Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Pamoja na hayo poa raisi aondolewe kinga ya kushtakiwa
 
Utaambulia matusi humu...
Humu hawataki habari zozote nzuri kuhusu mazuri....sadists people only thrives in negativity
Haiwezekani msaliti atoe bure bandari zetu zote kwa wajomba zake halafu nije kumsifu kwa kutimiza wajibu wake.

Sadist ni huyo shangazi yako aliyetugeuza watumwa ndani ya mipaka ya Tanganyika yetu.
 
Haya ya SDL yeye hayajui na wala hana habari nayo. Unampa sifa za bure tu katika jambo ambalo yeye hahusiki kabisa kama ilivyo kwa hilo la Dubai.

Hata kama angejua na kuhusika na hiyo SDL; hiyo isingetosha chochote kumpa sifa ya aina yoyote kutokana na uzito wa DPW

Hata sielewi kabisa ni sababu zipi zilizofanya uone ni muhimu kumtaja yeye kwenye mada yako hii?
 

Hatusahau bandarini🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mh.Rais sina ninachokudai naiona dhamira yako sahihi ya kuwakomboa watanzania nikupe moyo Mungu atakusimamia.

Ushauri kwa hawa uliowapa mamlaka ya Kukimbiza Mwenge wanavaa mamlaka yako na kutoa amri za kutweza na kunyanyasa watumishi wa Umma. Mfano Mwaka Jana waliwaweka askari wa mkoa Mara mahabusu zaidi ya Siku tano kwakuwasingizia kwamba wamewatukana na kuna sehemu katika mkoa wa Mbeya waliwasemea uongo viongozi wa Polisi na kuleta usumbufu kwao na familia zao Leo tena wamemuweka mahabusu Dereva wa TRA kwa maneno hayohayo kwamba anataka kuwagonga yapo mengi hawa watoto wanayafanya kwa kiburi na kufanya mbio za mwenge wa Uhuru kuwa kaa la moto na kuondoa malengo yaliyokusudiwa.

Kama wanatumwa kuja kutishia watu na kuathiri ustawi wa watumishi basi jambo hili litazamwe upya maana litaondoa thamani ya Mwenge wetu.

Pia tuheshimu haki za binadamu watu wananitoa kushiriki mbio hizi alafu mshahara wake in kufokewa na kuwekwa ndani!!

Mimi nimeyaona na ninatoa ushauri na ushauri in hiari kuupokea au kuukataa.
 
Rais Samia, Mimi mwananchi wako, naishi huku Kigamboni, nakuomba Tuma Vijana wako wafuatilie kuona jinsi gani akina Mama wa Kigamboni wanavyofanywa na Benk ya CRDB na mwana siasa mmoja anaye itwa Lilian Wasira.

Huyu Mama amewaandikisha wamama kuwa wanachama cha NGO yake inayoitwa Citizen Foundation na kuwalazimisha kulipa ada ya Mwaka mzima kwakuwaahidi kuwapatia mikopo, cha ajabu walisulutishwa kulipa ada na kuahidiwa kukopeshwa na taasisi ya Boka microfinance, kilichotokea waliitwa waandishi wa habari na kushuhudia kisainiwa kwa makubaliano ya kuwakopesha wamama hao, pamoja na kukidhi mashart lakini waliitwa wachache tena kwa siri wakapewa mkopo na wengine wakiambulia patupu.

Mwezi mmoja uliopita akina Mama hao hao walikusanywa huko Mbezi beach, na maafisa wa CRDB Kibada na huyo Lilian Wasira kwa madai kuwa Benk hiyo itatoaka mikopo ya Mama Samia, lakini cha ajabu waliambiwa ili wapate mikopo hiyo shart walipe ada ya uanachama wa Citizen foundation akina Mama kwa dhiki kuu ya kujinyima ili wapate hiyo ada lakini hadi sasa huo mkopo wa Mama Samia hawajapata, na matumaini yamefuti.

Najiuliza hiyo mikopo ya Mama Samia haipatikani hadi ulipe ada ya Citizenshi Foundation? Akina Mama wameapa sababu Lilian Wasira ana mpango wa kugombea ubunge hatapata, kamwe sababu kinyume cha SHERIA, wamama wanaumizwa sana huku kigambini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…