Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Uzi wako inawezekana ukawa na jambo la kulijadili ila ufanyie kwanza eddit maana umepoteza maana.
 
Naunga mkono kwa heshima ya mwanamke wa kwanza kuwa dereva wa gari letu nchini.
Kumi tena kwa mama.
 
Wazo zuri,BUT too soon tumwache afanye yaliyo ndani ya uwezo wake kwanza, after delivery of the promises she is giving and eventually her tenure ends ( hii minne au mitano zaidi if she wishes to continue) ndio tuje tuzungumze habari ya kuchapisha fedha...zoezi la kubadili shilingi sio jepesi, sura haiongezi nguvu ya sarafu bali uchumi imara, ifike wakati shillingi yetu iwe na denomination kubwa ya 1000 badala ya 10000 ..turudi kutumia shilingi 20,10 hata 5 kwa manunuzi, sarafu yetu kidogo iweze kununua dola,pauni, yen n.k, tukiweza kuboresha thamani ya uchumi tukauza nje zaidi kuliko kununua japo tukiweza tu kutumia 1000-1300 kwa dola 1 ya kimarekani hapo tutakuwa pazuri ila kwa sasa narudia tena TOO SOON kuchapisha fedha mpya, zenye sura ya mama, au hayati JPM au BWM au any of wastaafu tulio nao.
 
Kwenye maendeleo italeta impact gani?? Watanzania wengi ni wapumbavu kwakweli mnapenda kujipendekeza kwa ujinga ujinga tuu
 
Tuna watu muhimu kama akina Mkwawa na Songea hao ndio tungetakiwa tuwaweke kwenye fedha
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 kipindi kile walipiga kelele za mwendazake achapishiwe noti saivi zamu ya SSH, ngoja tuone ila Utopolo wameua jana
 
kwakuwa emeelewa hivyo ngoja nisemee kwa namna ulivyoelewa

Sikiliza kijana: hakuna mzee mwenye utimamu wake kamili anayekubali kuishi mjini

Ukiona kuna jitu zima ambalo ni zee lipo mjini halina nyumba wala usafiri binafsi utakao muepusha kutukaniwa mzazi aliyekwisha jifea kimoyomoyo na watoto hasa vijana (wanafunzi).!

Tambua kuna sababu kuu mbili kama si tatu
1.aina ya maisha aliyoichagua kuishi wakati bado ni kijana_inamgharimu

2.kutokutambua wakati sahihi wa kuchukua hatua_akalemaa

Ni kama wapo kwenye net hawana pa kutokea na hii inatokana na kutokukubali matokeo mapema 'mji ni uwanja wa fujo'

Hivyo basi maisha hayawezi kusimama eti kwakua wewe ni babu au bibi

Sasa kesho ukimuita mzazi toka shamba hakikisha unamfata na usafiri binafsi au uba ukikosa kabisa bajaji ili asiwe kwenye makundi hayo.. sawa
 
Achana na Mwendazake team maana bado Wana hangover ya unafiki na kujipendekeza. Tabia hiyo wameileta kwako. Hawatakusaidia kukushauri ukweli ili mambo yaende.

Watumie, Hili ni kwa every aspect of your government be it judiciary, Parliament and executive, of course I am well aware kuwa the other two arms need to be independent, but at some time as a President, you can not avoid "talking" to them.

Maria Sarungi na Fatima Karume wako bold enough kukushauri ukweli na si unafiki.

Kama ulivyosema, as long as one can deliver, you won't mind one's political inclination
 
Ni rahisi kukosoa. Ila kutenda kazi ni jambo lingine. Si kila anaye kosoa anaweza kutenda kazi ya maana akipewa nafasi.

Ni kama mchezo wa mpira tu. Ukiwa nje ya uwanja ni rahisi kuona makosa ya wengine. Ukiingia kucheza ni shughuli nyingine.

Wale wameumbiwa kukosoa. Ndo kitu wanachoweza, ila sidhani kama wanaweza kuwa na msaada wakipewa nafasi za kutenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…