Katika jambo ambalo wananchi wanalisubiri kwa hamu hasa ndani ya siku 100 za Rais wetu Mama Samia Suluhu ni kuiona alitumia aina tofauti kabisa ya uongozi wake ulijaa utashi na ubunifu mpya badala ya kutegemea kufanya yake Marehemu JPM.
Aliyoacha JPM yamebebwa na timu yake aliyoweka kwenye mfumo wa serikali na chama. Watu hawajui kua Magufuli alikua ni Mafuli na Samia atakua Samia, Hawa wawili ni watu tofauti kimtizamo na hulka, kwahiyo uongozi wao lazima utofautiane tupende tusipende.
Ushauri wangu kwa Mama Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania: Kamwe asije akaegemea washauri wa mzee wamsaidie kutekeleza aliyoyaacha iwe kwenye chama au ndani ya mfumo, Mama atulie kwanza ikiwezekana akae hata mpaka miezi 3 asome Ramani kisha aje na mfumo wake mpya uliojaa ubunifu mpya, anaweza kutekeleza yote aliyoacha JPM lakini kwa style tofauti. Huu mfumo alioacha mzee akiutengemea utaanza kufanya maandalizi kwa kujijenga zaidi kuandaa mtu wao 2025 ambaye Mama atajikuta yupo nje bila kujua.
Alifanyiwa hivyo Mama Joyce Banda wa Malawi aliyekua akiongoza kwa kutumia washauri wa Prof Mutharika ambao waliingia na kuanza kujijenga na kisha wakamuondoa.
Chonde chonde Rais wangu Mama Samia kwa sasa tulia soma mazingira kwanza jipe muda, angalia shida iko wapi kisha baadae anza kufanya mabadiliko. Makamu wa Rais awe ni mtu mpya kabisa asiyetoka kwenye team JPM,JK au Lowassa, chagua mtu ambaye ana uzoefu na mchamungu lakini ambaye utaweza kufanya naye kazi ukimtuma ataenda.Kamwe asitoke katika timu yeyote usije ukaharibiwa kazi.
Baada ya kumaliza kumpata Makamu wa Rais nenda kwenye Baraza la mawaziri na kisha malizia kufanya mabadiliko ndani ya chama na mfumo wa serikali. Chagua timu itakayoendana mfumo wako ambao ni Unique na wa kufuata katiba ya nchi na mafanikio makubwa.
Watu wa mfumo wa mzee wanajulikana,hawakua wabunifu na wala hawana ushauri wowote ndio maana mambo mengi alikua akiamua yeye wao walibakia kumuogopa tu.
Rais Mama Samia you are the President of United Republic of Tanzia, all powers are yours, no one can disturb you.