Wakuu Salaam,
Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.
Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?
Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.
Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.
Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.