Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hii ni Tanesco Tukuyu

Tumezulumiwa pesa zetu zaidi ya miaka miwili baada ya kusitisha mikataba yetu ya kazi chakushangaza wafanyakazi mikoa mingine walishalipwa ni Tukuyu peke yake bado wameshikilia pesa zetu pamoja kufungua kesi mahakamani na Takukuru bado uongozi umegoma kulipa pesa zetu tunaishi kama mashetani mtaani madeni kibao naombaTanesco makao makuu au wizara kuingilia kati ili tulipwe pesa zetu kama mikataba inavyo sema na Fidia juu ya usumbufu,walioshikilia pesa zetu wachukuliwe hatu za kesheria Tanesco Tukuyu wanaichafua Tanesco vibaya mno
 
Nilitaka nisikujibu ila acha nitie neno

1. Raisi ndo kiongozi mkuu nchini

2. Anatizama idara zote za serekali

3. Nadhani anafanya teuzi zaidi ya 500+ am stand to be corrected

4. Kwa teuzi hizo sio rahisi kujua kila jina la mtu aliemteua na sidhani kama ni majukumu yake

5. Amekuwa muwazi na msema kweli ila kwa mwenye akili sidhani kama raisi kusema vile ndo ticket ya kufuja mali za umma na kujiachia. Raisi hakujui ila anamkono mrefu kuliko maelezo sidhani

6. Nimemaliza
 
Dunia inaenda kasi mubashara ni muhimu.

Ila rundo la wakuu wa mikoa kutinga Dodoma kushuhudia viapo ndio limenishangaza labda kama kuna majukumu mengine!

Hawa Makatibu Tawala wanakwenda kufanya nao kazi hawa MaRC, hivyo uwepo wao kushuhudia wanapokula kiapo ni muhimu!
 
Kipindi cha mkapa kilikuwa ni cha old stone age, completely analogy, dunia inaenda kwa kasi sana, people need to be informed at a considerable high pace. Ukikaa kimya, wanakupiga.
 
3. Nadhani anafanya teuzi zaidi ya 500+ am stand to be corrected

4. Kwa teuzi hizo sio rahisi kujua kila jina la mtu aliemteua na sidhani kama ni majukumu yake

Rais Samia sio mgeni na hii serikali kwani amekuwa VP wa Jiwe kwa nusu karne na alikuwa anatembea nchi nzima hivyo kwa level ya MaRC na MaRAS kusema kweli hawajui majina ya wangi wao inaleta shaka kidogo. Kama Rais hawafahamu vizuri kwenye level za juu namna hiyo je huku chini si ndio tutegemee kuwa wasaidizi wake watakuwa wanamchomekea ndugu na michepuko yao!!!

Anatakiwa awe muangalifu sana kwenye level ya MaDC kwani ni wengi na inavyoelekea sidhani kama atawafahamu wengi majina yao yatakayopendekezwa. Same thing kwa wakurugenzi, due diligence ya hali ya jiu itabidi ifanyike.!!
 
"Wakati hatuna pesa"

Wewe na nani?
Alishindwa kushirikiana na bwana yule ambae "...anakula raha, hata wale wakubwa zake wanamjua!!!" Sijui hawa wanaojilalamisha humu walikuwa wapi wakati wenzao wanajineemesha!!? Au walikuwa wangali wakiimba mapambio na kucheza nyimbo wasizozijua?
Tulikariri mara nyingi tu "...maendeleo hayana chama!!, Tanzania si mali ya mtu bali ni ya watanzania wote..., mtu usiishi kwa kumtaraji mtu..., haikutosha tuliweka falsafa ya maisha... utakachotenda ndicho utakacholipwa wala hutopunjwa 'ikiwa ulifedhehesha watu utafedheheka pia... ikiwa uliumiza utaumizwa pia... ikiwa ukidhulumu usidhani familia yako itadumu katika ukwasi... ikiwa ulijenga chuki usitarajie kuvuna upendo... na... na... na...".
Wengi wa wanaolia na kusaga meno ni wale walioishi kwa "u-kupe" siku hizi wanaitwa chawa... sasa wanapaswa wajitambue na wachape kazi sio mapambio na vigelegele... hatutaki sifa za kijinga
Kazi iendelee
 
Hili shirika halijapata kumuacha mtu salama... watu wanajisahaulisha tu ni awamu ipi watu wameuza sana majenereta!!? Uzuri wa watanzania wiki moja inatosha kuwasahaulisha mambo ya mwaka mmoja!!! Tanesco ina matatizo ya muda mrefu na shida inatokana na watawala waliomo maofisini kutopita mitaani kwa wateja wao kuangalia nini kinaendelea. Aidha siku za mechi kubwa za soka ni jambo la kawaida mara nyingi katika miji mingi umeme kukatika alau kwa kipindi cha dakika 20-45 kisha unawaka ndiposa unajiuliza "kuna biashara gani inaendelea baina ya wenye vibanda vya video na Tanesco?"
 
Kuunganishwa umeme huku kaskazini sasahivi imekuwa ni hisani na siyo huduma ya msingi hata kama umelipia control number zaidi ya mwezi, kuomba kuunganishwa napo utazungushwa mpaka utoe rushwa. Kwa kifupi TANESCO kumeoza kabisa poor customer care
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Tafadhali tupatie namba ya taarifa na namba ya simu kwa hatua zaidi
 
Kwa nini Raisi na isiwe kwanza hatua kwa hatua hadi kwa Waziri.isiwe Raisi ndio kila kitu,wananchi jinfunzeni kuwasakama mawaziri hadi wajue kwamba embe ni tunda,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…