Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mkuu subiri tumalize matanga, mambo mengine kama teuzi nk, yataendelea baada ya hapo.
 
Ndugu,hii ni kwa mujibu wa mahaba yako tu,ama unayaangalia maslahi fulani,kama anastahili Mama apate,isije kuwa kuna maslahi binafsi katika hoja na mtazamo wako tu.
 
Hilo ni ombi langu kwako.

Chato kuwa mkoa ni hadhi itayopelekea miradi mingi na ya kukumbukwa iliyo asisiwa na Hayati John iwe endelevu na kwalo hata mamlaka za wa wananchi zitakuwa jirani.

Magufuli kaifanyia mengi Nchi hii na shime nasi tuliobaki hasa wenye mamlaka ya juu kama wewe mheshimiwa Rais japo kwa kiasi basi tumuenzi JPM kwa vitendo na hata Chato kuufanya mamlaka kamili ya kimkoa iwe ni sehemu ya uenzi wetu kwake.

Wana jf mliopo madarakani kama Mwigulu Nchemba itapendeza mukimfikishia ushauri huo mama yetu Samia.
 
Halafu?
 
Huko ni Kuongeza gharama zisizokuwa na msingi tu,kachato ni kadogo sana,hakakidhi kuwa mkoa hata kuwa hiyo Wilaya wameforce,hakana idadi ya watu wanaotosha kuanzishiwa Mkoa,hakana mapato tosha pia,inatosha kuwa hivyo ilivyo
 
Yeah, imekwisha hiyo💪!
 
Butiama ni mkoa?
Sijui huwa mnafikiri kwa kutumia nini!
Muasisi wa taifa(JK Nyerere) hakuwahi kufanyiwa hivyo,sembuse huyo monevu na muuaji.
 
Chato itabaki ilivyo tena watu washukuru ikiwa hivyo, sana sana itaporomoka na kuwa magofu. Mama Samia ni kiumbe tofauti kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…