Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 8,996
- 6,927
MRADI MKUBWA KABISA WA KUANZA NAO NI.
[emoji3504]Kutuunganisha kama taifa.
Uzuri wa mradi huu ni kwamba hauna gharama kubwa ya matumizi ya rasilimali.
Mradi huu Hauhitaji wakandarasi, unahitaji utashi na maamuzi.
Hauhitaji upembuzi yakinifu na michakato, unahitaji meza ya duara tu.
Hauhitaji teknonlojia za kisasa, unahitaji hekima na busara kutoka vichwani,moyoni na vinywani.
Mengine yote Kama Treni ya umeme, umeme mto rufiji, barabara, madaraja, hospitali, maji, elimu bure n.k iwe mwendelezo alipoishia Hayati JPM Ni rahisi Sana kuyatekeleza tukiwa wamoja wenye Ari, nguvu, umoja na kupendana
#UmojaNiNguvu
Aisafishe wizara ya Afya mapema sana,Mradi huu ni bora uende sambamba na kuwa na mwongozo mpya kuhusiana na Corona.
Gonjwa hili linatupotezea watu muhimu sana kwa ujenzi wa nchi hii.
Gonjwa hili linatupotezea raslimali nyingi kushughulika na misiba.
Aisafishe wizara ya Afya mapema sana,
Dr Gwajima arudi wodini akatibu wagonjwa,na naibu wake arudi bungeni pamoja na katibu wao fyekelea mbali.
Tupime corona na kutoa elimu ya kutosha.
Chanjo ichunguzwe kama inafaa haraka iingie kwenye matumizi
Ngoja tuone kutaendaje...
MRADI MKUBWA KABISA WA KUANZA NAO NI.
[emoji3504]Kutuunganisha kama taifa.
Uzuri wa mradi huu ni kwamba hauna gharama kubwa ya matumizi ya rasilimali.
Mradi huu Hauhitaji wakandarasi, unahitaji utashi na maamuzi.
Hauhitaji upembuzi yakinifu na michakato, unahitaji meza ya duara tu.
Hauhitaji teknonlojia za kisasa, unahitaji hekima na busara kutoka vichwani,moyoni na vinywani.
Mengine yote Kama Treni ya umeme, umeme mto rufiji, barabara, madaraja, hospitali, maji, elimu bure n.k iwe mwendelezo alipoishia Hayati JPM Ni rahisi Sana kuyatekeleza tukiwa wamoja wenye Ari, nguvu, umoja na kupendana
#UmojaNiNguvu
Sasa ukabila gani ndugu mbona una mawazo potofuTukamilishe SGR kuelekea Kigoma badala ya Mwanza.
Mwanza hakuna biashara ya Shirika la Reli Tanzania, TRC.
Miradi iliyolenga Mwanza ilichochewa na Ukabila badala ya vigezo vya uchumi.