Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

1755234518293.png

==
Kuna kitu wengi hamkijui kwa Rais Samia, Hebu jiulizeni mpaka uzalishaji maziwa umeongezeka hadi Lita mpya 900,600,000 za maziwa. Mtu mwenye baraka akitawala kila kitu kinastawi kama hivi.

Uzalishaji wa jumla wa maziwa umeongezeka kutoka Lita 3,101,384,000 mwaka 2020 hadi 4,009,985,321 mwaka 2024|25, tofauti ya 908,601,321 sawa na ongezeko la asilimia 29. Ng’ombe wa asili na wa kisasa wamesaidia kufanikisha ongezeko hili kupitia mbegu bora, teknolojia mpya za ufugaji na lishe bora, hatua iliyoongeza tija, ubora wa maziwa, usalama wa chakula, kipato cha wakulima na thamani ya uchumi wa mifugo na wafugaji.
 
Lita ya maziwa imepungua bei ili niweze kuyanywa na mimi?
 
View attachment 3441698
==
Kuna kitu wengi hamkijui kwa Rais Samia, Hebu jiulizeni mpaka uzalishaji maziwa umeongezeka hadi Lita mpya 900,600,000 za maziwa. Mtu mwenye baraka akitawala kila kitu kinastawi kama hivi.

Uzalishaji wa jumla wa maziwa umeongezeka kutoka Lita 3,101,384,000 mwaka 2020 hadi 4,009,985,321 mwaka 2024|25, tofauti ya 908,601,321 sawa na ongezeko la asilimia 29. Ng’ombe wa asili na wa kisasa wamesaidia kufanikisha ongezeko hili kupitia mbegu bora, teknolojia mpya za ufugaji na lishe bora, hatua iliyoongeza tija, ubora wa maziwa, usalama wa chakula, kipato cha wakulima na thamani ya uchumi wa mifugo na wafugaji.
Hivi huwezi kutoa mada bila kumsifia mwanasiasa?
Mwanasiasa ndiye anayefuga?
Kwa taarifa yako, uzalishaji haujaongezeka kiasi hicho katika kipindi ulichokitaja, bali kuongeza ukusanyaji wa taarifa ndio umesababisha kupata hizi namba.
Undocumented production data (Black market) Tanzania ni kubwa mno.
 
1755235636308.png


Chini ya Rais Samioa uzalishaji wa nyama ya ng`ombe umeongezeka kutoka tani 508,355.17 mwaka 2020 hadi tani 666,227.02 mwaka 2024/25, tofauti ya tani 157,871.85 sawa na ongezeko la asilimia 31, Hii ni kutokana na maboresho ya mbegu bora, ufugaji wenye tija na usimamizi mzuri, hali iliyoongeza tija, kipato vijijini na thamani ya pato la taifa.
 
kilo ya nyama umesema au unataja uzito wa nyama.
 
Hizo data zimepatikanaje? Zamani zile wale wa 1980s kurudi nyuma kulikuwa na vituo vya kukusanyia maziwa- Dairy kila mkoa, Leo viko wapi? Vingekuwepo hivi walao kila kijiji ungeweza kusema hizo data zina uhalisia. Labda huko Iringa na Mbeya anakonunua Asas.

Wakati wa kampeni za JPM za 2020 alizungumzia hili jambo. Baadae PM alikuja kuzindua mkakati wa suala kama hili wakati huo JPM hatuanaye. Taarifa kupitia vyombo vya habari. Kulikuwa na wafadhili toka Marekani.Sijui mapango umefikia wapi. Mwenye taarifa za Vituo hivi atuwekee orodha vilipo kimkoa, mie nikawekeze maana ni shughuli wengi tunahimudu. Usisahau maziwa ni "white Dimond"
 
Umechanganya aina za nyama bana hatuli nyama ya ng'ombe tunakula dagaa wa nyama
 
1755236904493.png


Chini ya Rais Samia, mifugo aina ya ng’ombe imeongezeka kutoka 33,928,391 mwaka 2020 hadi 39,241,375 mwaka 2025, sawa na ongezeko la ng’ombe 5,312,984 ambao ni asilimia 16,

Hii ni kutokana na sera za uboreshaji wa mbegu, huduma bora za mifugo ikiwemo chanjo za ruzuku, na upatikanaji wa malisho bora na ya uhakika, hatua iliyoongeza tija, kipato cha wafugaji na usalama wa nyama na chakula nchini.
 
Huyu Samia huyu. Hata kwenye ng'ombe yumo. Mtakuja kumuua mama wa watu kwa sifa maana machawa dah! Mungu Azidi kumlinda kwa kweli!
 
View attachment 3441723

Chini ya Rais Samia, mifugo aina ya ng’ombe imeongezeka kutoka 33,928,391 mwaka 2020 hadi 39,241,375 mwaka 2025, sawa na ongezeko la ng’ombe 5,312,984 ambao ni asilimia 16,

Hii ni kutokana na sera za uboreshaji wa mbegu, huduma bora za mifugo ikiwemo chanjo za ruzuku, na upatikanaji wa malisho bora na ya uhakika, hatua iliyoongeza tija, kipato cha wafugaji na usalama wa nyama na chakula nchini.


Wazee wa kupika data
 
Nchi inaendelea kuwa ya kijinga kadili siku zinavyokwenda. Sijui kizazi gani kitakuja kuwa na akili huko mbele na kuiokoa mama Tanzania.
 
Back
Top Bottom