Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nikiri tu wazi, NCHI YETU IMEPITIWA NA AWAMU 5...MIMI NIMEIKUTA NCHI IKIWA AWAMU YA PILI...

ILA NADHANI KATIKA AWAMU ZOTE ZILIZOPITA NA HII YA MAMA SAMIA...AWAMU YA MAMA SAMIA SULUHU HASAN NI KIPINDI BORA KABISA CHA UONGOZI... HATUJAPATA KUWA NA RAIS BORA KAMA MAMA SAMIA...

KATIKA KIPINDI CHAKE...

SHIDA YA MAJI IMEKUWA NI HADITHI ZILIZOPITA...
UMEME WA UHAKIKA TENA BEI NAFUU...MGAO TULISHASAHAU AWAMU ZILIZOPITA..

WANANCHI WANA NEEMA NA MAENDELEO YA MMOJA MMOJA...VITU BEI CHEE KAMA BURE... TABU YA SUKARI SIJUI MCHELE...HAKUNAGA HIYO SHIDA KABISA...

MAISHA MAZURI...VIONGOZI WAADILIFU...RUSHWA IMEPUNGUA...

HAKUNA ANAYEDHULUMIWA UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI UMEONGEZEKA SERIKALINI...HAKUNA UZEMBE KABISA...AJIRA BWERERE...

HII NCHI HAIJAWAHI PATA RAIS KAMA MAMA...MAMA BWANA...ANAUPIGA MWINGI MNO...TUNAKUPENDA SANA MAMA...TUNATAMANI HII NCHI UONGOZE MILELE.
Basi makofi kidogo kwa mama😂
 
Ni wazi kabisa bila Upendo wa dhati wa Rais wetu Mpendwa Dr Samia kwa Shujaa Magufuli miradi hii mikubwa ya Bwawa la Nyerere, SGR na daraja la Kigongo-Busisi isingefikia hatua za mafanikio iliyopo

Kipekee kabisa nikushukuru mama wa Upendo Rais Samia kwa kuzienzi Juhudi za Mtangulizi wako

Tunajua baadhi ya Wanasiasa na hata Mawaziri wanatamani miradi hii mikubwa ifeli lakini ndio wameshachelewa

Mungu wa Mbinguni mbariki Rais Samia
 
Tunampongeza kwa kuisimamia miradi hii kikamilifu, japo ni kweli kuna baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wa chama chake na wa vyama vya upinzani hawakupenda hii miradi itimie ili waweze kulitumia suala hilo kisiasa hapo baadae. Lakini ameweza kuwanyong'onyesha na kuwaharibia mipango yao waliyopanga kuitumia muda mrefu.

Tunasubiri mradi wa barabara yetu ya mwendo kasi hapo Bagamoyo road nao ukamilike.
 
Tunampongeza kwa kuisimamia miradi hii kikamilifu, japo ni kweli kuna baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wa chama chake na wa vyama vya upinzani hawakupenda hii miradi itimie ili waweze kulitumia suala hilo kisiasa hapo baadae. Lakini ameweza kuwanyong'onyesha na kuwaharibia mipango yao waliyopanga kuitumia muda mrefu.

Tunasubiri mradi wa barabara yetu ya mwendo kasi hapo Bagamoyo road nao ukamilike.
Pale Kunduchi mecco itakapojengwa Depot ya Mwendokasi utaratibu wa fidia umeanza
 
Pale Kunduchi mecco itakapojengwa Depot ya Mwendokasi utaratibu wa fidia umeanza
Good... Nashauri tenda hii ya ujenzi wa BRT phase 4 wasiipe ile kampuni ya kipumbavu inayojenga ile barabara ya BRT phase 3 kule Nyerere road.

Sijui kwanini moderators wameuunganisha huu kwa uzi mungine na wakati uzi huu ulitakiwa ujitegemee wenyewe. Anyway pongezi nyingi ziende kwa raisi Samia na serikali yake.
 
Bonafsi nampongeza mhe rais, lakin awe makini na wasaidizi walioko upande wake, some of them wana sabotage jitihada zake
 
Tuzingatie hapo kwenye chanjo ya corona.
Mama asione hii 😂😂

20240304_003630.jpg
 
Haya ndio mambo muhimu zaidi ambayo yanawagusa raia walio wengi zaidi hivyo yanapaswa kuulizwa na kuzungumziwa zaidi na kiongozi mkuu wa nchi kila mara, kila wakati na kila mahali.

1. Ajira
2. Kodi
3. Mfumuko wa bei
4. Afya
5. Barabara
 
Nini Kifanyike?

SIASA
Ipo haja ya kuangalia mzigo ambao nchi inabeba kupitia michakato mbalimbali ya kiasiasa na demokrasia.Idadi ya Wizara -Mawaziri/Manaibu Waziri ipunguzwe (Tupunguze gharama kubwa),Idadi ya Majimbo ya uchaguzi ipunguzwe na pia wabunge (Kwa miaka 5 tunatumia fedha kiasi gani kulipa wabunge-Mishahara,Posho,Viinua Mgongo,Etc)..

Madiwani:Viwango vya Sifa,uzoefu na weredi viongezwe ikiwamo elimu,exposure..

Wakuu wa Mikoa/Wilaya:Waondelewe badala Yao watumishi wa umma Wapewe majukumu kupitia hierarchy Za kiutumishi (Hii itapunguza utitiri wa gharama na vyeo)

TOZO KWA DOLA
Malipo ya tozo,fees,ada,pango Kwa dola ni uhujumu uchumi..Fedha Za Tanzania zitumike..Hatuna sababu ya kutengeneza mahitaji (Demand) isiyo ya lazima..
Bandari/shipping lines/CFS/Transporters ..Apartments..Vyuo..Kwa nini walazimishe kulipwa USD?..Ikibidi hata mishahara ya watumishi kwenye baadhi ya Makampuni,taasisi na mashirika (NGO’s) ilipwe Kwa TZS.

KODI
Kufanyike review ya kina kwenye utitiri wa kodi ktk mamlaka zetu na halmashauri zetu..Taasisi..Kodi zinazodidimiza na kifubaza maendeleo ya Viwanda,Uwekezaji na biashara zipunguzwe au kuondolewa.
Tumepoteza wafanyabiashara wengi waliohamia nchi jirani Kama Malawi,Zambia,DRC,Mozambique sababu ya ongezeko la kodi ktk bidhaa nyingi..Tuangalie upya..Tujiulize Kwa nini?

MIRADI

Mwisho nchi ipunguze miradi ya miundombinu inayokula fedha nyingi ambazo kimsingi wanalipwa wakandarasi wa kigeni..

ZABUNI

Zabuni kubwa za taasisi Za Serikali zenye thamani mabilioni ya fedha ktk procurement (IFB/ICT/ICB/RT)ya nchi wapewe wazawa kimkakati ili malipo yake yabaki nchini badala ya sasa fedha nyingi kwenda nje..

MIKOPO

Ni wakati wa kusitisha mikopo isiyo na tija ya haraka Kwa nchi.Ikopwe MIKOPO ya kujenga viwanda (Tuzarishe na kuuza kisha kupata faida),Kilimo (Boost Export),Elimu (Uwekezaji kwenye taaluma Za Kisasa-Engineering,AI,Robotics Science,Nuclear Science,Management Sciences,ICT…)
 
Mheshimiwa Rais, sijui kama ndio unatengenezewa ajali za kisiasa ili wabaya wako ndani ya chama wapate kisingizio au namna gani?

Hudama ya maji Dar imezorota mno, imekuwa ya hovyo kuliko maelezo. Ukiwapigia simu DAWASA wanatoa excuse za kijinga kabisa, eti "umeme unasumbua"! Kwamba wao hawawezi kuwa na backup generators??

Mtaani yamejaa magari ya kuuza maji ambayo ukiyachunguza ni biashara zao hao hao.

Tafadhali mheshimiwa, acha kulea uzembe wanakuharibia hawa!!

Jitahidi kuwa 'pro-active na chukua hatua mapema sio mpaka watu walalamike weee. Waziri wa maji na naibu wake pamoja na menejimenti yote ya DAWASA wanapaswa kuwekwa pembeni, kazi imewashinda!

Na kama kweli TANESCO wanakata umeme kwenye line critical kama hiyo inayopeleka umeme kwenye mitambo ya kuzalisha maji basi nao pia wanapaswa kuliwa vichwa.
 
Najua CCM, hawatashinda kwenye uchaguzi huru, lakini, iwee iwavyo, ili, angalau wawavutie wapiga kura, itawalazimu kujiiegemeze kwenye mvumo wa jina Magufuli

Sasa, kwa namna yoyote ile, CCM kampeni zao, itawalazimu, narudia tena, itawalazimu kutumia sifa za hayati Magufuli ili angalau wapate wa kuwavutia, ijapokuwa hawawezi kushinda tena, ikiwa tu uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki

Wanachokifanya baadhi ya mawaziri wa Samia, iwe kwa kutokujua ama kwa kujua, kinamgharimu moja kwa moja mgombea wao ambaye ni Rais Samia kwa mjibu wa mwongozo wao na chama chao, Magufuli hayupo, lakini huku mitaani, karibu kila mtu bado anasikitishwa na kukosekana kwake, wengi wamekuwa wakiamini kwamba, Rais Samia angejikita kuyaenzi kwa dhati yale aliyokuwa akiyasimamia Magufuli hasa kwa kuwatetea wazi wazi walala hoi, masuala ya kukatika katika umeme, huku mambo ya wananchi kudhulumiwa na kunyanyaswa na baadhi ya viongozi wa serikali yakirudi kwa kasi kubwa, hii inawaongezea hasira dhidi ya ccm na viongozi wake

Wanaposikia kuna kiongozi yeyote anatoa kauli mbaya dhidi ya waliyekuwa wakiamini ni mtetezi wao, ni kuwafanya wachukie uongozi wote mpaka Rais aliyepo

Mimi nadhani, hawa watu wanajua fika kabisa kwamba, wananchi wanachukizwa sana pindi jina Magufuli linaposemwa vibaya, pengine mawaziri hao ama viongozi hao wanaosema vibaya jina Magufuli, ni aidha wanakuwa wajua wanachokifanya kwamba, Rais achukiwe na wapiga kura hawa, ni au hawajui kwa sababu hata hivyo, hawamsaidii vya kutosha Rais samia

Narudia tena, JPM hayupo, lakini jina lake ndilo litakuwa sababu ya kuamua ni nani atakuwa Rais wa nchi hii

Mawaziri wa serikali hii wanajua na hata wapinzani wanajua, labda ni kiburi tu cha kupingana na ukweli huu

Nawahakikishia, hao viongozi wanasema eti wapo wanawake watampa kura, wanamdanganya Rais, wanawake wepi watakaompa kura Rais Samia, ni hawa wanaoendelea kupigika mitaani wakiwa wamebeba mabeseni ya mbogamboga na wateja hakuna?

Ni hawa ambao wanalalamika kukimbiwa na waume zao kwa sababu ya maisha magumu?

Ni wanawake wepi hao nauliza?

Utafuteni ukweli viongozi wa CCM, wanawake ambao mimi nimekuwa nazunguka karibu Tanzanua nzima, hawana habari na mnayesema watamchagua

Njia salama kwa wagombea wote, ni kibeba sera zilizokuwa akizitumia JPM zilizojikita kutatua kero za wasio na nguvu wala wasemaji (ak) wanyonge

Wanyonge hawahitaji mambo makubwa, na ndio hao wapiga kura, walimkubali sana JPM na walimwamini sana, sasa inapotokea mtu mmoja, kwa sababu ya hila zake binafsi kulibagaza jina lake, ni kuwajaza hasira dhidi ya... na hata kwa wanaemsemea

CCM, wapende wasipende, nguvu yao bado inabebwa na itabebwa na jina JPM

Endeleeni kujidangaya, mtakutana na hasira za walala hoi mitaani

Muulizeni Katibu wenu mwenezi awaeleze vizuri
 
Kwetu maji mara ya mwisho yalitoka Januari 6, leo ni miezi 3 hatuna maji. Nimeenda ofisini kwao hadi nimechoka.

Visingizio vyao ni umeme mdogo, mara marekebisho, mara sijui ujinga gani.

Watanzania chini ya CCM tuko kifungoni, kwenye open prison, tuko huru ila tunaishi jela ya wazi.
 
...solution ni push back,nenda pale ofisini kwa dawasa area manager wao,hakikisha haendi nyumbani hadi maji yametoka mtaani kwako, kulalama humu hakusaidii chochote, kwanza muda huu ndio kwanza anakunywa Don Pedro pale Kibo Bar 🍸, Serena Hotel maana kwake maji yapo
 
Mheshimiwa Rais, sijui kama ndio unatengenezewa ajali za kisiasa ili wabaya wako ndani ya chama wapate kisingizio au namna gani?

Hudama ya maji Dar imezorota mno, imekuwa ya hovyo kuliko maelezo. Ukiwapigia simu DAWASA wanatoa excuse za kijinga kabisa, eti "umeme unasumbua"! Kwamba wao hawawezi kuwa na backup generators??

Mtaani yamejaa magari ya kuuza maji ambayo ukiyachunguza ni biashara zao hao hao.

Tafadhali mheshimiwa, acha kulea uzembe wanakuharibia hawa!!

Jitahidi kuwa 'pro-active na chukua hatua mapema sio mpaka watu walalamike weee. Waziri wa maji na naibu wake pamoja na menejimenti yote ya DAWASA wanapaswa kuwekwa pembeni, kazi imewashinda!

Na kama kweli TANESCO wanakata umeme kwenye line critical kama hiyo inayopeleka umeme kwenye mitambo ya kuzalisha maji basi nao pia wanapaswa kuliwa vichwa.
ni hako kaeneo ka tabata sio ndio bado kanasumbua?

nadhani ni kuripoti tu kwa watendaji wa eneo mahalia inatosha, but bila shaka umeskika, umeeleweka pole kwa adha 🐒
 
Back
Top Bottom