Najua CCM, hawatashinda kwenye uchaguzi huru, lakini, iwee iwavyo, ili, angalau wawavutie wapiga kura, itawalazimu kujiiegemeze kwenye mvumo wa jina Magufuli
Sasa, kwa namna yoyote ile, CCM kampeni zao, itawalazimu, narudia tena, itawalazimu kutumia sifa za hayati Magufuli ili angalau wapate wa kuwavutia, ijapokuwa hawawezi kushinda tena, ikiwa tu uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki
Wanachokifanya baadhi ya mawaziri wa Samia, iwe kwa kutokujua ama kwa kujua, kinamgharimu moja kwa moja mgombea wao ambaye ni Rais Samia kwa mjibu wa mwongozo wao na chama chao, Magufuli hayupo, lakini huku mitaani, karibu kila mtu bado anasikitishwa na kukosekana kwake, wengi wamekuwa wakiamini kwamba, Rais Samia angejikita kuyaenzi kwa dhati yale aliyokuwa akiyasimamia Magufuli hasa kwa kuwatetea wazi wazi walala hoi, masuala ya kukatika katika umeme, huku mambo ya wananchi kudhulumiwa na kunyanyaswa na baadhi ya viongozi wa serikali yakirudi kwa kasi kubwa, hii inawaongezea hasira dhidi ya ccm na viongozi wake
Wanaposikia kuna kiongozi yeyote anatoa kauli mbaya dhidi ya waliyekuwa wakiamini ni mtetezi wao, ni kuwafanya wachukie uongozi wote mpaka Rais aliyepo
Mimi nadhani, hawa watu wanajua fika kabisa kwamba, wananchi wanachukizwa sana pindi jina Magufuli linaposemwa vibaya, pengine mawaziri hao ama viongozi hao wanaosema vibaya jina Magufuli, ni aidha wanakuwa wajua wanachokifanya kwamba, Rais achukiwe na wapiga kura hawa, ni au hawajui kwa sababu hata hivyo, hawamsaidii vya kutosha Rais samia
Narudia tena, JPM hayupo, lakini jina lake ndilo litakuwa sababu ya kuamua ni nani atakuwa Rais wa nchi hii
Mawaziri wa serikali hii wanajua na hata wapinzani wanajua, labda ni kiburi tu cha kupingana na ukweli huu
Nawahakikishia, hao viongozi wanasema eti wapo wanawake watampa kura, wanamdanganya Rais, wanawake wepi watakaompa kura Rais Samia, ni hawa wanaoendelea kupigika mitaani wakiwa wamebeba mabeseni ya mbogamboga na wateja hakuna?
Ni hawa ambao wanalalamika kukimbiwa na waume zao kwa sababu ya maisha magumu?
Ni wanawake wepi hao nauliza?
Utafuteni ukweli viongozi wa CCM, wanawake ambao mimi nimekuwa nazunguka karibu Tanzanua nzima, hawana habari na mnayesema watamchagua
Njia salama kwa wagombea wote, ni kibeba sera zilizokuwa akizitumia JPM zilizojikita kutatua kero za wasio na nguvu wala wasemaji (ak) wanyonge
Wanyonge hawahitaji mambo makubwa, na ndio hao wapiga kura, walimkubali sana JPM na walimwamini sana, sasa inapotokea mtu mmoja, kwa sababu ya hila zake binafsi kulibagaza jina lake, ni kuwajaza hasira dhidi ya... na hata kwa wanaemsemea
CCM, wapende wasipende, nguvu yao bado inabebwa na itabebwa na jina JPM
Endeleeni kujidangaya, mtakutana na hasira za walala hoi mitaani
Muulizeni Katibu wenu mwenezi awaeleze vizuri