Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Hilo la kupambana ili ukamilishwaji wa miradi ya mamilioni iliyoachwa na mtangulizi wake JPM ufikiwe hakika dada Samia ameupiga mwingi sana!
Unapoongelea SGR, Bwawa la Nyerere, Daraja la Busisi, majengo ya Hospitali za Kanda na ujenzi wa barabara zilizoanzishwa na mwendazake hakika unaongelea mabilioni ya Tsh ambazo kwazo pasipo na utashi wa kisiasa wa Samia isingeendelezwa abadani.
Kwalo, nakupongeza sana dada yetu Samia.