Kwa kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo ilivyokuwa inazidi kudhihirika kuwa Rais Magufuli ni mzalendo kweli kweli na amejitoa mzima mzima kupambania maendeleo ya nchi yetu.
Katikati ya matumaini makubwa namna hiyo taa kubwa iliyokuwa inaangaza imezimika ghafla! Ni vigumu kuamini lakini ndivyo ilivyotokea! Kwa maneno mengine watanzania tumenyang'anywa tonge mdomoni wakati ndo kwanza tumeanza kufurahia utamu wake na kujiandaa kumeza.
Lakini Mungu ni mwema! Mungu ametupa Joshua wetu, (Mama Bi Salma Suluhu). Mungu hakosei. Kama ambavyo ilikuwa ni vigumu kwa Wana wa Israel kumlinganisha Joshua na Musa, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwa watanzania kumlinganisha Bi Samia Suluhu(Rais) na Magufuli!
Lakini katika mipango ya Mungu pamoja na ushujaa wa Musa lakini jukumu lake lilikuwa ni kuwatoa tu wana wa Israeli toka Misri utumwani lakini si kuwaingiza.
Wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi imiminikayo maziwa na asali!
Jukumu la kuwaingiza Wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi lilikuwa ni la Joshua mwana wa Nini! Hali kadhalika Jukumu la Rais Magufuli ilikuwa ni kututoa utumwani (mikono ya mabeberu iliyoshikilia uchumi wetu), kumbuka alivyofuta Sheria ya madini iliyokuwa ya kifisadi na kuweka Sheria mpya inayotoa mwanya wa kufanya marejeo ya mikataba ya madini ili watanzania wafaidike!
Kumbuka Magufuli alivyokataa kupokea amri ya kutushinikiza tufuate matakwa yao namna ya kushughulika na covid-19.
Magufuli amemaliza kwa ukamilifu ngwe yake!
Bi Samia Suluhu(Rais), umepokea kijiti usiogope! Jukumu lako ni kuwaingiza watanzania kwenye nchi ya ahadi! Mama utuvushe!! Mungu yu pamoja nawe utuvushe! Ndivyo Mungu alivyopanga! Paisha uchumi wetu! msingi umeshawekwa. Miradi mingi ya maendeleo uisimamie ikamilike! Watanzania tutakuunga mkono! Tutakuheshimu, Tunakupenda! TUNA IMANI NA Bi SAMIA SULUHU HASSAN (RAIS).
Watanzania tuna JAMBO LETU na Bi SAMIA SULUHU, nalo ni kutuingiza kwenye nchi ya ahadi! Watanzania tuchape Kazi! Tulipe kodi! Tuwafichue maadui wa ndani na nje! Mungu ametupa Joshua wetu, wala tusiogope!