Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kufunga ramadhani
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kumuamkia babangu leo
Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuvuka barabara ya Manzese leo
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kupiga pasi nguo zangu za kuvaa leo
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuandika maneno haya
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuiona tena ramadhani na kufunga
Namshukuru rais kwa kuniwezesha kuamka kula Daku leo
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuelewana na mke wangu
Namshukuru rais kwa kuniwezesha
Kuwa hai mpaka leo
Hapo vipi niendelee kumshukuru
Au ni ishie hapo