Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Shida yetu wabongo ni wasahaulifu sana na tunapenda vitu vya kutufariji kwa muda mfupi tu

Hizo sifa unazompa Mh Samia ni mambo ambayo Jakaya aliyatekeleza kwa asilimia kubwa sana,, aliachia Uhuru wa habari, demokrasia ilitamalaki, taasisi za Serikali na NGOs zilikuwa huru pasipo kuingiliwa ingiliwa etc

Kwa kifupi JK alipenda Serikali iweke mifumo ya kujiendesha lakini shida kubwa iliyomuangusha ni kuwa wabongo wana hulka ya wizi wizi na ufisadi,, kelele za wizi wizi, ufisadi, rushwa zilikuwa kila kona

Kwa mfano tu watumishi hewa ktk ngazi za Halmashauri ziliratibiwa ktk ofisi za wakurugenzi, vyeti feki ziliratibiwa kuanzia wizara ya utumishi mpk ngazi za Halmashauri

Utekelezaji wa miradi asilimia kubwa ulikuwa chini ya viwango huku ikiidhinishwa pesa nyingi ktk hio miradi tofauti na uhalisia,, barabara za Halmashauri zinatengenezwa leo kwa kiwango cha lami baada ya mwaka ni nyang'anyang'a, kuna kipindi Halmashauri ya bagamoyo mjini ilijenga vyoo vinne vya shule kwa tsh 700ml ilizua kelele sana mpaka Mkurugenzi akahamishwa

Kwa kifupi ilitosha kuona namna Watanzania tusivyokuwa tayari kujisimamia wenyewe ktk nafasi mbalimbali za juu tunazoaminiwa,,, yaani kila mtu ktk ngazi za juu anawaza kuiba tu

Pamoja na mambo mengineyo haya tu machache yaliifanya Serikali ya JK ionekane imejaa wahujumu uchumi, ufisadi, rushwa na wizi ikavifanya vyama kama Chadema na vingine vya upinzani kupiga kelele sana juu ya huu udhaifu

Ndio maana JPM alipoingia madarakani alianza kusafisha Watumishi hewa,, Serikali inalipa billions of money kama mishahara kumbe wachache ndio wanazitumbua

Kwahyo anachokifanya Mamá Samia awe makini na macho kwelikweli kwasababu hizi taasisi za Serikali hazipaswi kuachwa huru kwa kiasi hicho kutokana na Watanzania baadhi wana hulka ya wizi, rushwa na ufisadi

Hata kama tulimchukia JPM lakini kwenye ukweli pasemwe tusisubiri muda ndio msema kweli ilhali ameyasafisha baadhi ya mambo ambayo Chadema na wapinzani wengine na Watanzania tusio na chama tuliyapigia kelele sana ktk awamu zilizopita
 
Huyu mama anaongea mambo ambayo yako wazi na yanayoshikika na kueleweka kwa akili za kawaida na ukiviangalia unaona utekelezaji wake unawezekana,sio wale waliokua wanatuhubiria ndoto zao kubwa bila kuonyesha namna ambavyo hizo ndoto zitatekelezeka,wakishindwa wanalaumu mabeberu.Kuna kiongozi alikua mzuri sana kwenye kuongea mambo makubwa makubwa ambayo ukiyaangalia unaona kabisa anadanganya kwasababu utekelezaji wake niwa zaidi ya miaka 100.Sasa hii ilikua kuhadaa watu nakwavile watu wanapenda kusikia mbwembwe nyingi bila kujiuliza maswali ya kina akajikuta anapata wafuasi ila ukweli ni kwamba zile zilikua porojo za siasa kama porojo zingine.Ngoja tuone mama atatufikisha wapi maana mengine yaliyobaki ni utekelezaji tu.
 
nasikia tetesi zikidai he was assassinated.... whether it was done to save the interest of the state or of some powerful individuals, that i don't care. ninachoshukuru tu yule mshenzi na katili hatunae tena duniani, no regret.
 
Watanzania lazima tumpe Mama Samia thumbs up mpaka sasa.
Yuko kwenye right track.
Anasma sera na maneno yanayoeleweka kirahisi, na anateua watu ambao tunaelewa watamsaidia katika kutekeleza sera zake n kusaidia uongozi.

Litakalodaiwa sasa na wananchi ni kutorudi kule walikotoka, kwenye kuishi kwa wasiwasi wa kubambikwa mikesi isiyo mbele wala nyuma.
Wafanyabiashara kupigwa kodi za kufilisi mtaji, na wengine kubambikwa kesi za uhujumu uchumi.
Haya mambo tusiyaachie kuwa ni by chance.
Mama Samia akimaliza muda wake itakuwaje?

Tunaweza kupata tena mtu kama aliyekuwa wa Awamu ya Tano, mtu katili, asiyesikia, serikali na dola kandamizi.

Hapo ndo tunataka Mama Samia aanze haraka iwezekanavyo mchakato wa kurekebisha Katiba, ili tuliyoyaona yaishie kuwa a bad nightmare!!!
 
Ofisi ya Bunge napo kapiga hodi na kutikisa- Covid kumi na tisa sasa matumbo joto..hatma haijulikani.
 
Wazalendo Kama wakina sabaya makonda bashiru.

WaTanzania kweli mtaliwa mpaka mchakae mkuu wa wilaya tu ana bil 3 kwenye account makonda nadhani atakuwa na trillion. Gambo alitumia bil kutengeneza mazingira nje ya kampeni. Kweli nikikwepa kulipa Kodi ata Mungu hatanihukumu.
story zako za kusadikika peleka ikulu. hapa amna mtu atakusaidia zaid ya kusoma na kupita
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Nirejee kwenye mada husika,ni ombi letu sisi watanzania wafanyabiashara wafanyakazi wa online business na wengineo ambao tumekuwa tukitumia huduma za internet kwa masuala ya kikazi na kibiashara,mpendwa rais wetu ulifikirie suala hili kwani pia ni njia mojawapo nzuri tu ya kuingizia nchi mapato kwa kukata commission na percentage zake stahiki,pia itasukuma watanzania wengi katika kuingia katika kazi za kimtandao za dunia yetu ya kisasa.
WASALAAM.
 
Mi naomba tu mama samia aniteue katika nafasi yyte ile (hasa inayohusisha utekelezaji/execution) ili nitumikie taifa langu maana nmetumia miaka 13+ kusoma lakn leo hii siitumii elimu yangu popote.
 
Hakuna ubishi sasa hali yetu imerejea kama ile tuliyoizoea siku zote. Hali ya kutumia common sense zetu kuendesha mambo yetu.

Common sense hufanya na kufanikisha mambo ambayo ni common pia. Kama hupendi kuwa common usitumie common sense, badala yake tumia uncommon sense ili ikupe uncommon mafanikio.

Mfano, wazungu kuja kutafuta makoloni Africa walitumia uncommon sense zao, kama wangetumia common sense wasingehatarisha maisha yao kutafuta watu wa kuwatawala na kuwanyonya. MTU anaetumia common sense hawezi kuwa shoga kwakuwa common sense inamtaka aoe mwanamke sio mwanaume mwenzake. Common sense inamfanya MTU aogope kufa, kutengwa, kuumizwa na kuugua. Common sense imekosana sana na kujaribu kitu kipya kwakuwa present is known and safe. Uncommon sense inawafanya watu kuthubutu bila kujali matokeo yatakayopatikana.

Common sense ni ile inayosema "kwa muoga kunakwenda kicheko lakini kwa shujaa kunakwenda kilio"

Common sense inajali zaidi wengine, utu wao na haki za wengine. MTU anaetumia common sense ana marafiki wengi na maadui wachache.
.
 
Mh. Rais wa JMT ambaye ni Amiri jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,raia namba moja na mfariji mkuu nchini Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassan amekua kweli ni mama wa Taifa.
Bila kupindisha maneno amesema Takukuru wamebambikizia watu kesi na amewataka wafute kesi hizo. Wamefuta kesi 147.

Mh. Rais hii ni fahari kubwa sana kwetu kua na kiongozi kama wewe lakini pia ni aibu na kichekesho kua na taasisi hiyo inayojiita Takukuru. Aibu kubwa sana kwa taasisi hiyo tena haifai kuaminika tena.
Umemla kichwa bosi wao lakini wabambikaji kesi wakubwa wapo mikoani na wilayani. Wanatia aibu sana. Nao wakuu wa Takukuru ambao wamelala usingizi wa pono saidia kuisafisha nchi mama,tulikua tunaelekea pabaya. Kama Takukuru ndio imeoza hivyo vipi hizo taasisi zinazo simamiwa? kama taifa tulikua tunaelekea kua taabani.

Takukuru hii inaweza kununuliwa na mtu mmoja. Mfano Tanga jiji Takukuru boratu ungeifuta. Wanatumia hela za umma bure. Hawana TIJA katika taifa. Wanaungana na watuhumiwa. Ikipelekwa kesi inayomgusa Mkurugenzi wa jiji,aliyelalamika lazima rumande itamhusu. Kama ukitishiwa usipoogopa utalazwa lupango. Kama nimtumishi utanyanyasika sana mpaka baadhi ya watumishi wameacha kazi.
Rushwa ya watu wanaotamaniana imetawala na jiji linatisha. Wasiokua na sifa wamepewa kazi ya kuongoza idara za serikali ndani ya jiji.

Ardhi inaporwa kwa hao wanaoitwa wanyonge na kupewa wenye nazo. Lukuvi maji ya Tanga chini ya Mkurugenzi aliyepo amechemka. Lukuvi kina cha Tanga kimekua kirefu kwake,achilia mbali Shigela na Mwilapi( RC) na (DC) wao hawahusiki na utatuzi wa kero za wananchi hasa ardhi.
Mh. Rais pia amewataka polisi kufanya uchunguzi wa kesi haraka na kulitaka jeshi hilo liache kubebesha watu kesi za uongo. Hongera sana mama Mungu akuweke tunakuhitaji

Mh. Rais ifumue Takukuru ingawaje wapo watumishi walio waadilifu lakini bora wamekiri kuwahujumu raia wenzao kwa kuwabambika kesi 147,wamejitia doa na hawaaminiki.

Anza na Tanga jiji maana Takukuru wanaungana na wateule wako kunyanyasa raia wako.

Kama ukifanyika utafiti wa kina, Tanga jiji itakua miongoni mwa halmashauri vinara wa rushwa(za aina zote) na mazingira magumu kwa baadhi ya watumishi na wakaazi wake. Rushwa kwenye ardhi imeacha watu wamekufa,wamepoteza mali zao,watu wameuziwa viwanja vyao mara mbili na Afisa ardhi amepelekwa Takukuru lakini wenye mamlaka ndani ya jiji lake anamkingia kifua.

Mh. Rais msaidie Ummy Mwalimu Tamisemi kwake ni mzigo mzito

Mh. Rais wafariji watanzania na wanatanga kwa kuondoa hao waumini wa kula rushwa na kubambikia kesi raia
Karibuni wanajukwaa kw a mjadala
 
Awamu ya Tano ilikuwa ya ajabu sana, Au Magufuli aliwahi ishi na Wasabato Masalia? Maana yeye chanjo kwake ilikuwa mwiko.
Halafu kichwani alikuwa anaamini yuko vitani na adui Beberu ambaye hatukuwahi kumuona
 
Angekuwa mzalendo angewawajibisha hao waliwabambikia kesi na kuwapa fidia walioathirika na ukatili huo.....neno uzalendo siyo rahisi rahisi ivyo mkuu
Mfano aliyekua Mkurugenzi wa Takukuru yupo anapiga jaramba akisubiria kupangiwa kazi nyingine
Amewajibishwa
 
Tangu mwanzo, mwanamke anapokuwa sambamba na mwanaume amekuwa msaada sana kwa mwanaume! Shida ni pale anapojitenga na kuwa mwenyewe mfanya maamuzi akizungukwa na makelele yenye kila aina ya vishawishi...ndipo hujikuta anatamani kuonja visivyoonjeka...anapokea tunda la mti wa kati linalomfundisha kuyaonja mabaya! Na anapokutana na mwanaume wake kwa ushawishi wake usiokifani anamlisha na kumuonjesha mabaya pia!
Mama yetu Samia, uling'ara sana ulipokuwa sambamba na jembe letu, shujaa wetu, Dr. JPM! Sasa upo mwenyewe ukisikizishwa makelele yote yenye vishawishi kama vyote, chondechoje hayo machanjo yako kama unayapenda sana we jiagizie tu kisirisiri ujichanje mwenyewe na hiyo team au tume yako ya utafiti wa kimagumashi wa covid-19, mtuache sisi tuishi maisha yetu mazuri tuliyoachiwa na Muumba wetu!
Msituletee hofu ya kubumbwa! Na tunataka vinasaba vyetu vibaki 'pure'! Hatuhitaji kuongezewa vya covid-19 na mengine mengine 😠!
 
Back
Top Bottom