Ukimsikiliza Makonda unaona kabisa ana uelewa na uthubutu wa kusukuma mambo ya msingi.
Mh.Rais Samia kama hutojali wewe Mteue Makonda awe Waziri Mkuu wako baada ya 2025.
Anaweza kuwasukuma Mawaziri wakawa wanashughulikia kero kama anavyofanya kulingana na ratiba ambayo atawapangia then wewe utapumua.
Baadhi ya mambo Kwa Sasa hayaendi Kwa sababu PM wa Sasa hana ujasiri wa kuwasimamia Mawaziri wenzake.
Ukiangalia kwenye Serikali Yako Mawaziri walau wanafanya kazi ya dhati ya Kumsaidia Rais ni
Bashungwa, Mchengerwa,Mavunde,Ulega,Aweso,Bashe na Naibu wa Uchukuzi.Waliosalia utawaona kwenye matukio tuu.
View: https://youtu.be/VpKhMRf7Oe4?si=0XsIzlSOD8QBIXaQ
Pili tubadili Muundo wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Ili wawajibike zaidi,Kwa sababu haiwezekani kero zimejaa na miradi imekwama na wao wapo na hawachukui hatua.Tuwape Nguvu za kimaamuzi Kwa kubadili muundo wa nafasi zao.
Mwisho Kwa Makonda umecheza kama Pele.