Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Attachments

  • FB_IMG_1608708500589~2.jpg
    FB_IMG_1608708500589~2.jpg
    40.2 KB · Views: 7
Ndugu zangu Watanzania,

Kwanza ningependa kuwakumbusheni kwa machache kati ya Mengi kuhusu mtu kuwa Rais.Ningependa kuwaambieni ya kuwa Mtu hawi Rais wala kukidhi vigezo vya Urais kwa kufanya tukio moja au kwa matukio yampito kama mvuke.wala mtu hawi RAIS kwa kuongea sana maneno mdomoni pake bila mipaka, mpangilio,utaratibu na utulivu.

Urais unahitaji mtu mwenye utulivu wa akili,mwenye afya njema ya akili .mwenye uwezo wa kudhibiti na kutawala hisia zake ,hasira zake,Mihemko yake,chuki zake, kinyongo chake na hata matamanio yake binafsi. Urais hauhitaji ujuaji. Urais ni taasisi inayohitaji mtu mwenye historia ya kiutendaji iliyotukuka. unaweza kumbeba beba mtu kwa njia zote na kumuweka katika nafasi fulani lakini kamwe huwezi kumbeba beba na kumzoa zoa mtu kumuweka kwenye kiti cha Urais.

Kwa hakika ni lazima utalitikisa,kulitetemesha,kulipoteza,kulivuruga,kulisambaratisha, kulikwamisha na kuleta sintofahamu kwa Taifa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha usalama na umoja wa kitaifa.unaweza kumpa mtu upendeleo wa kumpatia nafasi yoyote ile na hata akifanya makosa yasiwe na athari kwa Taifa .lakini kamwe huwezi kumpa mtu Urais kwa majaribio na matamanio yako tu binafsi.

Urais siyo mahali pa kujifunzia kazi au kufanyia majaribio.Urais ni nafasi inayohitaji mtu aliyepevuka kiakili na kimwili,mtu anayejiheshimu,asiye na utoto utoto hata katika maandishi yake na maamuzi yake.Urais unahitaji mtu mwenye ngozi ngumu na mwenye uwezo wa kuogelea na kupiga mbizi katika Mawimbi ya kila aina na kulivusha Taifa.Urais hauhitaji ushindi katika kila mjadala.bali unahitaji maridhiano,subira, uvumilivu,usikivu kila panapotokea jambo lenye kugusa hisia za watu na mivutano. .

Urais unahitaji mtu mwenye uwezo ,akili ya kuongoza watu na kuwaleta pamoja licha ya tofauti zao za kisiasa ,mitizamo,Imani na mengine Mengi. Urais unahitaji mtu mwenye uwezo wa kufikiri ndio kufanya maamuzi na siyo kufanya maamuzi au kutoa maneno au kauli na kisha kufikiria juu ya maamuzi au kauli au maneno yaliyokwisha kutolewa na kutoka kinywani kama Risasi.

Ukiangalia hayo machache niliyoyaeleza utakubaliana nami kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuvaa viatu vya Rais Samia vya Uraisi. Ni Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan anayestahili kuendelea kuliongoza Taifa letu.kwa sababu ameonyesha uwezo,utulivu na stamina ya hali ya juu sana hata katikati ya mambo mazito yenye kila aina ya hisa kali , minyukano ya maneno ,mawazo na maoni tofauti tofauti yenye kuibua hadi maneno ya ubaguzi na kibaguzi.

Rais Samia wakati wote ameonyesha umakini na utulivu wa kiwango cha juu sana.Historia yake pia ya kiutendaji imetukuka na iliyoonyesha ukomavu na utulivu wa kiuongozi alionao.amepita katika majaribu ya kila aina lakini amevuka akiwa imara na madhubuti.tofauti na wengine unakuta jambo dogo tu anajikuta akipaniki,kuhemuka,kupoteza utulivu,umakini na ustahimilivu na kujikuta akitumia na kuongozwa na jazba na hisia.

Rais Samia ameanzia na kupita maeneo mengi mpaka kufika hapo alipo kiutumishi.amekaa na kufanya kazi na watu mbalimbali na wenye aina tofautitofauti za kiuongozi.ndio maana yakuona ameiva na kukomaa kisawasawa.Anajiheshimu na ameiheshimisha taasisi ya Urais.Anajuwa nini anafanya na nini anapaswa kufanya na nini hapaswi kufanya hata kama anatamani kufanya kama binadamu wengine.kuna mwingine unakuta ni kiongozi mkubwa lakini anafanya vitu ambavyo vinashusha hadhi na kuchafua kiti alichokalia.ni lazima ufahamu ya kuwa kuna vitu binafsi inabidi ujizuie kufanya au kutenda.ni lazma ufahamu kuna uhuru binafsi fulani inabidi ukubali kupunguza unapokuwa kiongozi wa juuView attachment 3132946

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tunaye Mbowe
 
Na zaidi sana hakuna Mtanzania mwingine kwasasa, ndani na nje ya CCM, mwenye sifa, vigezo vya kizalendo na mipango yenye dhamira ya kweli na nia njema ya kuwaletea waTanzania maendeleo, zaidi ya huyu mama wa Taifa na kipenzi cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan 🌹
 
Back
Top Bottom