Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hakuna wizara ambayo hujaiongeza bajeti.
Swali la kujiuliza chanzo cha ongezeko la bajeti limetokana na uzalishaji mali nchini na kuuza mali hizo Nje ya nchi kwa wingi au ni njie nyingine ambayo si endelevu?
 
Ee Mungu tunashukuru kwa ulinzi wako. Tunaomba utujaalie baraka jumapili ikawe njema kwetu. Kipekee tunamuombea mh Rais mama yetu kipenzi aendelee kuwa mwenye afya njema Amen. Mkawe na asubuhi njema
 
Mama aelekeze na hili likatizamwe; ni hivi; aliyemuachia viatu vya uongozi amemuachia wanaolalamika kukosa ongezeko la mshahara kwa kutopandishwa vyeo walivyostahiki mnamo mwaka 2019, hao ni walioajiriwa mwaka 2014.
 
Wakuu,

Kabla ya mada husika, tusisahau kuendelea kuukataa mkataba wa bandari. Ni mkataba wa aibu kwa Taifa letu.

Twende kwenye mada, Mh Rais Samia na serikali yake wamefuta obligation kwa makampuni ambayo hayakuwa na sifa za kulipa kodi ya SDL ku fill returns. Hili kwa haraka unaweza kufikiri ni dogo lakini limeumiza wengi sana.

Mtu anafungua kampuni na ameajiri msaidizi mmoja bado akiwa na mtaji mdogo lakini baadae anakutana na fine and penalties kwa kuto fill SDL returns ambayo hana sifa za kuilipa. Inabidi awe na mhasibu ku fill nil returns kila mwezi.

Hii ni moja ya usumbufu wa kikodi uliochelewa sana kufutwa.

Asante sana mama Mh Rais Samia!

MKATABA WA BANDARI HAUFAI! UFUTWE AU UREKEBISHWE!
 
these are petty isues....kuuza nchi hizo shughuli watazifanyia wapi?
 
Je, hicho alichofanya ndio suluhisho la kudumu juu ya tatizo husika? Kwa nini hautafakari kwa kina na kumshauri Rais afikirie kuifuta Sheria mbaya na kandamizi iliyopelekea kuanziahwa kwa hilo tatizo ambalo wewe unaliona kama kero na kikwazo kwa wafanyabiashara wengi?
Kumbuka ya kwamba, unapotaka kufanya uamuzi au jambo la kudumu ni lazima uzingatie sababu za kudumu ktk kufanya uamuzi wako.
 
Kwahiyo usumbufu wa kuzikorokochowa EFD zetu haupo Tena?
 
Kampuni zote sasa hivi zina EFD, sasa kama hakuna oparesheni na ninalipa provisional tax bado naendekea kujaza returns nil?
Kama hakuna operations unatakiwa uwe una print nil Z report kwenye machines. Kama unaona ni usumbufu unatoa taarifa rasmi TRA Kama biashara imesimama.

EFD haina returns labda kama ni VAT registered.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…