Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan taarifa ikufikie kuwa mpaka hivi sasa Mwanao na Mzalendo Halisi wa Tanzania GENTAMYCINE nakuandikia hapa JamiiForums ni kwamba tayari Makampuni Sita ( 6 ) kutoka nchini Uturuki yaliyoko Mkoa wa Pwani na yalitokuwa yakiitumia Bandari yetu ya Dar es Salaam wameondoka na Kuhamia rasmi nchini Mozambique ( Msumbiji )
Kingine Mheshimiwa Rais kwa sababu zilizowatoa hao Waturuki ( ambazo nitazielezea kwa Kina mbeleni ) Mwekezaji mwingine kutoka nchini China ( mwenye Kampuni ya Good One ) anajiandaa kuhamia nchini Congo DR akitokea hapa Kwetu nchini Tanzania.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ufuatao ni sababu Kuu ambazo zimewakimbiza hao Waturuki na huyu Mchina...
1. Wakuu wa Mikoa kwenda mara kwa mara Kuomba Pesa.
2. Wakuu wa Wilaya kwenda mara kwa mara Kuomba Pesa.
3. Baadhi ya Askari Polisi na hasa hasa wale wa Barabarani ( Traffic Police ) kuwasumbua kwa Kuwaomba Rushwa kwa Mizigo yao wakiitoa Bandarini na Wengine hata Kutishiwa nao.
Mheshimiwa Rais Samia hawa Wawekezaji tajwa ( Waturuki na huyu Mchina ) wanasema Wao wanachojua Watu wanaotakiwa Kuwafuata ni TRA, NEMC na OSHA ila wanashangaa kwanini hawa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Police ( hasa Matrafiki ) wao ndiyo huwa wanawaendea na kutaka Pesa Kilazima?
KILIO
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa Wafanyakazi ( wa Kitanzania ) waliokuwa wakifanya Kazi kwa hawa Waturuki na huyu Mchina ( katika Makampuni yao ) wameshakosa Kazi ( Ajira ) na sasa wanajipanga kuzoea Maisha ya Jobless na Stress iliyozoeleka na Wengi.
Kuonyesha kuwa tayari Athari za kuhama kwa hawa Waturuki na huyu Mchina zimeanza kwa Wafanyakazi Wao ni kwamba hapo nyuma walikuwa Wakipakia / Wakijaza Kontena moja refu kwa Tsh 250,000/= na Maisha yao kuwa Mswano ( Mazuri ) ila kwa sasa Kontena moja refu wanalijaza / wanalipakia kwa Tsh 25,000/= za Kitanzania ambapo wakija Kugawana kila Mtu anaondoka na Tsh 3,500/= au hata Tsh 2,000/= huku wakiwa na Familia zao.
Mheshimiwa Rais Samia kwa mujibu wa Kauli zao ambazo wameniambia Mimi GENTAMYCINE wanasema kwamba kwa sasa ile Tanzania ya 2005 - 2015 ya Chukua Chako Mapema ( CCM ) imerudi na kwamba kuna Watu wachache ndiyo Wananeemeka na Rasilimali Keki ya Tanzania na Wengi sasa Wanataabika na Wataendelea Kutaabika.
Mwisho nimalizie tu kwa Kukuambia Mheshimiwa Rais Samia kuwa kamwe usitegemee Taarifa kama hii ukapewa na Watu wako ( Watendaji ) wanaokuzunguka Ikulu ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar kwakuwa 85% yao nao wamo katika hii Dhambi na Laana wanayojitafutia.
Nakuomba Mheshimiwa Rais Samia ukimaliza tu Kusoma huu Uzi wangu agiza Watendaji ( wale tu Unaowaamini na wana Maadili na Wazalendo wa Kweli kama Mimi GENTAMYCINE na hawana Unafiki wala Uwoga ) walifuatilie hili nililokuelezea hapa na ukikuta ni sahihi nakuomba usinipongeze kwa labda Kuniteua au kunipa Pesa ila nitakuomba tu Umshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kumuumba GENTAMYCINE na aendelee Kumbariki na Kumtunza ili awe na Jicho Kali la Ndege Tai ( An Eagle ) linaloangaza kila Pembe ya Nchi na Dunia na ambaye pia ni Mzalendo Halisi wa Tanzania .
Uwe na Majukumu mema Mh. Rais.