Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hilo ni ombi langu kwako.

Chato kuwa mkoa ni hadhi itayopelekea miradi mingi na ya kukumbukwa iliyo asisiwa na Hayati John iwe endelevu na kwalo hata mamlaka za wa wananchi zitakuwa jirani.

Magufuli kaifanyia mengi Nchi hii na shime nasi tuliobaki hasa wenye mamlaka ya juu kama wewe mheshimiwa Rais japo kwa kiasi basi tumuenzi JPM kwa vitendo na hata Chato kuufanya mamlaka kamili ya kimkoa iwe ni sehemu ya uenzi wetu kwake.

Wana jf mliopo madarakani kama Mwigulu Nchemba itapendeza mukimfikishia ushauri huo mama yetu Samia.
Chato haina hadhi technical ya kuwa mkoa. hawajifikia vigezo.

And nikwambie tu acheni kunipendekeza kwa marehemu. he is gone.

Marais wa nchi hii waliopita hawakugeuza maeneo waliyotoka kuwa mikoa.

Guyu kaja juzi tu mmnalamba viatu mpaka kaburini?

acheni unafki.
 
Hilo ni ombi langu kwako.

Chato kuwa mkoa ni hadhi itayopelekea miradi mingi na ya kukumbukwa iliyo asisiwa na Hayati John iwe endelevu na kwalo hata mamlaka za wa wananchi zitakuwa jirani.

Magufuli kaifanyia mengi Nchi hii na shime nasi tuliobaki hasa wenye mamlaka ya juu kama wewe mheshimiwa Rais japo kwa kiasi basi tumuenzi JPM kwa vitendo na hata Chato kuufanya mamlaka kamili ya kimkoa iwe ni sehemu ya uenzi wetu kwake.

Wana jf mliopo madarakani kama Mwigulu Nchemba itapendeza mukimfikishia ushauri huo mama yetu Samia.
Chato haijakidhi vigezo vya kuwa Mkoa, Viongozi wasitoe bila kuwa na kigezo kwa kutaka kumpendezesha mtu fulani
 
Hilo ni ombi langu kwako.

Chato kuwa mkoa ni hadhi itayopelekea miradi mingi na ya kukumbukwa iliyo asisiwa na Hayati John iwe endelevu na kwalo hata mamlaka za wa wananchi zitakuwa jirani.

Magufuli kaifanyia mengi Nchi hii na shime nasi tuliobaki hasa wenye mamlaka ya juu kama wewe mheshimiwa Rais japo kwa kiasi basi tumuenzi JPM kwa vitendo na hata Chato kuufanya mamlaka kamili ya kimkoa iwe ni sehemu ya uenzi wetu kwake.

Wana jf mliopo madarakani kama Mwigulu Nchemba itapendeza mukimfikishia ushauri huo mama yetu Samia.
Iwe nchi tu
 
Waswahili kwa mihemko
Mihemko ndiyo asili yetu, 😅 😅 😅 tunafikiria na kutafakari baadaye, huoni hata kuna msemo tumejipa kenge hasikii mpaka apigwe damu zitokee masikioni??

Haataariii sana!

Mh Raisi mama Samiah, asiingizwe kwenye mtego na hawa mamluki. Namuombea sana, Mungu amzidishie hekima na busara awang'amue na ajiepushe nao.

Everyday is Saturday................................😎
 
Hilo ni ombi langu kwako.

Chato kuwa mkoa ni hadhi itayopelekea miradi mingi na ya kukumbukwa iliyo asisiwa na Hayati John iwe endelevu na kwalo hata mamlaka za wa wananchi zitakuwa jirani.

Magufuli kaifanyia mengi Nchi hii na shime nasi tuliobaki hasa wenye mamlaka ya juu kama wewe mheshimiwa Rais japo kwa kiasi basi tumuenzi JPM kwa vitendo na hata Chato kuufanya mamlaka kamili ya kimkoa iwe ni sehemu ya uenzi wetu kwake.

Wana jf mliopo madarakani kama Mwigulu Nchemba itapendeza mukimfikishia ushauri huo mama yetu Samia.
Wasukuma ninyi ni wa hovyo sana, hamkuridhika na Juhudi za kuiinua Chato?
 
Amna cha Chato wala chatu kila mtu anajenga kwao sasa huyo nae akajenge kule kijiji ametoka itapendeza na nchi itaendelea kiaina, Kama Nyerere angeimarisha Butiama, Ali angeimarisha kwao, Mkapa angeimarisha kwao Kikwete nae, umeona eei sasa tiyari tungekuwa na miji yenye ustawi mkubwa sana.

BiShow akajenge kwao na tusisikie kwin'yoo kaeni kimya kama mnaonyolewa para ,sasa ni mwendo mdundo kila anaekaa uraisi ndani ya miaka mitano anajenga huduma za kimataifa kijijini alikotoka kama ni daraja uwanja wa ndege bandari reli atachagua mwenyewe na vyengine atavishughulikia sehemu zingine ,tumemuona Marehemu Magufli alijenga kwao lakini hakusahau sehemu zingine,reli ya kasi,mabasi mwendo kasi,gesi ni mengi mpaka vituo vya mabasi akijenga sehemu ambazo si kwao.
 
Mna matatizo ya akili na ukabila ninyi.

Mkoa wa watu 350,000 zinawatosha kweli!

Au bado mmelewalewa kupendelewa?

Mbona hatuna mkoa wa Butiama, Mkoa wa Chalinze au Mkoa wa Lupaso na viwanja vyake vya ndege.

Akili mbovu kabisa!
 
Wahenga walisema kauli hujenga.

Ebu yasikilize maneno ya mama yetu Samia akiwaasa kina mama wale wanao lilia 50/50.

Kama atakuwa na muendelezo wa kuamini ktk heshima kwa kila mtanzania na kuichukulia kuwa Tanzania ni moja basi wacha tuanze kufanya mazoezi ya kutembea vifua mbele.
 
Kwa muda sasa, udhibiti wa mada hapa JF umekuwa ukiongezaka kupita kiasi na kuondoa kabisa maana ya slogan inayotumiwa na huu mtandao( inafahamika kwa member humu).

Inafika hatua mtu unaandika mada huku unajiuliza hii mada itabaki au itafutwa. Tumefika hatua mbaya.

Sasa leo nimelata mada ya kuwashauri Mama Samia ateua IGP,CDF na Boss wa TISS kutoka Zanzibar eti nayo imeondolewa. This is too much!
Mods wa jf ni wajivuni (kama wahaya) na wanajipendekeza, wanatamani ateuliwe mmoja wao awe IGP.
 
Ushauri huu ulitolewa mnamo Dec 17, 2015.
 
Katika jambo ambalo wananchi wanalisubiri kwa hamu hasa ndani ya siku 100 za Rais wetu Mama Samia Suluhu ni kuiona alitumia aina tofauti kabisa ya uongozi wake ulijaa utashi na ubunifu mpya badala ya kutegemea kufanya yake Marehemu JPM.

Aliyoacha JPM yamebebwa na timu yake aliyoweka kwenye mfumo wa serikali na chama. Watu hawajui kua Magufuli alikua ni Mafuli na Samia atakua Samia, Hawa wawili ni watu tofauti kimtizamo na hulka, kwahiyo uongozi wao lazima utofautiane tupende tusipende.

Ushauri wangu kwa Mama Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania: Kamwe asije akaegemea washauri wa mzee wamsaidie kutekeleza aliyoyaacha iwe kwenye chama au ndani ya mfumo, Mama atulie kwanza ikiwezekana akae hata mpaka miezi 3 asome Ramani kisha aje na mfumo wake mpya uliojaa ubunifu mpya, anaweza kutekeleza yote aliyoacha JPM lakini kwa style tofauti. Huu mfumo alioacha mzee akiutengemea utaanza kufanya maandalizi kwa kujijenga zaidi kuandaa mtu wao 2025 ambaye Mama atajikuta yupo nje bila kujua.

Alifanyiwa hivyo Mama Joyce Banda wa Malawi aliyekua akiongoza kwa kutumia washauri wa Prof Mutharika ambao waliingia na kuanza kujijenga na kisha wakamuondoa.

Chonde chonde Rais wangu Mama Samia kwa sasa tulia soma mazingira kwanza jipe muda, angalia shida iko wapi kisha baadae anza kufanya mabadiliko. Makamu wa Rais awe ni mtu mpya kabisa asiyetoka kwenye team JPM,JK au Lowassa, chagua mtu ambaye ana uzoefu na mchamungu lakini ambaye utaweza kufanya naye kazi ukimtuma ataenda.Kamwe asitoke katika timu yeyote usije ukaharibiwa kazi.

Baada ya kumaliza kumpata Makamu wa Rais nenda kwenye Baraza la mawaziri na kisha malizia kufanya mabadiliko ndani ya chama na mfumo wa serikali. Chagua timu itakayoendana mfumo wako ambao ni Unique na wa kufuata katiba ya nchi na mafanikio makubwa.

Watu wa mfumo wa mzee wanajulikana,hawakua wabunifu na wala hawana ushauri wowote ndio maana mambo mengi alikua akiamua yeye wao walibakia kumuogopa tu.

Rais Mama Samia you are the President of United Republic of Tanzia, all powers are yours, no one can disturb you.
 
Magufuli was the one of his own, sidhani kama alikuwa na kundi au mtandao.

Samia atasumbuliwa na magenge mtandao ya ccm na visasi vya waliopoteza vyeo.

Ngoja tuone lakini! Mitano tena
 
Mijadala ya bajeti ambayo imeshaandiliwa kwa upande wa Serikali haioneshi kamwe kama kutakuwa na kupanda kwa mishahara. Ile Wage Order ina Zaidi ya miaka nane ipo vile vile tu. Sasa Mungu katusaidia - je Mheshimiwa Rais wa sasa Samia Suluhu utaanza na ahadi gani kuhusu mishahara ya wafanyakazi Mei Mosi ya Mwaka huu? Kazi kwako!
 
Mi binafsi nakuamini sana Mama. Najua unaweza kutufikisha pale ambalo Rais JPM alipaona.

Kuna mambo mawili nakushauri mimi kama mtanzania mzalendo

1. Uchaguzi umeisha, hatutaki siasa, tunataka kazi tu. Kampeni mpaka 2024. Simania hili mheshimiwa.

2. Ongeza jicho kwa majirani zetu KENYA.

Kwa miaka mingi wameshiriki kutuhujumu...ila kipindi cha JPM wamecheza kwaito...kaza kama alivyokaza Magufuli.
 
Back
Top Bottom