Kwasasa Bungeni kuna Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Waziri Mkuu mwenye Naibu Waziri Mkuu, Hongera ulimuondoa Katibu Mwenezi Mstaafu wa Chama.
Pia kuna Wabunge ambao wengi wao wanatuhumiwa kuwa ubunge walipewa tu bila kushinda na Wabunge hawa wanatoka Majimboni na wengi wao ni ama hawapatani na viongozi wa Chama au wanapatana nao na zaidi ya 60% ni Watanganyika ambao nafsi zao huenda zinawiwa kulipa fadhila. Aidha kwa upepo ulioko nje kwa Wananchi wengi wa wabunge hawa wanakuogopa kujinasibisha na wewe kisiasa.
Huku nje kuna DP World, Waraka wa TEC, Watanganyika, Sukuma Gang, na Chadema. Mpaka january Mwakani Mama Upinzani utakuwa mkali sana. Watu kama sisi tusiokuwa na unafiki ndio tutakusaidia. Tuendelee kunywa mtori.
Binafsi nilimpenda sana Magufuli na ninaona umeachana na mambo yake karibu yote. Nasikitika sana. Natamani urudi kwenye drawing board uanze upya