Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mnawaza uchaguzi wakati TAIFA liko GIZANI? Daaah ona chawa n madalali.
 
Huju
Ukimsikiliza Makonda unaona kabisa ana uelewa na uthubutu wa kusukuma mambo ya msingi.

Mh.Rais Samia kama hutojali wewe Mteue Makonda awe Waziri Mkuu wako baada ya 2025.

Anaweza kuwasukuma Mawaziri wakawa wanashughulikia kero kama anavyofanya kulingana na ratiba ambayo atawapangia then wewe utapumua.

Baadhi ya mambo Kwa Sasa hayaendi Kwa sababu PM wa Sasa hana ujasiri wa kuwasimamia Mawaziri wenzake.

Ukiangalia kwenye Serikali Yako Mawaziri walau wanafanya kazi ya dhati ya Kumsaidia Rais ni

Bashungwa, Mchengerwa,Mavunde,Ulega,Aweso,Bashe na Naibu wa Uchukuzi.Waliosalia utawaona kwenye matukio tuu.

View: https://youtu.be/VpKhMRf7Oe4?si=0XsIzlSOD8QBIXaQ
Pili tubadili Muundo wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Ili wawajibike zaidi,Kwa sababu haiwezekani kero zimejaa na miradi imekwama na wao wapo na hawachukui hatua.Tuwape Nguvu za kimaamuzi Kwa kubadili muundo wa nafasi zao.

Mwisho Kwa Makonda umecheza

Hujui usemalo, atamfitini hadi amtoe kwenye kiti kama sio kumuua kabisa.

Makonda anautaka urais na sio kingine...wajinga hamjui hilo
 
Ukimsikiliza Makonda unaona kabisa ana uelewa na uthubutu wa kusukuma mambo ya msingi.

Mh.Rais Samia kama hutojali wewe Mteue Makonda awe Waziri Mkuu wako baada ya 2025.

Anaweza kuwasukuma Mawaziri wakawa wanashughulikia kero kama anavyofanya kulingana na ratiba ambayo atawapangia then wewe utapumua.

Baadhi ya mambo Kwa Sasa hayaendi Kwa sababu PM wa Sasa hana ujasiri wa kuwasimamia Mawaziri wenzake.

Ukiangalia kwenye Serikali Yako Mawaziri walau wanafanya kazi ya dhati ya Kumsaidia Rais ni

Bashungwa, Mchengerwa,Mavunde,Ulega,Aweso,Bashe na Naibu wa Uchukuzi.Waliosalia utawaona kwenye matukio tuu.

View: https://youtu.be/VpKhMRf7Oe4?si=0XsIzlSOD8QBIXaQ
Pili tubadili Muundo wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Ili wawajibike zaidi,Kwa sababu haiwezekani kero zimejaa na miradi imekwama na wao wapo na hawachukui hatua.Tuwape Nguvu za kimaamuzi Kwa kubadili muundo wa nafasi zao.

Mwisho Kwa Makonda umecheza kama Pele.

Ni lazima makonda agombee ubunge, au wasigine katiba kama kawaida yao
 
Mzee wangu aliwahi niambia. Tunza vizuri pesa zako uwe na uhuru wa kiuchumi. Njaa mbaya sana. Nlimwelewa mpaka sasa nafurahia uhuru wangu. Njaa mbaya.
 
Mzuuka wanajamvi.

Yumkin hakuna ajuae ni nini Rais anafikiria kufanya ifikapo 2025 ,

Vile vile yawezekana ni wachache Sana wajuoa maandaliz anayofanya kuelekea 2025.

Sasa Kwa kuwa mara kadhaa amekiri kupitapita jf itakuwa vyema Kwa jinsi ulivyouona uongozi wake takribani miaka 3 sasa utoe ushauri wako ili ajipime.

1. Je Rais Samia aendelee kujiandaa kugombea 2025? Kama jibu ni ndio au sio toa sababu zako ili ajipime.

2. Je Rais Samia aendelee kujiandaa kupumzika ifikapo 2025 ili kupisha wengine? Kama ndivyo je ni Kwa nini ?
 
Mimi naona kuhusu waziri mkuu wetu kipindi hiki bado anafanya vizuri na tuendelee kumpa nguvu,kumuunga mkono na kumpa ushirikiano ili amalize salama. Ni msaidizi wa Mheshimiwa Rais wetu na hata tunapomsifia na kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kuwa amefanya vizuri ni ngumu kutompa pongezi zake waziri mkuu wake ambaye amekuwa akipita huku na huku kufanya kazi anazoagizwa na mheshimiwa Rais pamoja na kufanya mengine mengi yaliyo ndani ya uwezo wake.

Lakini pia Mheshimiwa waziri mkuu wa sasa amefanya kwa sehemu yake kama mwanadamu na kama kiongozi.ikimbukwe ya kuwa serikali ni kama timu tu ambapo viongozi wetu wanahitajiana sana katika kutekeleza shughuli za kimaendeleo.kumbuka huwezi ukawa kila mahali kwa wakati mmoja.hivyo ili uonekane bora ni lazima na wachini yako wawe bora, watekeleze vyema majukumu yao na waache kufanya kazi kwa mazoea.

Pili katika mawaziri wachapa kazi nakubaliana na hao uliowataja lakini mimi siwezi kuacha kuwataja na kutambua mchango wao watu kama Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba.hawa ni ngumu sana kuwaacha katika list ya wachapa kazi na waliofanya kazi vyema kabisa katika kutekeleza majukumu yao.

Mfano kama huyo mheshimiwa Ummy Mwalimu mimi namuona kama kiraka ambaye unaweza mpeleka wizara yoyote ile unayotaka wewe na akafanya vizuri sana. Hata Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba naamini naye ametumia vyema sana taaluma yake ya uchumi kutoa ushauri mzuri kwa serikali na Rais wetu katika kujenga uchumi imara na shirikishi.ndio maana tunaona kwa sasa hali ya mfumuko wa bei siyo mkubwa,hali ya uchumi na miradi ya kimkakati inaendelea kujengwa ambayo siku za mbele italeta faida kubwa sana katika uchumi wetu.mzunguko wa fedha ni mzuri sana ambapo kwa mwaka ulioisha inaonyesha ulikuwa mzuri sanaa.

lakini pia mimi naamini mawaziri wetu kwa kiasi kikubwa sana wametekeleza vyema sana majukumu yao na ndio maana kuna maendeleo katika kila eneo na kila sehemu.kwa kuwa kama wasingefanya vizuri lazima tungeona kupwaya katika eneo fulani.

Lakini pia kila wizara ina namna ya kuongoza. Mfano wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa ni wizara ambayo haihitaji makelele ya waziri au mwanasiasa yoyote yule kwa kuwa mambo huko yanakwenda kikanuni na siyo matamko tamko tu.kwahiyo katika wizara hii huwezi ukasema kuwa waziri wake hafanyi kazi kwa kuwa yupo kimya .inakuwa siyo sawa na nikumuonea tu na hata usipomuweka katika wachapa kazi unakuwa unamvunja moyo na kumkosea. Huu ni mfano tu.

Kwa hiyo kikubwa tuwatie moyo mawaziri wetu wote na tutoe ushauri pale tunapoona inafaa kufanya hivyo.lakini mimi naamini wamefanya kazi kubwa na kujitahidi sana kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania.baraza la mawaziri ni kama timu.ambapo wakati mwingine usilazimishe kufunga wewe wakati upo eneo ambalo ukitoa pasi kwa mwenzako itakuwa rahisi zaidi kufunga kuliko wewe.

Ni lazima serikali yetu ifanye kazi kama timu mmoja na iwe na mawasiliano ya kiutendaji kuanzia juu mpaka chini huko na sifa tuwape wote kwa pamoja.tukumbuke hapo hapo kuna makatibu wakuu ambao nao wanakesha wakifanya kazi ili kumfanya waziri apate majibu ya kujibu kwa watu.
Wakati mwingine una busara na hekima kama uliyoitumia kumvisha mtu nguo aliyekuwa uchi wa mnyama kwenye kadanamsi ya watu!
 
Back
Top Bottom