Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

RUSTEM PASHA
nakubaliana na wewe!
lakini huoni utaratibu huu wa ukamataji hauna tofauti na aina za ushughulikiaji wa mambo wa kisheria ya awamu ya tano,ambao karibu 70% ulikuwa ukihegemea kwenye itikadi za kisiasa?
 
Sio kuwakamata mkuu,wapo ambao mpaka muda huu tunavyoandika hapa wameshahukumiwa vifungo gerezeni,yani ile kukanyaga mahakama wala hakukuwa na ile habari ya uchunguzi unaendelea.
 
Jiwe tulikuwa hatupendi yeye na lichama lake. lakini kifo chake kimetuhuzunisha sana. mtu kushangilia kifo cha mwenzako sio jambo jema.

Hii kitu ilianza kwenye utawala wa magu lisu alikuwa anaombewa mabaya live na hamna hatua yoyote iliyochukuliwa
 
Mheshimiwa Rais Mama Samia ni makusudio ya Mungu kuwa nawe leo kama kiongozi wetu mkuu.

Kama familia tuna gonjwa hatari baina yetu, tena linalouwa. Hayupo mmoja aliye salama.

Mengi yamesemwa kuhusu ugonjwa huu:

IMG_20210321_221658_828.jpg


Itoshe kusema, mwanzo mpya wizara ya afya wenye kuakisi hatari iliyoko mbele yetu ni jambo la dharura sana.

Tumepoteza wengi na wanapotea wengi. Kwa pamoja tunaweza kuushinda ugonjwa huu.

Tumuunge mkono mama yetu kuyalinda maisha yetu na yale ya wote wanaotuzunguka.

Ninawasilisha.
 
Tuko msibani lakini kulinda uhai ambao ungalipo ni muhimu pia:

IMG_20210322_075718_462.jpg


Mjingamimi karibu huku tumwuunge mkono mama yetu.

Gonjwa hili linahitaji sana jitihada zetu sote kulikabili na hasa jitihada za serikali.

Kawia ufike.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Ujenzi wa SGR ambao umeruka kipande cha Dodoma-Isaka na kwenda Isaka-Mwanza, urekebishwe.

Uanzie Dodoma-Tabora.

Mabadiliko haya yafanyike mapema ili kupunguza hasara kwa Taifa kabla Wakandarasi hawajaanza kazi.

Wakandarasi hao hao wahamishiwe kwenye kipande cha Dodoma-Tabora.
 
Kuna watu wameanza kujisahau wakidhani serikali imeenda likizo, na wengine wanataka kuleta mazoea kwa mama... Angalieni tena nyongo ya mwanamke ikichafuka ni hatari sana. Hakuna kiongozi yeyote wa juu atafanya kazi kwa maelekezo ya wasaliti... Never

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Kama itapendeza baada ya shughuli zote za mazishi ya Mpendwa wetu aliyekuwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli basi kwa heshima na taadhima tunaiomba Serikali iagize chanjo ya corona ili wananchi wapate kuchanjwa.

Ikumbukwe kuwa majirani zetu tayari wameagiza chanjo na sisi tusione aibu kuagiza chanjo. Serikali iliyopo madarakani imewekwa na wananchi na hivyo mnatakiwa kutusikiliza.
 
Kwa kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo ilivyokuwa inazidi kudhihirika kuwa Rais Magufuli ni mzalendo kweli kweli na amejitoa mzima mzima kupambania maendeleo ya nchi yetu.

Katikati ya matumaini makubwa namna hiyo taa kubwa iliyokuwa inaangaza imezimika ghafla! Ni vigumu kuamini lakini ndivyo ilivyotokea! Kwa maneno mengine watanzania tumenyang'anywa tonge mdomoni wakati ndo kwanza tumeanza kufurahia utamu wake na kujiandaa kumeza.

Lakini Mungu ni mwema! Mungu ametupa Joshua wetu, (Mama Bi Salma Suluhu). Mungu hakosei. Kama ambavyo ilikuwa ni vigumu kwa Wana wa Israel kumlinganisha Joshua na Musa, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwa watanzania kumlinganisha Bi Samia Suluhu(Rais) na Magufuli!

Lakini katika mipango ya Mungu pamoja na ushujaa wa Musa lakini jukumu lake lilikuwa ni kuwatoa tu wana wa Israeli toka Misri utumwani lakini si kuwaingiza.

Wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi imiminikayo maziwa na asali!

Jukumu la kuwaingiza Wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi lilikuwa ni la Joshua mwana wa Nini! Hali kadhalika Jukumu la Rais Magufuli ilikuwa ni kututoa utumwani (mikono ya mabeberu iliyoshikilia uchumi wetu), kumbuka alivyofuta Sheria ya madini iliyokuwa ya kifisadi na kuweka Sheria mpya inayotoa mwanya wa kufanya marejeo ya mikataba ya madini ili watanzania wafaidike!

Kumbuka Magufuli alivyokataa kupokea amri ya kutushinikiza tufuate matakwa yao namna ya kushughulika na covid-19.
Magufuli amemaliza kwa ukamilifu ngwe yake!

Bi Samia Suluhu(Rais), umepokea kijiti usiogope! Jukumu lako ni kuwaingiza watanzania kwenye nchi ya ahadi! Mama utuvushe!! Mungu yu pamoja nawe utuvushe! Ndivyo Mungu alivyopanga! Paisha uchumi wetu! msingi umeshawekwa. Miradi mingi ya maendeleo uisimamie ikamilike! Watanzania tutakuunga mkono! Tutakuheshimu, Tunakupenda! TUNA IMANI NA Bi SAMIA SULUHU HASSAN (RAIS).

Watanzania tuna JAMBO LETU na Bi SAMIA SULUHU, nalo ni kutuingiza kwenye nchi ya ahadi! Watanzania tuchape Kazi! Tulipe kodi! Tuwafichue maadui wa ndani na nje! Mungu ametupa Joshua wetu, wala tusiogope!
 
Back
Top Bottom