Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3. Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4. Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5. Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7. Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8. Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.
Wapumbavu kama huyu walikuwa wengi sana 😁😁
 
View attachment 1729237View attachment 1729236

Nakukumbusha mama wakati unaanza kurekebisha baraza la mawaziri anza na Wizara ya Afya. Wizara imeyumba sana imekuwa na waziri asiye na msaada wowote. Hii ni wizara serious sana lakini waziri wake aligeuka kuwa comedian na kuacha sayansi. Ikukupendeza mheshimiwa huyu atenguliwe hata ubunge maana ni hasara tu.

Hatuwezi kuwa na watu wanafiki wa kumfuatisha rais anachopenda badala ya kuwa mshauri asiyeyumba katika kusimamia fani yake kwa weledi
Wajinga na wapumbavu kwenye huu uzi mlikuwa wengi sana 😁😁😁
 
😂😂😂naiona roho ya Magufuli ikifanya kazi kwa kasi ya ajabu kupitia Mama Samia! Wezi mtajiju! Siyo kwa mapovu hayo! Magufuli's secret weapon Mama Samia ndio kapewa rungu! Gogogogo 'Iron lady' go go go!
Tanzania 1st
Vipofu mlikuwa wengi sana kwenye huu uzi 😁
 
Samia namuona kwamba ni Rais mwenye lugha ya staha,mwenye uungwana na utu.

anayeshaurika,mchapa kazi bila kutaka 'kuabudiwa',aliye makini lakini bila ubabe; asiyejiamria mipango ya kifedha vyovyote atakavyo,mwenye kuuheshimu muhimili wa BUNGE, asiyeelekeza miradi mingi kule tu alikozaliwa,asiye na viashiria vya ukabila;

muwakilishi wetu mzuri kwenye masuala ya Kimataifa, mwenye 'kuwajali' watumishi wa Umma, asiyebeba visasi moyoni, asiyeua vyama vya Upinzani, mwenye bahati za kipekee,Mtumishi Mzoefu Serikalini,Mchumi,pia kwa Taifa zima(mbali na madaraka aliyonayo) yeye bado ni mama yetu mwema!

UNA LA KUMSHAURI NA KUPENDEKEZA?
Vipofu mlikuwa wengi sana kwenye huu uzi 😁
 
Hongera Dr Samia kwa ujasiri uliouonyesha Bahari imetulia kila kitu kipo shwari nchi na chama kwanza mengine baadaye ama kweli mzigo mzito hufikishwa na wanawake huyo mrithi wako physician ateue msaidizi mtulivu kama yeye asiye maarufu kama yeye bali mtendaji zaidi
 
Huyu mama bana,anachapa sana kazi.
Na uzuri mmoja sio mtu wa kukurupuka na kusikiliza majungu
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Andiko mujwarabu kabisa hili sijui nilikuwa wapi kulisoma mie
 
Kitu pekee anachoamini mama ni kwamba vijana wake anawaanda kuwa viongozi unajuwa mtandao huo vizuri wewe au unausikia ! Hao watu wanatengeneza mpango wa mda mrefu kutawala nchi hii kwa kupumbaza watu kwa kuwapa vyeo vidogovidogo! Hawa watu ndiyo wanaojiweka karibu na vyombo vyetu vya dola na hutokuta vyombo vyetu vinawajibika kwa kutetea wananchi
 
1755079627935.png


Akiongea na wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Annamringi Macha amesema ng’ombe milioni 2.54, mbuzi 0.96 milioni na kondoo 0.79 milioni, jumla ya mifugo milioni 4.39, ni rasilimali muhimu zinazoiweka Simiyu kwenye nafasi ya tatu kitaifa kwa wingi wa mifugo.

Aidha, ameeleza kuwa katika kuboresha sekta hii, Serikali imeongeza majosho kutoka 111 mwaka 2020 hadi 164 mwaka 2025, kuanzisha kituo cha maabara ya mifugo Wilaya ya Meatu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa, kusambaza madume bora ya ng’ombe aina ya Borani, kuanzisha mashamba darasa ya malisho na kuboresha miundombinu ya masoko ya mifugo.

Hata hivyo hatua hizo zimeongeza tija, kupunguza magonjwa na kuongeza mapato ya wafugaji, huku zikichangia ajira na ustawi wa kiuchumi kwa jamii za wafugaji katika Mkoa.
 
View attachment 3440007

Akiongea na wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Annamringi Macha amesema ng’ombe milioni 2.54, mbuzi 0.96 milioni na kondoo 0.79 milioni, jumla ya mifugo milioni 4.39, ni rasilimali muhimu zinazoiweka Simiyu kwenye nafasi ya tatu kitaifa kwa wingi wa mifugo.

Aidha, ameeleza kuwa katika kuboresha sekta hii, Serikali imeongeza majosho kutoka 111 mwaka 2020 hadi 164 mwaka 2025, kuanzisha kituo cha maabara ya mifugo Wilaya ya Meatu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa, kusambaza madume bora ya ng’ombe aina ya Borani, kuanzisha mashamba darasa ya malisho na kuboresha miundombinu ya masoko ya mifugo.

Hata hivyo hatua hizo zimeongeza tija, kupunguza magonjwa na kuongeza mapato ya wafugaji, huku zikichangia ajira na ustawi wa kiuchumi kwa jamii za wafugaji katika Mkoa.
Imesaidianini hata kama mifugo ipo?
 
Back
Top Bottom