Shalom from Jerusalem,
Wandugu, kwa maoni yangu, naona kwa muda mfupi sana aliokaa madarakani Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kipaji cha hali ya juu sana cha uongozi kwa kuonesha mambo makuu yafuatayo yanayomfanya amzidi mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli;
1. Ametoa uhuru kwa mifumo ya serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia kufanya kazi na kuondokana na mfumo wa ONE MAN SHOW uliotumiwa sana na mtangulizi.
2. Hatumii maguvu sana kwenye kuelekeza mambo maana amewaamini wateule wake kufanya kazi kwa nafasi na kuonesha vipaji vyao.
3. Neno haki halikauki mdomoni mwake, jambo ambalo lilikuwa ni gumu sana kwa mtangulizi.
4. Ameiamini sana SAYANSI na siyo consipiracy theories kwenye kukabiliana na janga la corona na kuteua tumbe ambayo imekuja na mapendekezo ya namna bora ya kuushinda ugonjwa.
6. Anachagua maneno ya busara wakati anaongea.
7. Kwa kiwango kikubwa amerudisha diplomasia na nchi nyingine duniani na pia amerejesha mahusiano mazuri na mashirika ya kimataifa.
8. Anafuatilia watu wanasema nini kupitia vyanzo mbalimbali kutoka kwa wananchi na kuvifanyia kazi.
9. Anakwenda na wakati, anathamini maoni yanayotolewa kupitia mitandao ya kijamii, maana anajua ndiko dunia ilikofikia na huwezi kuizuia.
10. Ameondoa hofu kwa watumishi wa umma ambao kimsingi mtangulizi wake aliwahukumu bila hata kuwasikiliza kwa kuwadhalilisha hadharani ili apate umaarufu.
MAMA YETU NAKUOMBEA AFYA NA HEKIMA MAANA JUKUMU ULILONALO NI KUBWA, MUNGU AKULINDE