Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

JPM aliambiwa atawale mpaka mwisho wa maisha yake kumbe mwisho wa maisha yake ulikuwa kwenye utawala wake. Ni Mungu tu.
 
Muda mchache ujao utasikia baadhi ya wabunge wanawasilisha hoja bungeni ya kutaka kipengele cha katiba cha ukomo wa rais kirekebishwe ili mama aendelee kwasababu anaupiga mwingi. Enzi za magu hoja kama hizi pia zilianza kujitokeza bungeni
 
Mtasababisha historia ijirudie.
Magufuli alikuwa anaongoza kwa amani mpaka watu walipoanza kusema kwa nini asiendelee milele.
Rais huyu hapendwi na wananchi.
Akienda kuhutubia Mkutano wa hadhara inahitajika battalion au zaidi ya battalion ya askari kumlinda.

Hata akiambiwa Nyerere alikuwa anapita barabarani na gari moja ya doria mbele na gari moja ya walinzi nyumba, hawezi kuamini.

Lakini yote hii tisa tisa bado kumi.
Yale mambo aliyojuwa anasema juzi Heche ni quite interesting.
Kwamba hela zinakopwa na nchi kujenga miradi ya maendeleo.
Lakini Kwa kila shilingi inayotumika kujenga barabara,ipo shilingi inakwenda katika akaunti ya mtu binafsi.

Ugomvi wangu na watu kama Heche ni kwamba hizi siri wanazijua toka zamani isipokuwa mpaka wakiona Samia hana mpango wa kuwagawia hela ndio wanatangaza.

Lakini siyo rahisi kwangu ku comment kuhusu mambo ya Ikulu.
Mambo siku hizi yanafixgwa sana. Everything is shrouded in secrecy.
Every once in a while anatokea mtu anasema Rais Samia amefariki.
Basi tu,imekuwa kwamba this government takes great delight in being mysterious.

Lakini kuwa na viongozi Tanzania matajiri kama Weakness Chivayo mimi naona ndiyo weakness ya hii serikali.
 
■ Rais Samia Suluhu Hassan aelekeza Tanzania kutumia nafasi yake ya kimkakati kuvutia uwekezaji wa kimataifa.

■ Waziri Mkuu aielezea Dar es Salaam kama lango la biashara linalounganisha Afrika na masoko ya dunia.
HUum339XYAEtwFn.jpg
 
Hii mipango ya namna hiyo kuilinda na kuitekeleza tunahitaji utawala wa kifalme.
Juzi kaja Raisi anaamini ktk reli ya SGR umeme wa uhakika na kujitegemea

Kesho anakuja raisi mwingine mwenye maono tofauti na raisi aliymaliza muda wake akija mwingine na yeye ana maono tofauti

hii inazorotesha maendeleo ya nchi.

Kule Morocco kuna utawala wa kifalme na wanasonga mbele kimaendeleo hata kwenye michezo
 
picha kuu ya mbele ya gazeti, Raisi, Makamu wa Rais na Waziri mkuu
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
We pray for our state.
 
Back
Top Bottom