Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hii ni Tanesco Tukuyu

Tumezulumiwa pesa zetu zaidi ya miaka miwili baada ya kusitisha mikataba yetu ya kazi chakushangaza wafanyakazi mikoa mingine walishalipwa ni Tukuyu peke yake bado wameshikilia pesa zetu pamoja kufungua kesi mahakamani na Takukuru bado uongozi umegoma kulipa pesa zetu tunaishi kama mashetani mtaani madeni kibao naombaTanesco makao makuu au wizara kuingilia kati ili tulipwe pesa zetu kama mikataba inavyo sema na Fidia juu ya usumbufu,walioshikilia pesa zetu wachukuliwe hatu za kesheria Tanesco Tukuyu wanaichafua Tanesco vibaya mno
 
Si ushauri mzuri. Mimi sikubaliani nawe..

Awe anahutubia wakati wowote anaoona yeye mwenyewe inafaa na hususani kama ana jambo la kusema...

Nionavyo mimi ni kuwa, ipo kasoro kubwa ya hotuba zake nyingi, ya kusema baadhi ya mambo ambayo hapaswi kuyasema hadharani mbele ya subordinates wake...

Mfano leo ktk hotuba yake kwa ma - RAS na RC amesema kitu ambacho kina- expose udhaifu wake na walio chini yake wanaweza kuutumia kumwingiza mkenge ktk baadhi ya maeneo ktk utawala wake...

Alisema "....baadhi yenu (aliowateua) siwajui vizuri, lakini nitaendelea kuwaelewa kidogo kidogo..."

This is untimely statement and it was absolutely not required to be said there in public like that even if it is true..!!

Hii inatupa maswali sana sisi huku nje. Maana kama humjui vizuri mtu uliyemteua wewe mwenyewe na kumpa jukumu nyeti la uRC au uRAS au Uwaziri nk, ikawaje ukamteua...??

Tukumbuke kuwa wengi wa maRC au RAS wanaongoza mikoa mikubwa yenye wakazi (population) wengi na rasrimali nyingi kuliko idadi ya watu wote ambao Rais wa nchi ya Zanzibar yote anaowaongoza...!

Huwezi kulinganisha mathalani mkoa wa DSM, Mwanza, Arusha, Mbeya nk na nchi ya Zanzibar yote kwa idadi ya watu na rasrimali zilizopo ktk kila mikoa hii...

Nasema hivi kwa sababu, RC au RAS ni mtu muhimu na mwenye wajibu na jukumu nyeti na kubwa sana ktk utawala wa nchi hii. Uteuzi wao lazima uwe very carefully scrutinized...

Sasa Rais kukiri hadharani hawajui kwa undani baadhi ya wateule wake hawa inatia shaka kidogo...

Tuandike na kumshauri kuhusu hili...
Nilitaka nisikujibu ila acha nitie neno

1. Raisi ndo kiongozi mkuu nchini

2. Anatizama idara zote za serekali

3. Nadhani anafanya teuzi zaidi ya 500+ am stand to be corrected

4. Kwa teuzi hizo sio rahisi kujua kila jina la mtu aliemteua na sidhani kama ni majukumu yake

5. Amekuwa muwazi na msema kweli ila kwa mwenye akili sidhani kama raisi kusema vile ndo ticket ya kufuja mali za umma na kujiachia. Raisi hakujui ila anamkono mrefu kuliko maelezo sidhani

6. Nimemaliza
 
Dunia inaenda kasi mubashara ni muhimu.

Ila rundo la wakuu wa mikoa kutinga Dodoma kushuhudia viapo ndio limenishangaza labda kama kuna majukumu mengine!

Hawa Makatibu Tawala wanakwenda kufanya nao kazi hawa MaRC, hivyo uwepo wao kushuhudia wanapokula kiapo ni muhimu!
 
Natoa ushauri kwa rais wa awamu ya sita mhe SSH kuachana na utaratibu huu mbaya uliobuniwa na mwendazake wa kulihutubia taifa kila anapowaapisha viongozi.

Nini madhara yake?
Frequency ya kulihutubia taifa inakuwa kubwa mpk mhe rais atafika mahala ataanza kuongea petty issues.

Rais SSH ajiwekee utaratibu wake wa kutoa hotuba kwa taifa. Aweza kupanga kulihutubia taifa kila mwezi, kila baada ya miezi 2 ama 3. Mkapa aliweza, na SSH ataweza tu.

Hata anapowaapisha hakuna haja ya kulifanya tukio hilo kuwa live (mubashara). Nyerere, Mwinyi sr, Mkapa na Kikwete hawakufanya utopolo huu wa kuwaapisha viongozi.mubashara.

Bunge ndiyo tunataka liwe mubashara

Nchi ni yetu sote
Kipindi cha mkapa kilikuwa ni cha old stone age, completely analogy, dunia inaenda kwa kasi sana, people need to be informed at a considerable high pace. Ukikaa kimya, wanakupiga.
 
3. Nadhani anafanya teuzi zaidi ya 500+ am stand to be corrected

4. Kwa teuzi hizo sio rahisi kujua kila jina la mtu aliemteua na sidhani kama ni majukumu yake

Rais Samia sio mgeni na hii serikali kwani amekuwa VP wa Jiwe kwa nusu karne na alikuwa anatembea nchi nzima hivyo kwa level ya MaRC na MaRAS kusema kweli hawajui majina ya wangi wao inaleta shaka kidogo. Kama Rais hawafahamu vizuri kwenye level za juu namna hiyo je huku chini si ndio tutegemee kuwa wasaidizi wake watakuwa wanamchomekea ndugu na michepuko yao!!!

Anatakiwa awe muangalifu sana kwenye level ya MaDC kwani ni wengi na inavyoelekea sidhani kama atawafahamu wengi majina yao yatakayopendekezwa. Same thing kwa wakurugenzi, due diligence ya hali ya jiu itabidi ifanyike.!!
 
"Wakati hatuna pesa"

Wewe na nani?
Alishindwa kushirikiana na bwana yule ambae "...anakula raha, hata wale wakubwa zake wanamjua!!!" Sijui hawa wanaojilalamisha humu walikuwa wapi wakati wenzao wanajineemesha!!? Au walikuwa wangali wakiimba mapambio na kucheza nyimbo wasizozijua?
Tulikariri mara nyingi tu "...maendeleo hayana chama!!, Tanzania si mali ya mtu bali ni ya watanzania wote..., mtu usiishi kwa kumtaraji mtu..., haikutosha tuliweka falsafa ya maisha... utakachotenda ndicho utakacholipwa wala hutopunjwa 'ikiwa ulifedhehesha watu utafedheheka pia... ikiwa uliumiza utaumizwa pia... ikiwa ukidhulumu usidhani familia yako itadumu katika ukwasi... ikiwa ulijenga chuki usitarajie kuvuna upendo... na... na... na...".
Wengi wa wanaolia na kusaga meno ni wale walioishi kwa "u-kupe" siku hizi wanaitwa chawa... sasa wanapaswa wajitambue na wachape kazi sio mapambio na vigelegele... hatutaki sifa za kijinga
Kazi iendelee
 
Hili shirika halijapata kumuacha mtu salama... watu wanajisahaulisha tu ni awamu ipi watu wameuza sana majenereta!!? Uzuri wa watanzania wiki moja inatosha kuwasahaulisha mambo ya mwaka mmoja!!! Tanesco ina matatizo ya muda mrefu na shida inatokana na watawala waliomo maofisini kutopita mitaani kwa wateja wao kuangalia nini kinaendelea. Aidha siku za mechi kubwa za soka ni jambo la kawaida mara nyingi katika miji mingi umeme kukatika alau kwa kipindi cha dakika 20-45 kisha unawaka ndiposa unajiuliza "kuna biashara gani inaendelea baina ya wenye vibanda vya video na Tanesco?"
 
Kuunganishwa umeme huku kaskazini sasahivi imekuwa ni hisani na siyo huduma ya msingi hata kama umelipia control number zaidi ya mwezi, kuomba kuunganishwa napo utazungushwa mpaka utoe rushwa. Kwa kifupi TANESCO kumeoza kabisa poor customer care
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Binafsi nimetokea kulichukia hili shirika ,,,kutokana na watendaji wake,,Tarehe 20Apr2021,,nilinunua umeme kwa njia ya Nmb mobile nakupa token ,,kutokana na kiwango cha fedha yangu,,,niliingiza Token nilizopewa ,,,lakn haikuaccept karibu kwa muda wa siku nzima,,,maandishi yaliyokuwa yanajitokeza ni Error 77,,,ndipo nikawapigia TANESCO Emergency,,Chanika nao wakanifungulia TB,,,(Taarifa binafsi)tarehe 26Apr2021,,,wakaja mafundi na hapo ni baada ya kupiga simu sana,wakaniambia kile kiremote nikipeleke Chanika TANESCO,,nitapewa maelekezo huko,Trh27 Apr 2021 nikaenda nikaonana na customer care wakanieleza niingie ofisi ya Engineer.akakiona na kunipeleka kwa muhasiba ,,,eti nilipie 133,097/= kwa kuwa kirimoti kimeharibika ,,,,sikuwa na hiyana ,,nikapewa control number ,,na kulipia kiwango hicho,,,,,,baada ya kulipia nikawapelekea risit,,na kuambia system imeonyesha nimeshalipia hivo nisubiri ndani ya wki moja TANESCO watakuja kuondoa metre ya zamani na kuweka mpya maana ile ya hakuna rimot mbadala,,,.nimesubir toka kipnd hicho cha wiki moja kimeisha,,hakuna fund aliyekuja ,,,nimepiga simu mpaka nimechoka jibu nalopewa TANESCO Emergency,,,wapo njiani watanipitia,,,,Trh 24May nikafunga safar had TANESCO kuwauliza kulikoni mbona sihudumiwi,,,nikaambiwa ,,,nifungue Taarifa upya ,,,maana Hawana metre mpya kuja kunifungia,,hivyo watakuja kukata mfuniko wa metre ya zamani nami nitapata huduma ,,,ivo ndani ya masaa24 watakuwa wamenifikia,,masaaa 24 yamepita hamna huduma ,,nimepiga simu emergency majibu yao ni hayo hayo,,nimewasiliana na Boss wao anaitwa salvatory majibu yake ni yale yale eti watakuja ,,wanataarifa zangu,,jana tarehe 1jun napigiwa simu saa moja jioni,,na emergency ,,niwaelekeze kwangu mewaelekeza lakn hawakutokea,,,nimewapigia simu.kuwauliza kulikoni ,,,,naletewa tu ngonjera,,,,kiukwel ,,nimetokea kuwachukia mno,,.tukichukua hatua za kuwambia viongozi ngazi za juu mtaona tunawachongea,,,,naomba shirika chukueni hatua kwa watendaji hawa ambao wanalitia madoa shirika,,,waziri wa nishati naomba liangalie hilo swala kwa umakini,,
Tafadhali tupatie namba ya taarifa na namba ya simu kwa hatua zaidi
 
Kwa nini Raisi na isiwe kwanza hatua kwa hatua hadi kwa Waziri.isiwe Raisi ndio kila kitu,wananchi jinfunzeni kuwasakama mawaziri hadi wajue kwamba embe ni tunda,
 
Back
Top Bottom