Wakuu,
Kabla ya mada husika, tusisahau kuendelea kuukataa mkataba wa bandari. Ni mkataba wa aibu kwa Taifa letu.
Twende kwenye mada, Mh Rais Samia na serikali yake wamefuta obligation kwa makampuni ambayo hayakuwa na sifa za kulipa kodi ya SDL ku fill returns. Hili kwa haraka unaweza kufikiri ni dogo lakini limeumiza wengi sana.
Mtu anafungua kampuni na ameajiri msaidizi mmoja bado akiwa na mtaji mdogo lakini baadae anakutana na fine and penalties kwa kuto fill SDL returns ambayo hana sifa za kuilipa. Inabidi awe na mhasibu ku fill nil returns kila mwezi.
Hii ni moja ya usumbufu wa kikodi uliochelewa sana kufutwa.
Asante sana mama Mh Rais Samia!
MKATABA WA BANDARI HAUFAI! UFUTWE AU UREKEBISHWE!