Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Unajua maana ya syndicate?

Pia kuna shida gani mtu akinywa na marafiki zake nje ya muda wa kazi?
 
Uongozi ni dhamana na inatakiwa kuwatendea wote unaowaongoza sawa. Imezuka tabia ya baadhi ya watu kujipenyeza kwa viongozi na kujenga urafiki kwa maslahi yao binafsi.
Mama ameonya na anajua anachosema. Kama mtu unataka kuwa private, usifanye kazi kwenye ofisi za umma. Rais anajua fika wapi watu wanatengeneza mauzauza tunayoyaona...ni katika hizo nyama choma na party za marafiki
 
Wapi duniani viongozi hawaruhusiwi kuwa na marafiki?

Wewe hauna marafiki? Hao viongozi unaotaka wasiwe na marafiki ni binadamu kama sisi au wameshushwa special kutoka mbinguni?

Kuna namna unaweza tengeneza mfumo mzuri tu wa kuzuia conflicts of interest kwa viongozi na marafiki zao

Mfano kwa Uingereza - Kiongozi wa umma kama ameitwa kwenye kikao cha biashara na mfanyabiashara ni lazima a declare kikao hicho na mahala kinapofanyika kwa ethics Committee

Unaweza kuweka mifumo mizuri na mambo yakaenda vizuri tu sio kuwakataza watu kuchoma nyama na kunywa mvinyo

Nyerere alivyoweka Leaders clubs kwa ajili ya viongozi na Officers mess hakuwaga na akili au?
 
Naungana na raisi lakini ni ngumu kuzuia hilo na haiwezekani.
Amos makalla akiwa na birthday ya mwanae ni lazima atachoma nyama na kuwaalika rafiki zake.
 
Wapi duniani viongozi hawaruhusiwi kuwa na marafiki?

Wewe hauna marafiki? Hao viongozi unaotaka wasiwe na marafiki ni binadamu kama sisi au wameshushwa special kutoka mbinguni?
Naungana na raisi, lakini hili la party haliwezekani. Mkuu wa mkoa ana ndugu na jamaa, akialikwa kwenye sherehe ni lazima atahudhuria na akihudhuria lazima atakua karibu na ndugu na marafiki zake
 
Naungana na raisi, lakini hili la party haliwezekani. Mkuu wa mkoa ana ndugu na jamaa, akialikwa kwenye sherehe ni lazima atahudhuria na akihudhuria lazima atakua karibu na ndugu na marafiki zake
Mambo ya kishamba tu

How comes unanizuia kuchoma nyama hata nyumbani kwangu na kualika marafiki zangu? Huu utakuwa ushamba na utumwa
 
We mfuasi wa jiwe Huo ushauri peleka chato
 
Moderators tendeni haki please! huu uzi unajitegemea na haustahili kuunganishwa na uzi mkuu wa maoni na ushauri
 
Anaweka vizee vya kipemba huku bara kwa kuviteua wakati havina uwezo wowote. Jana kakiapisha kizee fulani kipemba eti ilikua karibu atemwe ndio kampa uteuzi. Halafu anajidai hana upendeleo anafuata uwezo...shwain. eti tumsamehe, wala hatumsamehi tunasubiri 2025 kumtema kama bigjee.
 
Soma Biblia Mwanzo 2:18, 21-23
 
Mama taarifa kaipata hapa, tusubiri nini kitafuata!
 

Attachments

  • _20220802_122026.JPG
    228.1 KB · Views: 18
Nani kasema viongozi wanakatazwa kuwa na marafiki? Hizo nyama choma na kula bata, halafu kugawiana deal ndio urafiki?
Unafikiri walioondoshwa wameonewa? Ukiona mtu kwenye TV anavyogombeza watu unaweza kufikiri kuna kitu serious...kumbe ntu wa deal.
Urafiki wetu mwingi kwenye siasa za bongo hauna afya kwa jamii iliyo kubwa. Umejaa kujenga mazingira ya kula kwa nafasi tu
 
Naungana na raisi lakini ni ngumu kuzuia hilo na haiwezekani.
Amos makalla akiwa na birthday ya mwanae ni lazima atachoma nyama na kuwaalika rafiki zake.
Ni ngumu mno. Unajua sababu ya ugumu wa kutekeleza sheria za maadili ya uongozi wa umma, kuna wengi wanaotumia hizo fursa kufanya mambo mengine yasiyo na tija kwa Taifa letu
 
Uwe unasoma comment nzima

Nimesema hapo juu namna ya kurekebisha hilo kimfumo na sio kukataza watu kuchoma nyama na kunywa mvinyo
 
Teuzi mh:Raisi zifanyike hata kwa wakulima pia hililinafya,maana ukiteua mkulima ukampeleka sehemu wanazolima mfano.Mapachichi,Mahindi nk,kwa uzoefu wake na shamba darasa tuapata mazao mengi vilevile na mapato ya sehemu husika na Taifa kwa ujumla yataongezeka.Pia hata kwa wafugaji na wafanyabiashara.Ahsante,Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kazi iendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…