Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mtanikumbuka πŸ˜‚πŸ˜‚
Yule hafai kama ambavyo Makonda hafai kwenye nafasi ya Rais ila kwenye nafasi ya PM.

Nafasi ya Rais inahitaji mtu mwenye utulivi wa akili na anaweza kudhibiti hisia Ili asiimize watu.

Si umemsikia Makonda akidai Chuma angekuwepo angewavunka miguu ila anamuogopa Uungwana wa Samia?
 
Una hoja ila hapo ulipoweka wa "ujasiri wa kisukuma" sasa umeleta ukabila. Na sisi Wazaramo hatupendi ukabila atii. Mchango wa elimu, exposure na mengine aliyoyapitia unaweza kuwa umemfanya alivyo na sio usukuma wake. Ujasiri hauna kabila, Nyerere na Sokoine hawakuwa wasukuma ila ujasiri walikuwa nao.
 
Mimi naona kuhusu waziri mkuu wetu kipindi hiki bado anafanya vizuri na tuendelee kumpa nguvu,kumuunga mkono na kumpa ushirikiano ili amalize salama. Ni msaidizi wa Mheshimiwa Rais wetu na hata tunapomsifia na kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kuwa amefanya vizuri ni ngumu kutompa pongezi zake waziri mkuu wake ambaye amekuwa akipita huku na huku kufanya kazi anazoagizwa na mheshimiwa Rais pamoja na kufanya mengine mengi yaliyo ndani ya uwezo wake.

Lakini pia Mheshimiwa waziri mkuu wa sasa amefanya kwa sehemu yake kama mwanadamu na kama kiongozi.ikimbukwe ya kuwa serikali ni kama timu tu ambapo viongozi wetu wanahitajiana sana katika kutekeleza shughuli za kimaendeleo.kumbuka huwezi ukawa kila mahali kwa wakati mmoja.hivyo ili uonekane bora ni lazima na wachini yako wawe bora, watekeleze vyema majukumu yao na waache kufanya kazi kwa mazoea.

Pili katika mawaziri wachapa kazi nakubaliana na hao uliowataja lakini mimi siwezi kuacha kuwataja na kutambua mchango wao watu kama Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba.hawa ni ngumu sana kuwaacha katika list ya wachapa kazi na waliofanya kazi vyema kabisa katika kutekeleza majukumu yao.

Mfano kama huyo mheshimiwa Ummy Mwalimu mimi namuona kama kiraka ambaye unaweza mpeleka wizara yoyote ile unayotaka wewe na akafanya vizuri sana. Hata Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba naamini naye ametumia vyema sana taaluma yake ya uchumi kutoa ushauri mzuri kwa serikali na Rais wetu katika kujenga uchumi imara na shirikishi.ndio maana tunaona kwa sasa hali ya mfumuko wa bei siyo mkubwa,hali ya uchumi na miradi ya kimkakati inaendelea kujengwa ambayo siku za mbele italeta faida kubwa sana katika uchumi wetu.mzunguko wa fedha ni mzuri sana ambapo kwa mwaka ulioisha inaonyesha ulikuwa mzuri sanaa.

lakini pia mimi naamini mawaziri wetu kwa kiasi kikubwa sana wametekeleza vyema sana majukumu yao na ndio maana kuna maendeleo katika kila eneo na kila sehemu.kwa kuwa kama wasingefanya vizuri lazima tungeona kupwaya katika eneo fulani.

Lakini pia kila wizara ina namna ya kuongoza. Mfano wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa ni wizara ambayo haihitaji makelele ya waziri au mwanasiasa yoyote yule kwa kuwa mambo huko yanakwenda kikanuni na siyo matamko tamko tu.kwahiyo katika wizara hii huwezi ukasema kuwa waziri wake hafanyi kazi kwa kuwa yupo kimya .inakuwa siyo sawa na nikumuonea tu na hata usipomuweka katika wachapa kazi unakuwa unamvunja moyo na kumkosea. Huu ni mfano tu.

Kwa hiyo kikubwa tuwatie moyo mawaziri wetu wote na tutoe ushauri pale tunapoona inafaa kufanya hivyo.lakini mimi naamini wamefanya kazi kubwa na kujitahidi sana kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania.baraza la mawaziri ni kama timu.ambapo wakati mwingine usilazimishe kufunga wewe wakati upo eneo ambalo ukitoa pasi kwa mwenzako itakuwa rahisi zaidi kufunga kuliko wewe.

Ni lazima serikali yetu ifanye kazi kama timu mmoja na iwe na mawasiliano ya kiutendaji kuanzia juu mpaka chini huko na sifa tuwape wote kwa pamoja.tukumbuke hapo hapo kuna makatibu wakuu ambao nao wanakesha wakifanya kazi ili kumfanya waziri apate majibu ya kujibu kwa watu.
 
Nimesema ujasiri na uthubutu wa kuwasukuma Mawaziri wenzie sio ujasiri wa kisukuma
 
Bado hujasema

Makonda Go.....Go.... Go.... hallelujah πŸ˜€
 
Wasukuma ni watu wa hovyo sana!
 

Waziri mkuu aliye mwenye jina fake? waziri mkuu ambaye kapigwa marufuku kuingia nchi nyingine! waziri mkuu mwenye kashfa ya kutaka kumuua Lissu tuache ndogo za mchana
 
Waziri mkuu aliye mwenye jina fake? waziri mkuu ambaye kapigwa marufuku kuingia nchi nyingine! waziri mkuu mwenye kashfa ya kutaka kumuua Lissu tuache ndogo za mchana
Hayo yanazungumzika Kidiplomasia na hizo embango zinaweza ondolewa.

Mambo ya majina fake etc sio Dili sana Bali uwezo wake na ujasiri wake ndio muhimu.
 
Hayo yanazungumzika Kidiplomasia na hizo embango zinaweza ondolewa.

Mambo ya majina fake etc sio Dili sana Bali uwezo wake na ujasiri wake ndio muhimu.

Tuache ujinga yaani tuache watu wa maana tukachague wauaji. Jamaa ana kesi mpaka za kutaka kupora watu mali zao hasa wahindi. Kama ni chawa hongera kwa kazi maana vijana wa siku hizi hamna ubunifu kabisa.
 
Wenye akili wameshaona na nyie watu anaowatuma humu mnathibitisha maneno ya wenye akili.


Hizi ziara ni za kujibrand yeye wala sio Taasisi na mbaya zaidi zinazidi kuonyesha jinsi gani waafrika tulivyokosa akili as badala ya kushughulikia mifumo thabiti hasa checks and balances tunashughulikia kuwabrand watu ambao hawana lolote la maana zaidi ya kuwa ma populist tu
 
Tuache ujinga yaani tuache watu wa maana tukachague wauaji. Jamaa ana kesi mpaka za kutaka kupora watu mali zao hasa wahindi. Kama ni chawa hongera kwa kazi maana vijana wa siku hizi hamna ubunifu kabisa.
Weka ushahidi wako wenye uthibitisho kwa hayo unayozungumza na siyo kuandika tu bila ushahidi wa aina yoyote ile.
 
Jingalao hoja moja ngonjera nyiiiiingi kama unaolewa au unaomba posa jombaa
 
Kumbe na wewe una qkili kubwa namna hii?
 
Nimetoa tusi, wewe tu ujiulize ni tusi gani, halafu ndio hilohilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…