View attachment 1733240
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,
Tumeona juhudi kubwa ulizofanya tangu ulivyoingia madarakani, unastahili pongezi kubwa, kama mtanzania nakuomba angalia sekta ya afya angalau ifikie level ambayo mtu ukilazwa na kufanyiwa operesheni ujue kuwa unaweza kupona. Nina maana kuwa operesheni za kawaida zinazofanywa Tanzania kupona ni kazi kubwa, wagonjwa wengi hawaponi, wanabaki na vidonda vya operesheni na wanakufa baada ya operesheni.
Mheshimiwa binafsi nafanya kwenye healthcare system (siyo surgeon) na nimeona watanzania wanavyoteseka na inaweza kukufanya ulie na ukae na huzuni maisha yako yote, sijui inakosewa wapi?
Nimefanya hospitali za rufaa zote za Tanzania lakini mheshimiwa rais vilio ni hivyo hivyo....WATU HAWAPONI.
Wengi wa watanzania hata kama wanahitaji operesheni wanaogopa kwa sababu uhakika wa kupona ni mdogo, siyo ugonjwa wenyewe bali kupona kutokana na procedures zenyewe.
Kuna tatizo kwenye hospitali zetu zote, na kubwa siyo vifaa bali ni ujuzi wa wataalamu na usafi, kuna shida kubwa ya sepsis, usafi ni tatizo na utumiaji wa vifaa, kuna vifaa vingi lakini hakuna waliofundishwa au waliopelekwa kozi na pia ufuatiliaji kama kweli wanafahamu.
Mheshimiwa rais, wizara ya afya imefanya kazi ya kusambaza vifaa na madawa lakini kilichokosekana ni UTAALAMU.
Navyooelewa kupeleka watu kuwafundisha haigharimu sana, hata kama ni gharama, basi kuna umuhimu wa kuwaleta wataalam wa kuwafundisha wataalam wetu hapa nyumbani na kuhakikisha wanaiva ili kuokoa maisha ya watanzania.
Mheshimiwa rais, tungekuwa na utaratibu wa kufuatilia wanaotibiwa hospitali zetu hasa surgeries, tungeweza kuona idadi kubwa ya wagonjwa ambao hawajapona au wamefariki. Mheshimiwa rais kuna shida kubwa sana na wenzetu huko mahospitalini wakiona huponi wanafukuza wagonjwa haraka haraka.
Mheshimiwa rais, haya mambo yapo wazi wazi na watu wamekuwa sugu, hawajali. Hayo yaliyotokea Bukoba ni tone la maji tu katika bahari.....yapo mengi.
Ushauri wangu:
1. Wataalam waendelezwe ili waweze kutoa huduma bora zaidi
2. Wagonjwa wanaopewa huduma ya operesheni na za kawaida waangaliwe ili serikali na wizara iwe na data zao kuona kama wamepona au la.
3. Ujenzi wa mahospitali na vituo vya afya ni muhimu, lakini pia viwekwe vifaa vyote vinavyohitajika na wataalamu wa kutumia wafundishwe. Majengo pekee hayatoshi mheshimiwa rais, tuna Mloganzila hospitali ya gharama lakini imekosa wataalamu wa maana, hawana ujuzi.
4. Kuwe na hospitali angalau mbili zenye uongozi wa madaktari mabingwa wa nje, kutoka kwenye nchi kama za Marekani, Uingereza, Ulaya na hata Cuba, ambazo zitakuwa za kulipia (siyo gharama kubwa), hizo zitakuwa na specialized treatments. Kuna shida sana za madaktari wazawa, bado tupo nyuma sana kwenye technology....Tupo nyuma sana. Hiyo itatupa changamoto pia kufanya vizuri kwenye hospitali hizo za rufaa na pia italeta health tourism.
Mheshimiwa rais, tunaweza kunyanyua huduma zetu za matibabu na tukafanya vizuri kwenye ukanda huu. Tunaofanya kazi huku tunajua weaknesses za system yetu, lakini tunaweza tukafanya vizuri sana kama tutatenga hospitali bora zaidi zenye wataalam wengi wa kutoka nje waliobobea na wanaofanya kazi nzuri kwa kuzingatia ethics za kazi. Kwetu sisi itatuchukua miaka mingi tuwe na discipline ya kazi.