Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Tumeshaelewa kwamba ndo umeanza kazi baada ya kusugua benchi.
 
nmetoka kusikiliza Wimbo maarufu wa enzi zetu wa Nyuki akizungunzia asali ina ladha gani toka kwa Hayati Issa Matona

Sanaa iliyotumika kwny wimbo ule kumbe ulikuwa unazungumzia asali waliyolamba Makamanda na Wataalam wa kuchambua report za CAG miaka ya nyuma

Mzee Matona anamueleza Mtawala 'Nyuki' kuwa asali unayoitengeneza inatupendeza waja japo inatengenezwa kwa vitu 'viliyooza' ( haramu) na laiti ungetueleza walambaji tusingetamani kulamba zaid
 
kwa mwendo huu mzuri wa Rais wetu Samia, tutampa kura za kutosha 2025.
tunamuombea afya na nguvu za kutosha.
 
1. Wanalalamika kuwa rais Samia kachagua mzee kuwa kamishina, kisa ni mwalimu wake.

-Mwendazake alichagua professor aliyemsimamia PHD yake kuwa katibu mkuu wa wizara X nasi tulikaa kimya....
Wew kama nani nyumbu mmoja wa njano,

Kwa lipi tuwapigie makofi wajinga nyie,

Kwa kuslow down project ya bwawa la Nyerere kwa maslahi yenu binafsi,

Kwa kuondoa malipo ya umeme ya 27,000/= , au kwa kulazimisha wamama wajawazito kuchanja chanjo ya korona kabla hawajajifungua.

Tukupigie makof kwa royo tuwa yako.

Kunanyakat huwa mnatumia makalio kufikiria enyi nyumbu wa kijan?
 
Kimsingi amejtahidi sana katika kipindi hiki kifupi cha uongozi wake kuliondoa Taifa katika lindi la GIZA na HOFU ambavyo vilikuwa vimekithiri wakati wa UTAWALA wa mwendazake katika Awamu ya 5; Ni jambo jema kwa sababu watu waliojaa HOFU na MASHAKA kuhusu maisha yao, familia zao, wapendwa wao na mali zao hawawezi kuwa na tija katika uzalishaji mali na kuliinua taifa, Hongera sana SSH.

Mimi namshauri kuangazia kwa jicho la tatu katika kuamsha hamasa ya wananchi katika kujiletea maendeleo, kusimamia mipango ya maendeleo inayogusa maisha ya mwananchi wa kawaida moja kwa moja, lakini pia aongeze ukakamavu katika kushughulikia ubadhirifu ambao unaelekea kushamiri kwa kasi ya 5G! hususani TAMISEMI, Wizara za NISHATI na Maji, avisukume zaidi vyombo husika vifanye kazi zake kwa weledi vinginevyo atapambana kuifungua nchi na kuinua utalii lakini ufujaji wa raslimali za taifa na pesa za serikali vitamuangusha asipojizatiti kukomesha kansa hiyo ya ubadhirifu wa mali ya umma.

Kauli yake ile kwamba "kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake lakini kwa kiasi imeleta balaa, wengi wameichukulia kama ni Rhuksa ya kuongeza kasi ya kula rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma! Kwa mwendo huu, hatutafika!

Ni hayo tu kwa leo, Namtakia kila la kheri ili afanikishe maono yake kwa manufaa mapana ya Taifa letu na watu wake, vineno vidogo vidogo havikosekani, visimnyime usingizi, wewe Kanyaga twende, katu huwezi kumridhisha kila binadamu mwenye mdomo wake, makuzi yake na mazoea yake! Blessings and best wishes Madam President!
 
Ninacho kioo hapa mbele yangu, nataka nikiulize jambo gani litatokea Tanzania katika miezi sita ijayo. Lakini naona kwamba swali hilo litakuwa siyo halali, kwa sababu sijaona Rais wala Serikali imekwama katika kitu chochote.

Kioo, watu watauliza,"Kioo gani hicho?"

Kioo ni kifuniko cha taa ya pikipiki, ambacho kina umbo la dish, ambacho chini nimekipaka rangi nyeusi, halafu nakiweka juu ya kitambaa cheusi, nakiuliza maswali.
 
Acha pombe Mkuu
 
Una maana gan, Samia ndiye rangi nyeusi iliyopakwa nyuma ya kioo bila shaka?.[emoji1787]
 
Samia Raisi wangu leo nimekuja Mpanda mkoani Katavi ili kuja kukupongeza umeonyesha usikivu na Busara za hali ya juu kabisa na Uraisi haujakuzuzua kama mtangulizi wako

Ombi langu kwako Mama nimeshuhudia uharibifu mkubwa wa Mazingira nikitokea Tabora kuja hapa Mpanda maeneo yaliyokuwa yamejaa uoto wa asili yanavunwa kwa kasi ya ajabu.

Roho yangu ilikuwa inasinoneka na kulia.

Samia kumbuka miti pia inamuomba Mungu na kulia

Juhudi za lazima endelevu za kulinda Mapori haya zunahitajika,nimepishana na Malori baada ya Malori yaliyojaa Magogo hii ni hatari kubwa.

Mama ukilinda Mazingira Wajukuu wako watakukumbuka ukiwaachia Jangwa Wajukuu wako watakuwa wa kusubiri WFP nadhani unaielewa vizuri.
 
Bandari ya Dar es salaam kuna mabadiliko makubwa ya upakuaji na ushushaji wa mizigo kutoka siku 14 hadi siku 7 mzigo unakuwa umetoka hii ni hatua kubwa sana chini ya Rais Samia Suluhu.
Tutegemee mabadiliko makubwa zaidi ndani ya bandari yetu.
Yale maneno ambayo tulikuwa tunayapigia kelele humu naona yamefanyiwa kazi hakuna longolongo.

#MamaYukoKazini
 
Great Thinkers wa JF,

Hakika Rais wetu Mh. Samia anaupiga mwingi ktk maeneo mengi ya kimaendeleo. Mfano tu ni hili jambo la kuhakikisha anaendeleza yale yote yaliyopo kwenye ilani ya Chama Chetu cha Mapinduzi. Kwa kipindi alichokaa madarakani tunaona kuna vitu vingi mno kavifanya katika kipindi hiki kifupi tena kafanya kwa uzalendo wa hali ya juu mno kwa mapenzi ya nchi yake.

Tuzidi kumpatia ushirikiano ili aendelee na huu moyo wa upendo na kujitoa kwa ajili ya watanzania.

Mama Samia watanzania tunakupenda mnoooo! Mungu akujalie maisha marefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…