Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Ameanza kufuata nyendo zake baada ya watu kuwa wakali kwa kugawa raslimali zetu.Huyu wa sasa vp
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ameanza kufuata nyendo zake baada ya watu kuwa wakali kwa kugawa raslimali zetu.Huyu wa sasa vp
Shetani akitajwa lazima nitokee kuweka record sawa.Ningeshangaa atajwe JPM usijitokeze fasta😂😂😂, sijui alikufanyaje 😅
Kwetu wapi wewe tulia!kama ilivyokuwa kwenu kila kitu kutukana...mwiba hitolewa ulipoingilia
Endeleeni kumdanganya mama yetu.Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Anashikilia furaha yako kwa vile anakutupia makombo.Ndugu zangu Watanzania,
Napenda tu mfahamu ya kuwa Mkuu wa Nchi au waweza kusema Rais wa Nchi anaweza kuwafanya wananchi na Taifa kwa ujumla kuwa na Furaha,amani na utulivu mioyoni Mwao.anaweza kuwafanya watu wakaishi pasipo hofu wala wasiwasi wala mawazo ya huzuni au Msongo wa Mawazo.
Matendo ya Rais ,kauli za Rais,sera za Rais,matamko ya Rais ni vitu vinavyoweza kuchochea hayo niliyoyaeleza hapo juu. Ni kauli za Rais zinaweza kujenga umoja wa kitaifa, mshikamano, upendo miongoni mwa wananchi na kwa upande Mwingine ni kauli hizohizo Za Rais zinaweza kuchochea na kujenga hali ya uhasama ,ubaguzi ,mpasuko katika Taifa,kuvunja umoja wa kitaifa na hata kujenga chuki katika mioyo ya watu.
Ni matendo ya Rais Pia yanaweza chochea umoja na mshikamano pamoja na imani ya wananchi kwa serikali yao ,taasisi za serikali na ofisi za umma.na ni matendo ya Rais yanaweza ondoa imani ya wananchi kwa serikali yao,taasisi zao na hata ofisi za umma pamoja na kuwa na chuki nazo.
Lakini pia sera za Rais zinaweza inua matumaini ya watu au kuwakatisha tamaa.zinaweza fanikisha ndoto za watu au kuzima ndoto za watu.ndio maana wengine hufikia hatua ya kutamani kiongozi fulani na utawala wake upite haraka ili wapate kupumua na kupata matumaini kiuchumi.ndio sababu wengine hupata sauti ya kumpinga kiongozi fulani na kumtaka ajiuzuru kwa sababu ya kukosa matumaini chini ya utawala wake.
Ukiangalia tangia kuingia madarakani kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan unaona namna alivyoinua matumaini ya watu,imani ya watu kwa serikali yao,kujenga umoja wa kitaifa, mshikamano na upendo miongoni mwa wananchi.amaeleta nuru na mwanga kwa maisha ya wengi,amechochea matumaini ya wengi kutimiza ndoto zao na kufikia malengo yao.
Rais Samia amewafanya Watanzania kuwa wenye furaha kutokana na kauli zake zenye kuhimiza umoja na mshikamano,kuhimiza na kutenda haki kwa vyombo vyote vya utoaji haki. Sera zake kiuchumi zimekuwa zenye kuleta matumaini makubwa sana.ndio sababu kila siku mitaani biashara mpya zinafunguliwa na kuongezeka kwa kasi.
Watanzania Tuna kila sababu ya kumshukuru sana Rais Samia kwa uongozi wake huu wenye kugusa maisha ya watu na kumfikia kila mmoja kwa kadri ya mahitaji yake na kiu yake.tuna kila sababu ya kumpa miaka mingine mitano Ya Urais kwa kishindoo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.amani na furaha yetu vipo mikononi mwa Jemedari wetu Hodari Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.View attachment 3074324
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ni chukizo hata kwa MunguMama samia kwangu ni chukizo kwa familia yangu na majirani zangu, nikiona sura yake nazima tv
Furaha yako tu Mwenyewe imeshikiliwa na Rais Samia na ndio maana inacheza cheka na kufurahi sana huku jukwaani.maana huna msongo wa Mawazo wala wasiwasi ya aina yoyote ileAnashikilia furaha yako kwa vile anakutupia makombo.
Wewe hunaga akili kabisa.Ni chukizo hata kwa Mungu
Umeelewa andiko langu ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo na chuki binafsi.Everyone is replaceable. Nyie nyie ndio mlikua mnasema hakuna kama Magu. Wanafiki na vigeugeu
Ni some ujinga wako kweli, kichwa cha habari kimetosha kufanya maamuziUmeelewa andiko langu ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo na chuki binafsi.
Furaha yangu inashikiliwa na Bwana Mungu. Huo ujinga wa kuabudu wanadamu baki nao mwenyeweFuraha yako tu Mwenyewe imeshikiliwa na Rais Samia na ndio maana inacheza cheka na kufurahi sana huku jukwaani.maana huna msongo wa Mawazo wala wasiwasi ya aina yoyote ile