Mh. Rais wa JMT ambaye ni Amiri jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,raia namba moja na mfariji mkuu nchini Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassan amekua kweli ni mama wa Taifa.
Bila kupindisha maneno amesema Takukuru wamebambikizia watu kesi na amewataka wafute kesi hizo. Wamefuta kesi 147.
Mh. Rais hii ni fahari kubwa sana kwetu kua na kiongozi kama wewe lakini pia ni aibu na kichekesho kua na taasisi hiyo inayojiita Takukuru. Aibu kubwa sana kwa taasisi hiyo tena haifai kuaminika tena.
Umemla kichwa bosi wao lakini wabambikaji kesi wakubwa wapo mikoani na wilayani. Wanatia aibu sana. Nao wakuu wa Takukuru ambao wamelala usingizi wa pono saidia kuisafisha nchi mama,tulikua tunaelekea pabaya. Kama Takukuru ndio imeoza hivyo vipi hizo taasisi zinazo simamiwa? kama taifa tulikua tunaelekea kua taabani.
Takukuru hii inaweza kununuliwa na mtu mmoja. Mfano Tanga jiji Takukuru boratu ungeifuta. Wanatumia hela za umma bure. Hawana TIJA katika taifa. Wanaungana na watuhumiwa. Ikipelekwa kesi inayomgusa Mkurugenzi wa jiji,aliyelalamika lazima rumande itamhusu. Kama ukitishiwa usipoogopa utalazwa lupango. Kama nimtumishi utanyanyasika sana mpaka baadhi ya watumishi wameacha kazi.
Rushwa ya watu wanaotamaniana imetawala na jiji linatisha. Wasiokua na sifa wamepewa kazi ya kuongoza idara za serikali ndani ya jiji.
Ardhi inaporwa kwa hao wanaoitwa wanyonge na kupewa wenye nazo. Lukuvi maji ya Tanga chini ya Mkurugenzi aliyepo amechemka. Lukuvi kina cha Tanga kimekua kirefu kwake,achilia mbali Shigela na Mwilapi( RC) na (DC) wao hawahusiki na utatuzi wa kero za wananchi hasa ardhi.
Mh. Rais pia amewataka polisi kufanya uchunguzi wa kesi haraka na kulitaka jeshi hilo liache kubebesha watu kesi za uongo. Hongera sana mama Mungu akuweke tunakuhitaji
Mh. Rais ifumue Takukuru ingawaje wapo watumishi walio waadilifu lakini bora wamekiri kuwahujumu raia wenzao kwa kuwabambika kesi 147,wamejitia doa na hawaaminiki.
Anza na Tanga jiji maana Takukuru wanaungana na wateule wako kunyanyasa raia wako.
Kama ukifanyika utafiti wa kina, Tanga jiji itakua miongoni mwa halmashauri vinara wa rushwa(za aina zote) na mazingira magumu kwa baadhi ya watumishi na wakaazi wake. Rushwa kwenye ardhi imeacha watu wamekufa,wamepoteza mali zao,watu wameuziwa viwanja vyao mara mbili na Afisa ardhi amepelekwa Takukuru lakini wenye mamlaka ndani ya jiji lake anamkingia kifua.
Mh. Rais msaidie Ummy Mwalimu Tamisemi kwake ni mzigo mzito
Mh. Rais wafariji watanzania na wanatanga kwa kuondoa hao waumini wa kula rushwa na kubambikia kesi raia
Karibuni wanajukwaa kw a mjadala