Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kwahiyo ikitokea amefariki Dr Mpango hana uwezo huo?
Utakufa wewe na kutangulia .Rais wetu ni mpango wa Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu.Ni Mungu mwenyewe anayeendelea kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania
 
Acha uongo wako wewe! Tanzania hata Kilaza na CHAWA kama wewe, unaweza kutawala na kupata kabisa wajinga wachache wa kukupamba na kukusifia.
 
Hii sasa ni kufuru na upuuzi wa viwango vya juu mno
 
Kashikilia furaha ya ya baadhi ya wanachama machawaa na familia yake huku kimkazi ,familia ya mkwe wake ,hata wewe hajashikilia yako kujikomba tuu kama atakuonaaa.
 
Huyu mama tumpe maua yake,pamoja na kwamba anamapungufu yake hasa ya kutokudhibiti matumizi sahihi ya pesa za serikali zinawekwa kwenye miradi mbalimbali zinazoendelea hapa nchini

Nachompongeza mpaka sasa miaka aliyokaa madarakani hakuna cha raia kubeba tofari wala jiwe la msingi kujenga jengo la serikali au kituo cha afya yaan raia tumerelax serikali inafanya yote pasipo kushika bata wala mbuzi ya raia

Huyu binti tumpe tu mitano tena ila nachomuomba asicheke na kima tena

kwa uzamini wa pride of the nation konyagi

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
Unaishi Tanzania? Mbona kila siku wananchi wanachanga kujenga shule
Chukua taarifa hizi chache

 
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kujenga uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi.

Rais Samia anajua fika sekta ya viwanda ndio chimbuko la maendeleo ya haraka ya nchi mbalimbali na ni mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuongeza thamani ya malighafi tulizonazo, kutoa ajira kwa wananchi, kuongeza mapato ya Serikali, kuingiza fedha za kigeni pamoja na kusaidia katika mapambano ya kuondoa umaskini.

Katika miaka yake takribani minne sasa Serikali anayoiongoza imefanikiwa kuvutia uwekezaji wa viwanda vikubwa vyenye kuzalisha bidhaa za teknolojia ya hali ya juu na zenye kuhitajika sana kwenye uchumi wa kisasa wa leo.

Shilingi bilioni zaidi ya 92 zimewekezwa kwenye Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme na transfoma cha Elsewedy (Elsewedy Electric) kilichopo eneo la Kisarawe 11, Kigamboni Dar es Salaam. Huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya @ccmtanzania 2020 - 2025 kwa vitendo!

#SamiaKazini
#HakunaKilichosimama
#UchumiWaViwanda
#MaendeleoKwaVitendo
#TunaendaNaSamia2025

 
Tayari Kiwanda cha kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam kimeanza uzalishaji. Huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya @ccmtanzania 2020 - 2025 kwa vitendo!

#SamiaKazini
#HakunaKilichosimama
#UchumiWaViwanda
#MaendeleoKwaVitendo
#TunaendaNaSamia2025
 

Attachments

  • IMG_0063TCV-1024x683.jpg
    129.2 KB · Views: 5
  • IMG_0249TCV-860x573.jpg
    63 KB · Views: 6
  • IMG-20240509-WA0580-1024x789.jpg
    192.3 KB · Views: 5
  • SAMIA-6.jpg
    65.3 KB · Views: 5
  • IMG-20240509-WA0875.jpg
    134.9 KB · Views: 6
  • IMG-20240509-WA0876.jpg
    109.1 KB · Views: 5
  • IMG-20240509-WA0755-1024x797.jpg
    155.6 KB · Views: 6
  • SAMIA-9.jpg
    93.4 KB · Views: 6
  • SAMIA-5.jpg
    85.7 KB · Views: 7
Tumejaribu kumtetea sana.

1. Ubaya wa demokrasia uko palepale watu wanapotea na wagombea wanakatwa kiholela. 4R ni maneno tu
2. Rushwa imeongezeka na uwajibikajo wa wafanyakazi umepungua

Sasa tumsifie kwa lipi? Maana mwenzake alipambana na rushwa sana. Yeye kachukuwa yote mabaya ya Magufuli na mazuri kayaacha!.

Kwa wazalendo wa kweli msemeni Mama kwa manufaa yetu sote sio kusifia kwa unafiki na kufikiri mna msaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…