuwepo na wawakilishi wa sekta zote za sanaa ambao wengi ni waadilifu na wamechangia kwa sehemu kubwa mabadiliko ya sekta ya sanaa na utamaduni.

Be informed kwamba haya mabaraza yatakoma kufikia tarehe 31 agosti. Hautakaa kusikia tena baraza la wasanii la katiba
kupendekeza serikali moja inaonekana wengi kwenye kikao walikuwa na haraka ya kusepa maana mngesema serikali tatu kikao kingekuwa kirefu si unajua wasanii kwa gambe wikend leo.
 
Back
Top Bottom