Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

90
We kweli malaria kweli! Hao watanzania wengi uliwaona wapi? We unajua Tanzania ina watu wangapi?

Ni watu wangapi kati ya hao walikwambia mitano tena kwa Mh mama Samia??
90% we utakufa na kihoro Samia mpk 2030
 
Nina ushauri kwa Mheshimiwa Rais Samia, utapita kwenye uchaguzi ujao na ukianza kazi baada ya uchaguzi fikiria kujenga Kariakoo namba 2 Pwani(Kibaha au Mlandizi) kuhepusha msongamano mjini na maghorofa kuzidiwa na kuanguka. Inakuwaje mtu atoke Chalinze kwenda Kariakoo? Mbagala na Temeke na ukanda huo watumie Kariakoo ya mjini ukanda wa Pwani watumie Mlandizi au Kibaha maana itakuwa ni bei ileile ya bidhaa za Kariakoo namba 1 ndo bei hiyo hiyo Kariakoo namba 2 na structure ya jengo iwe ile ile ya Kariakoo ya mjini. Hiyo itaepusha pia foleni ya magari mjini.
 
1.Madaraja zaidi 1000 nchi nzima
2.viwanda 80,000
3.Shule mpya 2,000
4.zahanati mpya 5,000
5.kupandisha mishahara
6.Kupandisha madaraja ya kiutumishi
7.kuvutia wawekezaji wa ndani na nje
8.uchumi kupanda kwa zaidi ya 5%
9.kuimarika kwa shilingi yetu.
10.kusimamia sheria ipasavyo
11.kuunda tume ya maridhiano
12.kuongeza mikopo ya wanavyuo
13.kuanzisha samia scholarship
14.kuongeza ajira
15.madawati mapya zaidi ya laki moja
16.kuongeza pato la mtanzania
17.madawa bwerere hospitalini
18.maji nchi nzima yanatiririka
19.kumalizia miradi yote ya watangulizi wake
20.vituo vya police vipya zaidi ya 500.
Huyu mama jamani anapiga kazi,mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.
 
Project dodoki new version
 
Haya yote yanawezwa kufanywa na private sector ya Bwana kafulila PPP ( Pubic Private Partnerships) ndani ya mwaka mmoja tu... kyagata, accha kukuza mambo...
 
Hata marekani na china wanakopa pia
Tunajua,,, ndo maana tunasema hakuna jipya.... maana alichokopa ndo hicho alichotumia.. Ingshangaza kama angkuja na nia mbadala zaidi ya kuongeza mzigo wa deni,,, hao uliowataja hawakopi kwenda kuzamisha hela, zinaenda kuzalisha...
 
Ubarikiwee, ubarikiweeee, ubarikiwe na bwana! Una nafasi yako mbinguni kwa baba yetu. Huyu mama ni mpango mahsusi wa Mungu, ana akili sana, nchi sahivi ina pesa imetulia tulii. Mwezi huu kalipa nyongeza ya mishahara km alivyoahidi Mei Mosi, siyo mambo ya arrears. Ingekuwa siyo mafisi kuzengea urais ningetamani aongeze mpk achoke km Angel Merkel Chancellor wa Ujerumani. Ila wanawawake wako serious na kazi ingawa majinga yapo. Apewe maua yake Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan, uongozi ni kipaji siyo kufokafoka. Mungu ampe maisha marefu, OKTOBA TUNATIKI, na tunamchagua mama yetu.
 
Nikisoma hizi comment leo huwa nacheka sana ...😁😁kuna watu ni mmejaliwa upofu kabisa ...nakumbuka hii miaka ndiyo nilikuwa natukanwa na wana chadema balaa na kuitwa sukuma gang na kuchongewa nipigwe ban kila kukicha nikiitwa mchochezi kwa kuwaeleza watu ufunuo wa uovu utakao likumba taifa chini ya samia....leo nimeona nipitie nyuzi za nyuma kujikumbusha mazuzu mlivyo tutukana kisa mkimsifia samia na kuwambia aachane na sukuma gang wote serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…