Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan


Mama ametekeleza ombi la upinzani
 
Badala ya kukomaa na wezi bandarini anakomaa na sabaya kuufurahusha upande x

Ipo siku wapinzani watataka fulan mwengine atolewe atatolewa
Makada tumechutuma kwenye hili
Ila kwa usikivu na ufuatiiaji wa mambo mitandaon atakua ameona wapinzani hawajawai kua na jema over
 
Mkuu kwani wewe umezuiwa kupiga mdundo wako, mama mwenyewe atachagua ngoma ya kucheza....kwa nini kumchagulia ngomaaaa!
 

Yaani katumbuliwa halafu kawa DC mstaafu.... huna hoja unaleta vioja.

Ka hiyo kupambana na upinzani na kudhibiti democracy ndo anakuwa ametekeleza majukumu yake kama DC... only idiot think alike.

Nikueleze hivi Mama kuna mambo yuko sawa na Mwendazake lkn kuna mambo ambayo hakubaliani nayo kama hayo ambayo mpuuzi mwenzio Nyangoro Sabaya amefanya.
 
Sifa zilimuangusha Joyce Banda wa Malawi akitafuta kuwafurahisha wamalawi kuliko mtangulizi wake na wafadhiri hadi akaruhusu ushoga. Yuko wapi leo hii? NGO ni tofauti na nchi. Nchi haihitaji umaarufu binafsi na kusifiwa na wafadhiri, ni heshima kwa wananchi wake.

Rais wetu amemsimamisha mkuu wa wilaya kwa uchunguzi. Uchunguzi upi? Amua tu kwamba nimekuondoa kwa taarifa ulizonazo. Huyu ni afisa aliyefanyiwa vetting, ambaye kila anachokifanya kila siku kinaripotiwa na DSO ngazi za juu hadi taifa? Kumsimamisha ni uzembe na kutafuta kujulikana maana kila kitu kiko mezani kwa rais.

Rais wetu alihitaji muda wa kuifahamu nchi na makabila yake na uhusiano wetu na hata kujua yapi yalifanywa na serikali zilizopita zote, kabla hajaanza hizo papala. Uchagani kuna dhalau ya makabila yote yanayowazunguka na kwa mkuu huyu wa Wilaya, anayetokea mkoa jirani kwao wanaona hastahili kuwatawala. Ni hivyo kote! Iwe ni Shehe, Padri, Askofu, Diwani, mbunge, nk. Hawataki kabila jingine. Ooh! Njoni na matusi sasa lakini huo ndo ukweli.
 
Una uhakika gani kuwa amepata taarifa toka mitandao? After all mitandao ni source of information , ni matter ya kuzichuja.

Mfano wewe hapo jaribu kuandika kuwa utapindua serikali kama utalala nyumbani kwako.. unataka kusema taarifa kama hiyo ipuuzwe? Never!

Pili, Kwani hana njia za kupata taarifa za watu anowataka kupata tarifa zao kwa kutumia official means?

 
Sabaya alikuwepo hai kimkakati kila mmoja anajua , na alichokifanya ni Kwa manufaa ya CCM na ilimlazimu kufanya hvyo ili kufanikisha alichokifanya , kama mama anatafuta namna ya kumweka sehemu nyingine Sawa Ila kama amemfukuza Mazima basi amechochora , lakn ndo hvyo sometyme unajitoa kudhalilika alaf badae unatupiwa vilago
 
Tulia dawa ifanye kazi,dawa ya kushusha homa, vipo vidonge na sindano wewe, chagua sindano ama vidonge.
 
Endelezeni tu dharau,ukizingua ana zingua,tena uzuri sii kwa fedheha,ila kistaarabu kabisa.Pole kama ndiye mhanga mwenyewe.
 
Hama nchi na umwache mama arudishe nchi kwenye mstari. Hatuwezi kundesha nchi na wahuni kama hao unaowatetea hapa, Mama piga kazi, tuko wote kwa kila hali.
 
Acha kupotosha ,serikali hakuwahi kumtuma kwenda kupora maduka.
 
Tatizo lenu hamtaki kuamini kuwa baba yenu aliye wapa kiburi cha kufanya mnavyotaka amesha kufa.

Tulia sasa mtazame dunia inavyo kwenda .

Ndiyo msahau kabisa kugusa milango ya Ikulu.
 
Hizo tuhuma za kuomba rushwa,kuvamia sehemu na mabunduki kwako ni sawa?Wacha uchunguzi ufanyike!kwenye ukweli uongo hujitenga tulia,yataonekana yaliyopo!
 
Mtajifunza utawala wa sheria na haki taratibu mpaka muelewe, mmezoea vya kunyonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…