chase amante
JF-Expert Member
- Feb 24, 2018
- 5,599
- 2,115
Habarin wana jf.
Sote tunafahamu kua kilimo ndio uti wa mgongo wa watanzania kwa sababu kimeajiri watu wengi.
Serikali ya Mh kikwete ilianzisha utaratibu wa ruzuku za pembejeo ili kuhakikisha upatikanaji wake uwe rahisi na kuchochea uzalishaji wa chakula, na mazao mengine ya nafaka.lkn utawala wa awamu ya tano uliacha kutoa ruzuku hizo kwa kisingizio kua, kuna uendeshwaji mbovu wa ruzuku hizo.
Kutokana na hali ya sasa ya maisha, inakua ni vigumu sana kwa mkulima kumudu kununua pembejeo(mbolea) kwa sababu ya gharama yake kubwa.
Naomba serikali sikivu ya mheshimiwa rais samia, ianzishe upya ruzuku Hizi na iweke usimamizi madhubuti ili kuendesha ruzuku hizo kwani kufanya hivyo si tu kutachangia uwepo wa usalama wa chakula kwa kila kaya, bali pia kutatoa fursa za ajira na kukuza uchumi wa taifa.
Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app