Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Music ni ule ule tu ila amebadilika Dj,Dj yule aliyeondoka alikuwa anapiga reggae,DJ huyu sasa anapiga Blues lakini mnatokwa jasho[emoji16][emoji16][emoji16] eti mama ni kama nesi anakuchoma sindano halafu anakuambia pole mwanangu utaponaa ehhh[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1].
 
Nampongeza mheshimiwa rahisi Mama Samia Suluhu Hasani kwa kuyatoa makato ya 6% (Rentetion Fee) ni jambo zuri kwa wanufaika Wa HESLB
 
Magufuli alikuwa Genius sana kwanza alikuwa amenyooka kama ruler alikuwa hapendi cheap popularity kama ni moja alisema mojaa ili mradi aliamini alichokisimamia.

JPM aliamini nini katika kuboresha masilahi ya wafanyakazi?

JPM aliamini kuwa kuwalambisha nyongeza ndogo wafanyakazi wa serikali na baadaye inaambatana na mfumuko wa bei ni sawa sawa na kuweka maji kwenye basket ya kutunzia takataka yaani unatangaza kuongeza mshahara lkn kesho yake bidhaa zimepanda kwa makusudi tu walioongezewa ni watu wachache wanaumizwa watu weeengi.

JMP aliamini kutengeneza value for money ambalo ndilo suluhisho la kudumu la kutatua changamoto za wafanyakazi woote.

JPM alikuwa anedhamiria kuboresha huduma za kijamii kwa mfano afya yaani alikuwa ameshaanza kujenga magorofa na majengo ya kisasa ili wananchi wapate huduma bora ya afya kwa gharama nafuu badala ya wananchi wakiwemo na wafanyakazi kukimbilia kutibiwa Private unaenda kwenye Hospital ya serikali na bima yako unapata huduma ya uhakika.

Uboreshwaji wa shule za serikali kwamba watumishi wanaoingia gharama kuwapeleka watoto wao private JPM alikuwa amedhamiria kujenga shule bora kabisa za serikali zitakazowavutia wazazi wengi wapeleke watoto wao huko serikalini badala ya kwenda private.

Sehemu zingine ambazo zina multiplying effect kubwa kwenye jamii ni pamoja na kupatikana miundombinu imara, nishati ya uhakika, upatikanaji wa maji safi na salama vyote hivi ndivyo alivyovidhamiria JPM.

Mama ili asipate frustrations anyooke kama ruler sera zake zieleweke maana hajasomeka mpaka leo kwamba ni Rais bahiri au anatoa hela mitaani.
 
Magufuli alikuwa Genius sana kwanza alikuwa amenyooka kama ruler alikuwa hapendi cheap popularity kama ni moja alisema mojaa ili mradi aliamini alichokisimamia...
Ama kweli kuboresha!" ndo anatembea na begi la hela kwenye gari kugawa njiani ili kuwin cheap popularity.

Tunachomshukuru mama anafanya jitihada kuturudishia uhuru wetu.

Ile mijeredi hatuitaki tena , sisi si maksai, sisi ni binadamu.

Nchi ilitumbukia gizani, mama anarudisha mwanga,, tumwombee atimize lengo lake.

[emoji120][emoji120][emoji120]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Magufuli alikuwa Genius sana kwanza alikuwa amenyooka kama ruler alikuwa hapendi cheap popularity kama ni moja alisema mojaa ili mradi aliamini alichokisimamia.
JPM hakuwa genius. Just a experienced person with unlimited ammount of resources. And yes alipenda populism.
 
Wanajamvi najua hapa pana pro hayati, pro old CCM, and pro CHADEMA na wale ambao wapo tu kama kambale sharubu zipovutwa tu popote mwendo ndio unakuwa wa huko huko.

Naomba kwa pamoja tumpe sapoti mama yetu rais awamu ya sita, kwa kumsaidia ikiwa ni pamoja na kufichua maharibifu,hujuma hila na yote yasiyosawa katika njia iliyo ya staha,rais wetu anasikiliza ushauri ni hii ni bahati kubwa sana kupata rais wa aina hii ambaye ni msikivu kwa wananchi wake, nafahamu pia kama binaadamu hatakosa maadui yaani wale wasiomtakia mema watakaokuwa wanajaribu kutumia uandishi wao katika njia ambayo hakika kama ni mwenye hasira kali hayavumiliki, basi waache Mara moja kwani si hekima.

Tumsaidie na tuisaidie serekali katika kukemea wizi, wakwepa kodi, wala rushwa, wafanya magendo, wafanya miradi chini ya kiwango nakadhalka.

ALAMSIKI.
 
Kweli kabisa mkuu. Maana mfanikio yake ni mafanikio ya taifa letu na anguko lake ni pigo kwa watanzania wote waganganjaa na wasio waganganjaa.
 
Mama Samia ana set the pace!

Sasa ni mashambulizi ya kidiplomasia ili kurudisha na kuendeleža uhusiano mzuri na biashara na nchi za jirani.

Tayari Mama Samia katika Uganda na sasa Kenya.

Huu ni mwanzo mzuri.
Matokeo ya hizi moves tutaziona baada ya mwaka.
 
Ukweli usemwe kwenye swala la uwekezaji mama anaonekana atafanya vizuri.

But swala linakuja je kwenye ukusanyaji Kodi TRA hawatamuangusha?

Tuendelee kupambana tufikie 2 trions tax per month.
 
Ukweli usemwe kwenye swala la uwekezaji mama anaonekana atafanya vizuri.

But swala linakuja je kwenye ukusanyaji Kodi TRA hawatamuangusha?

Tuendelee kupambana tufikie 2 trions tax per month

Mungu ibariki Tanzania.
TRA SSH ameshajiangusha mwenyewe, saivi wafanyabiashara hawatoi tena receipts za EFD , wanajua hakuna wa kuwagusa tena, SSH anajua kuropoka vitu ambavyo vinaleta madhara makubwa baadaye.
 
TRA SSH ameshajiangusha mwenyewe, saivi wafanyabiashara hawatoi tena receipts za EFD , wanajua hakuna wa kuwagusa tena, SSH anajua kuropoka vitu ambavyo vinaleta madhara makubwa baadaye.
Mkuu uko TRA?
Inatuzingua sana na kodi zenu za wizi?
 
Asilimia 10 tu ya magu ndio aende nayo, hayo mengine mengi ya kutolipa madeni ya ndani, kuto pandisha mishahara/ madaraja, kuonea wapinzani, nk, ayaache!
 
Mkuu uko TRA?
Inatuzingua sana na kodi zenu za wizi?
Kutoa EFD ni kodi ya wizi ?
Hakuna kada ambayo Tz ni wezi wa kodi kama wafanyabiashara, mtu anayapata faida zaidi ya 100m kwa mwaka anataka kulipa TRA 5m, hii ni sawa na 5% tu wakati mfanyakazi mwenye mshahara huo atapiga almost 30% kama PAYE, wafanyabiashara Tz ni wezi wa kodi.
 
Kwako mama yetu Samia,
Pia usisahau kuvutia wawekezaji kuja kujenga viwanda vinavyo zalisha kemikali kutokana na gesi.

Mama yetu gesi asilia kwa jina jingine inaitwa METHANE (CH4), kama unavyoiona hapo in kaboni moja. Gesi hii inamatumizi mengi kama vile KUPIKIA, KUWASHIA, KUZALISHIA UMEME, KAMA NISHATI VIWANDANI,

LAKINI PIA GESI HII INATUMIKA KUZALISHA KEMIKALI MBALIMBALI ZENYE THAMANI KUBWA KULIKO GESI YENYEWE.

Mama yetu kutoka kwenye gesi tunapa MBOLEA ZA UREA, MBOLEA ZA AMMONIA, MBOLEA ZA SA, MBOLEA ZA DAP, MBOLEA ZA MAP N.K Zitatumika kwenye mashamba yetu na tutakuza kilimo, na tutawauzia majirani zetu.

Mama yetu kutoka kwenye gesi tunapa METHANOL, ina kazi nyingi, ina thamani.

Pia gesi inatumika kutengezea petroli hii hii ya kwenye magari, tunaweza kuwauzia watanzania kiurahisi sana.

Mama nchi za uarabuni zinakua tajiri kutokana na biashara za kemikali. Nchi ya Qatar ni mojawapo mama.

Mama tunakutegemea katika hili.
Ahsante mama yetu,
Tupo pamoja na tunakuunga mkono kazi iendelee
 
Back
Top Bottom