Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan



Hilo la kupambana ili ukamilishwaji wa miradi ya mamilioni iliyoachwa na mtangulizi wake JPM ufikiwe hakika dada Samia ameupiga mwingi sana!

Unapoongelea SGR, Bwawa la Nyerere, Daraja la Busisi, majengo ya Hospitali za Kanda na ujenzi wa barabara zilizoanzishwa na mwendazake hakika unaongelea mabilioni ya Tsh ambazo kwazo pasipo na utashi wa kisiasa wa Samia isingeendelezwa abadani.

Kwalo, nakupongeza sana dada yetu Samia.
 
Reactions: Ame

Ila chawa kazi mnayo, mpaka najiuliza kati ya chawa wa Magufuli na wa mama nani zaidi.
 
Kwa hapo anasimamia vizuri ile dhana ya katiba ya sasa ya VP kuwa Rais kama Rais ataondoka kwenye kiti chake kwa kuumwa au kufariki...Anaendeleza maono ya kilichopigiwa kura na wananchi...Hongera sana Mh. Rais kwakusimamia katiba ya nchi yetu kama ulivyoapa
 
Kwenye hii awamu uchawa hauna mipaka wala kiwango cha elimu. Ni kama kuna ushindani kati ya machawa wa wasanii na wateule wa Rais. Kila mteule afunguapo mdomo ni kumsifu Rais kwa hili na lile.

Nami nageuka chawa, kwa leo tu lakini. Namsifia mama mpaka anune.

1. Hapa Kahama juzi kati kulikuwa na hali ya hewa nzuri, jua sio jua baridi sio baridi. Hongera mama kutuletea hali ya hewa unyama kama hii.

2. Simba Sc tumetinga makundi Africa. Wanaosema ni kazi ya Phiri na Chama mnajidanganya. Hiyo ni kazi ya awamu ya 6 chini ya Mweshimiwa Samia. Popoooo poooo eeeeh Kidedeaaa. Mama waangalie na Yanga waingie makundi shirikisho. Yanga wakae wakijua bila mama hawataweza.

3. Shemeji yangu alisumbuliwa sana na miguu. Wiki hii akaenda MOI wakamponyesha. Mimi na madaktari tunamsifia mama kwa kuwaleta madaktari na kuwapa mishahara.

4. Kuna dalili za mvua kuanza mapema. Wakulima tuongee na mama mvua zije vizuri tuvune vizuri. Tufanye fasta tusisubiri mpaka Bashe Hussein aende.

5. Huku Kigoma barabara ilikuwa inasua sua kuisha. Mama akaambiwa tatizo ni hela. Palepale akachukua card ya ATM akachota hela barabara itaisha hii.

Kama una kitu cha kumsifia Mama uwanja upo hapa. Mama anaupiga mwili.
 
Jana ninebet na mkeka wangu umetiki aisee shukrani sana kwa mama samia kwa kufanikisha malipo yngu nimepewa pesa yngu cash bila longolongo hongera mama saMia
 
Mkurugenzi wa Medichecks Polyclinics Dr. Philip Kahema Fimbo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia mpango wa Serikali yake wa kutoa huduma za Afya bure kwa wananchi wote pamoja na kutoa Bima za Afya kwa kila Mtanzania.

Dr. Fimbo amesema kuwa mpango huu unakwenda kuwahakikishia Watanzania usalama wa afya zao kwasababu wengi walikuwa wakitumia gharama kubwa kwenye kupata huduma za Matibabu na vipimo na wengine kushindwa kabisa kupata huduma hizo kwasababu ya kukosa fedha pindi wapatapo maradhi.

Dr. Fimbo amewataka wataalamu kuratibu vema mpango huu ili adhma njema ya Serikali katika kuwaletea Watanzania huduma bora za Afya iweze kufikiwa vema.

Mwisho Dr. Fimbo amewaomba Watanzania kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu ina dhamira njema ya kuleta maendeleo kwa Watanzania!
 

Attachments

  • IMG-20221022-WA0076.jpg
    27.3 KB · Views: 24
Acha KABISA juhudi za kuutafuta urais wa 2025,utajisababishia matatizo makubwa Sana mkuu!!

Maliza kalee wajukuu, wakina shein wasikuponze!!

MUNGU ibariki Tanzania
 
Ninashauri nchi hii tusimamie haki za Raia hasa inapotokea mgogoro wa ARDHI dhidi ya Raia wa Tanzania na mgeni ambaye anaishi inchini bila kufuata taratibu zilizopo kwenye sheria.

Nimeshuhudia matukio zaidi ya manne ambapo Raia wa nchi nyingine anafanya Mipango Kwa kutumia viongozi wasio waaminifu na kumilikishwa Ardhi Tanzania na KULETA usumbufu mkubwa na kila kesi inakuwa ngumu kwakuwa wanao uwezo wa kuwanunua watoa haki wasio na chembe ya uzalendo mfano Kigoma,Mara,Songwe na Mtwara.

Mfano Kuna Mama mmoja amezaa na Raia wa kigeni ambaye Hana kibali cha kuishi Nchini na alikuwa tegemezi Kwa huyo mama na alimkuta akiwa na nyumba yake lakini baadaye mlowezi huyo akaanza KUMPIGA na kutaka aondoke akidai yeye ndiye mwenye nyumba hiyo eti tu kwasababu wamezaa naye kesi ilipokwenda Mahakamani Hakimu aligeuka wakili na kumsaidia kuandika madai ingawa yote yalikuwa ya uongo na hayakuwa na mashiko kisheria kesi iliamriwa Kwa haki katika mahakama za juu.

Wahamiaji haramu walifikishwa Mahakamani Mkoa Songwe walipatikana na vitambilisho vya NIDA,MIKATABA ya mauziano ya Ardhi lakini hukumu ikawa condition discharge! Yaani Raia anayeishi Nchini bila kibali anapewa ADHABU ya kifungo cha nje! na alirudishiwa vielelezo vyake vyote alivyovipata kwanjia zisizo halali! Mbaya zaidi wakamwambia mtuhumiwa kwamba waliotoa taarifa ni watu kadhaa ili waonekane kwamba wao ni wema Kwa GHARAMA ya kusingizia watu wa karibu.

Kigoma Raia wa kigeni aliingia mgogoro ulioshindwa kutatuliwa Kwa haki na kupelekea kifo Kwa Raia wa Tanzania.

Mtwara Raia wa kigeni alifanikiwa kununua Ardhi na kuitumia Kwa matumizi ambayo ni kinyume na sheria za nchi lakini hakamatiki!

Kwa ujumla ninashauri pamoja na kuthamini haki za watu bila kujali au Kuwa na ubaguzi lakini ni Muhimu kusimamia IPASAVYO sheria za nchi dhidi ya wahamiaji ambao hawataki kufuata sheria na kuleta madhara Kwa wapiga Kura wa nchi hii.Nawasilisha Tafadhali nitaandaa nakala pamoja na ushahidi Kwa Mamlaka husika Kwa hatua zao.
 
Nafuu zilizotolewa kwa wakulima toka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu:

1. Kaondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mbolea ya ndani.

2. Kaweka ruzuku kwenye mbolea ya nje ishuke bei.

3. Bei ya mbegu ina ruzuku ishuke bei

4. Riba ya mikopo ya kilimo imeshushwa.

Kama haitoshi ametafuta fursa za masoko China na Uingereza kwa bidhaa za Tanzania kuingia bila kodi.
 
I stand to be correct

Mama
peponi moja kwa moja

kwanini nasema hivi Life is Good than ever , peoples are getting 💰

No kidnapping
No Economic sabotage cases
No bullet

Dear Mama :- Nothing I can pay you back but I Appreciate ( I understand) free

this is why when our fake Father passed away We didn't cried
japo s .Gang , they say we are heartless
 
Salaam mama Samia S. Hassan.
Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Ya Ulinzi Na Usalama.

Ninapenda kusema yafuatayo nikiwa kama mwananchi na kijana wa Kitanzania.

Mosi, Ninakiri kwa dhati ya moyo kwamba Matumaini na unafuu wa fikra na Mioyo ya wengi haswa vijana yanaonekana na yameshamiri.
Ingawa umepokea kijiti au kiti kukiwa na migogoro na sintofahamu za kiafya na kiuchumi Duniani. Lakini bado kwa kijana mwenye kujishuhulisha na mwenye malengo binafsi ya muda mfupi na muda mrefu anaona wepesi na ulaini wa maisha haswaa siku za usoni.

Pili Nchi imefunguka. Tanzania imeondolewa na inazidi kuwekwa kwenye nchi za maana na muhimu kimataifa. Tumejifunza kwamba hakuna mtu mwenye mambo mema na mwema anaetengwa au kujitenga na watu au jamii au Jumuiya ya kimataifa. Tunapenda kufika mbali hivyo twende na wengine. After all Dunia ni so liberal now days hakuna mtu analazimisha mwingine au taifa lingine kufanya mambo wasioyataka au yasiyona faida ama yenye madhara. Na still kuna nafasi ya ku balance mambo mpka kila mmoja aridhike. Lakin si kujitenga na kujifungia ndani.

Tatu na mwisho ni ombi, ninaomba pamoja na mapinduzi makubwa ya kiuchumi na miradi mikubwa na kupromote kilimo na utalii.
Naomba uongeze muda kwa vijana waliomaliza vyuo. Maana hata fedha nyingi za mikopo unazowawezesha kusoma elimu ya juu. Bila ajira nadhan hazitarudi kwa muda sahihi. Pia inakatisha tamaa sana na yeyote ajaribu kuvaa viatu vya unemployed person ni vya moto kama tanuru. Tangu awamu ya 5 nilikuwa nawaambia watu ukiajiri vijana 10 umesaidia familia 10 kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Pamoja na jitihada za wazi kabisa za serikali kuajiri ila impact bado haijaenea sana kwa kuwa imekuwa miaka zaid ya 6 ni kama hakukuwa na ajira kwa kisingizio cha SGR, Bwawa la nyerere na miradi mingine. Mikubwa.

Kwa vile serikali yako na wewe mwenyewe mara kadhaa umekiri maendeleo lazma yamguse mwananchi yasiwe ya mavitu makubwa huku bibi kule urambo au Kagera akikosa raba ya kuvaa au sabuni ya kuoga kisa kamlipia mwanae ada kauza kila kitu alaf hajaajiriwa.

Ninazidi kukupongeza Mhe. Madam President.
Mungu akupe maisha Marefu sana sana kama Mama maria nyerere ama Mzee Ruksa.
Amin.
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasan ajitahidi kuhakikisha vijana wanapata mikopo kutoka halmashauri kutokana na suala la ajira kuwa changamoto. Kuna vijana wengi wana mawazo mazuri na nia njema ya kuwekeza ili kuinua uchumi wetu kwa pamoja. Hivyo ajitahidi sana kuhakikisha mikopo inapatikana kwa wakati na bila urasimu wowote.
Vinginevyo kutakuwa na ongezeko kubwa la vijana wenye matatizo ya afya ya akili pamoja na uhalifu ambao ungeweza kudhibitiwa kwa watu kufanya kazi au kujishughulisha.
 
Ushauri Mh. Rais apenyeze wachunguzi kwenye taratibu za kuwatambua wanasheria wa serikali ambao wamenyimwa vibali kutokana na ukiritimba na urasimu.

Bunge lilipisha sheria kuhusu upatikanaji wa wanasheria wa serikali ikiwa na lengo zuri ambalo wasiovaa miwani hawawezi kuona. Baadhi ya watendaji wa hovyo walisisimamia mchakato wa kibaguzi na upendeleo na kuchagua wanasheria kiduchu, jambo linalodunisha azma ya Bunge na serikali ya kuandikisha wanasheria walioajiliwa na serikali kutumikia tasnia yao ya sheria katika idara mbalimbali za serikali. Badala yake, aibu inaendelea na mabadiliko hayo ya sheria kutokuleta tija.

Ni maoni yangu Mh. Rais apeleke jicho pale kwenye sheria ili apate kuokoa nchi hii na kuwawajibisha watendaji wasioitakia mema nchi hii.
 
Kwa kweli kwa sasa maji sisi watu wa ruvu maji kwa sasa mi ya kumwaga. Hongera mama .
Dawasco maji kwa sasa yana presha mpaka mabomba yanapasuka.hapa mtaaan mbez afrikana mfano bulembo Street bomba ina presha balaa.
 
Kwa kukilinda chama chetu cha mapinduzi; jumuiya zetu pamoja na sisi wanachama tunapaswa kuwa mstari wa mbele kuhoji au kukosoa pale tunapoona mambo hayako sawa. Tusiwe wapongezaji na wasifu juhudi tu, tunayo nafasi ya kuhoji pia.
Je, hili daraja lina thamani ya B. 7?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji117] Yaani limeenda saana ni 2.5 B
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…