Mama Samia ,
Nikupongeza kwa dhati kwa kuapishwa kuwa Raisi wetu wa JMT.Hakuna ubishi ya kwamba umepokelewa kwa kishindo na makundi yote hata yale ambayo kimsingi yamekuwa makundi pinzani tangia mwaka 1992.
Mheshimiwa rais ,unayo nafasi ya kuwa raisi wa kwanza tangia mfumo wa vyama vingi kuanzishwa kuwa rais atakaekuwa anakunalika hata na akina Tomas wa upinzani ,hivyo Rais wetu naomba uzingatie yafuatayo:
1.Teuzi zote utakazofanya zizingatie uwezo wa mtu na sio affiliation ya mtu .Mfano former PST marehemu Likwelilie alipatikana kwa kuangalia uwezo na si chama.
2.Wale wenye teuzi na wamebaki kutoa lugha za kejeli kwa waliotofatiana nao ,tengua teuzi zao mara moja kwani wanakiharibia chama cha mapinduzi mfano ;Jerry Muro,Ole Sabaya ,Chalamila na hata yule RC wa Iringa.
3. Hakikisha miradi utakayoibua wewe kama mheshimiwa Rais inafanyiwa tathimini ya kina ,yaani itarudisha hela ya uwekezaji.
4.Jenga mazingira bora kwa ajili ya kukuza sekta binafsi na sio serikali kujikita kuanziasha mashirika ambayo hakika hayana ufanisi wowote mfano Suma JKT.
5.Anzisha sera ya kuvutia wawekeza wa nje ya nchi kwa mgeni yoyote mwenye kuwekeza zaidi ya dola milioni moja za kimarekani apewe resident permit ya miaka mitano bila malipo yoyote.
6.Anzisha Corpote flat rate kwa uwekezaji ambao utachochea ajira kwa wingi, mfano kwenye textile Industries.
Imenibidi nirudi humu jamvini kwani ni nadra saana kuwa na Rais aliepokelewa na makundi yote bila kujali itakadi zao .
Mungu mbariki saaana Raisi wetu Samia aka Mama wa nguvu.