Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Wiki hii kuliitishwa Baraza la Katiba la Wasanii ili kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo kwa ajili ya Rasimu ya Katiba Mpya.
Baraza lilifanyika ofisi za BASATA zilizopo Ilala Dar es Salaam.MSIMAMO WA BARAZA...
Pamoja na mambo mengine Baraza la Katiba la Wasanii liliafikiana kuweka msimamo mmoja kama ifuatavyo.
Pamoja na mambo mengine Baraza la Katiba la Wasanii liliafikiana kuweka msimamo mmoja kama ifuatavyo.
- Utamaduni uingizwe kwenye Katiba kwani ni unabeba maana pana tena ya utambulisho wa Taifa. Hivyo BARAZA limependekeza vifungu vya kuongeza na vingine viondolewe kwa minajili ya kuulinda, kuuenzi na kuuendeleza UTAMADUNI wetu. Mapendekezo hayo yameainisha maeneo ya kuongeza ambapo ni Utangulizi, Yaliyomo, Haki na Wajibu (Bill of Rights), Mahakama na sura zinginezo.. (nikipata nakala ya dodoso nita-update hii post)
- Mfumo wa serikali uwe mmoja na siyo tatu wala mbili. Baraza limeona kuna faida kubwa kama Muungano wa sasa utakuwa "TRANSFORMED" na si kuwa DIVIDED kama wanasiasa wanavyohubiri. Masuala makubwa ambayo yanatuunganisha ni UTAMADUNI, ELIMU, UCHUMI na ULINZI. Kwenye dodoso na mapendekezo ya Baraza kumeelezwa kwa kina kuhusu yote hayo pamoja na hasara za kuwa na serikali tatu.
- BARAZA limeona kuwa RASIMU iliyopo imetekwa na Wanasiasa na wanaharakati wenye mlengo wa Kisiasa hivyo KUWABURUZA Watanzania katika misimamo na malengo ya kisiasa wakati wa kutoa maoni yao.
Pia BARAZA limegundua kwamba TUME ya KATIBA ina maslahi kwenye Rasimu iliyopo kutokana na mtindo wanaoutumia wa kuitetea (Defend) rasimu badala ya kuiwasilisha kwa wananchi waichambue. Hivyo imeshauriwa kwamba Watanzania watoe maoni yao kwa UHURU na maoni yao yaheshimiwe badala ya kulazimisha misimamo ya wanaoisimamia sasa.