Rais Samia, Mimi mwananchi wako, naishi huku Kigamboni, nakuomba Tuma Vijana wako wafuatilie kuona jinsi gani akina Mama wa Kigamboni wanavyofanywa na Benk ya CRDB na mwana siasa mmoja anaye itwa Lilian Wasira.
Huyu Mama amewaandikisha wamama kuwa wanachama cha NGO yake inayoitwa Citizen Foundation na kuwalazimisha kulipa ada ya Mwaka mzima kwakuwaahidi kuwapatia mikopo, cha ajabu walisulutishwa kulipa ada na kuahidiwa kukopeshwa na taasisi ya Boka microfinance, kilichotokea waliitwa waandishi wa habari na kushuhudia kisainiwa kwa makubaliano ya kuwakopesha wamama hao, pamoja na kukidhi mashart lakini waliitwa wachache tena kwa siri wakapewa mkopo na wengine wakiambulia patupu.
Mwezi mmoja uliopita akina Mama hao hao walikusanywa huko Mbezi beach, na maafisa wa CRDB Kibada na huyo Lilian Wasira kwa madai kuwa Benk hiyo itatoaka mikopo ya Mama Samia, lakini cha ajabu waliambiwa ili wapate mikopo hiyo shart walipe ada ya uanachama wa Citizen foundation akina Mama kwa dhiki kuu ya kujinyima ili wapate hiyo ada lakini hadi sasa huo mkopo wa Mama Samia hawajapata, na matumaini yamefuti.
Najiuliza hiyo mikopo ya Mama Samia haipatikani hadi ulipe ada ya Citizenshi Foundation? Akina Mama wameapa sababu Lilian Wasira ana mpango wa kugombea ubunge hatapata, kamwe sababu kinyume cha SHERIA, wamama wanaumizwa sana huku kigambini