Tunajitaji kiongozi ambaye ndiye bora katika wale wanaozungumza.
Kiongozi ambaye Hana lawama, kiongozi ambaye vitivo vyake(faculties)vimetulia.
Kiongozi ambaye watu wote wanaompinga hawawezi kumfanya atetereke, kiongozi mwenye kuelewa upeo wa juu kabisa wa ukweli.
Kiongozi wa Chama ambaye mwenendo wake ni mkamilifu na dhamira zake ni kamilifu.
Kiongozi ambaye amejikita katika kutafakari.
Kiongozi ambaye Hana tabia ya kuona uchungu au kukata tamaa, ambaye Hana hofu wala uchovu.
Kiongozi ambaye ana uvumili u kwa watu; ambaye hagandamani na watu lakini pia hagombani nao.
Kiongozi wa Chama anapaswa kuwa na akili ya wema wakati wote.
Katika kila uwanja maarifa yake yanapaswa kuwa mengi.
Tunataka kiongozi ambaye anaweza kuwaunganisha watu, ambaye akizungumza watu wanakuwa na utengamano,furaha na utulivu.
Kiongozi ambaye anazungumza maneno matamu,yenye hoja na dhahiri.
Kiongozi ambaye hashirikiani na wapumbavu,wenye maoni yasiyofaa,ambao ni waongo,wanaozungumza maneno ya kashfa,ya ukali au wanadanganya.
Kiongozi ambaye anashirikiana na wote ambao wamenyooka,hawada nganyi,ambao kila wakati hufanya kazi baada ya kuzingatia athari ya matendo yao.
Wewe unamtafuta malaika?
Wa nini?
Utampata wapi dunia hii?
Kiongozi yeyote hawezi kukosa lawama, hata angefanya mazuri kiasi gani.
Tunataka kiongozi anayejali maslahi ya Tanzania na waTanzania wote, hata hao ambao hawashibi wakishaiba mali zetu.
Tunataka kiongozi asiyevumilia kabisa uchafu wa ufisadi, rushwa, ubadhirifu na matakataka yote. Hao ambao ni sugu na hawasikii kitu awashughulikie kwa sheria zilizopo; kama hazitoshi, awape Bunge watunge za kuwakomesha wanaohujumu nchi yao, ikilazimu hata wanyongwe kama ndiyo njia ya kuwatia akili.
Tunataka kiongozi anayewaunganisha waTanzania, kama taifa moja la watu wanaotambua thamani ya uraia wao na kuuonea fahari.
Kiongozi asionee watu asiowapenda na kuwafanya maadui, kwa vile hawakubaliani naye.
Kiongozi ajue, uongozi wake ni kuwatumikia waTanzania, na siyo kuwafanya wawe mateka wake wa kumsifia hata anapotenda yasiyostahili.
Tunataka kiongozi ambaye anao uwezo wa ushawishi na kuheshimiwa na viongozi wenzake wa mataifa mbalimbali. Anayeweza kuitetea Tanzania bila ya kujionyesha yeye ni bora kuliko wengine
Na zaidi ya yote, tunataka kiongozi atakayewafanya waTanzania kuwa na uthubutu wa kusema wanaweza kufanya mema kwa nchi yao. Kwamba wanaweza kujiletea maendeleo wao wenyewe, na siyo kutegemea watu wengine watoe misaada kwao.
Watu wanaolinda maslahi ya nchi yao, wakichukizwa na vitendo vya wachache kunufaiki na utajiri wa nchi huku wengi wao wakisononeka na kughubikwa na umaskini.
Kiongozi ahimize kila mwananchi wake anatimiza wajibu wake wa kujiletea maisha bora na kuiendeleza Tanzania kiujumla
Nina hakika kiongozi mwenye sifa hizo zote hayupo, lakini anayejitahidi katika mengi ya hayo atafaa sana kwa taifa hili sasa na kwenda mbele.
Je mama anazo kiasi gani ya sifa hizi? SIJUI! Lakini nasubili nione anaweza nini.