Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Narudia tena huenda unabeba maneno yanakuwezesha kujengea utetezi wako tu. Si kawaida kwa binadamu kuonyesha hadharani kufurahia kifo cha mtu. Hivyo usitarajie audience sawa kama ya waliojitokeza kuaga. Hao walioenda kumuaga hawakuwa watanzania wote, sasa sijui unatoa wapi uhalali kuwa watu wote/wengi walihuzunika kutokana na umati uliojitokeza. Na kama hawa ambao waliojitokeza kuonyesha furaha walizuiwa, unawezaje kujua walikuwa wachache?Ndio nimekuuliza ni kipi kinachokufanya ufikiri kuwa kulikuwa na watu wengi waliyofurahia kifo cha Jiwe sawa na wale tuliyowaona wakimuaga Jiwe au zaidi ya wale? usikimbilie kwenye kificho cha kudai et walikatazwa kana kwamba unajua kwamba hao walikuwepo kweli kwa kiwango sawa na kile ila tatizo ni kukatazwa. Ndio maana nikatoa mfano wa maandamano ya Lissu ambayo kwa kutizama mitandaoni mlikuwa mnaonesha kabisa mpo teyari kwa lolote hamuogopi kitu wengine tukawa tunasubiri tuone hizo fujo zitakuaje kati yenu na jeshi la polisi ila kumbe mtaani hali iko tofauti kabisa na mitandaoni na ndio kile kilichotokea siku ya tukio mtaani watu wako bize na shughuli zao hawakuwa na mawazo ya kufanya maandamano hakukuwa kabisa na dalili za kwamba hawa watu walikuwa wamepanga kufanya maandamano.
Sasa naona unaleta story hizo hizo za et walizuiliwa na ndio ishakuwa sababu ya kujifichia.
Hao waliokuwa wanataka kuandamana usalama wao ilikuwa ni kutojionyesha, huku Kila mmoja akisubiri kuona watu wengi kisha ndio ajitokeze. Kumbuka hata viongozi wa hayo maandamano walikamatwa ili kuzidisha hofu kwa waandamanaji. Ingekuwa hakukuwepo na vitisho vya vyombo vya dola kisha watu wasiandamane, hapo ungekuwa na cha kujivunia. Hayo maandamano yatakuwepo tu kama hali ya kidhalimu itajirudia. Hata hao waliotawaliwa miaka zaidi ya 20 kidictator mafanikio Zimbabwe, Egypt, Sudan nk ilisemekana hawawezi kuandamana, lakini siku ilifika na uliona kilichotokea.