Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

R.i.P John
Hili nalo limepita.

Rais Mama Samia Hassan Suluhu, kwanza napenda nikupongeze kwa jukumu jipya ulilo nalo mbele yako, ambalo ni kuongoza taifa la Tanzania na hasa jukumu kubwa la kurudisha imani ya wananchi hasa Vijana ambao hawajatengenezewa ajira kwa miaka kadhaa tangu walipo hitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati. Kwahakika vijana wengi wamepoteza nuru na imani ndani ya nchi yao.
Mh Rais, nakukumbusha uwakumbuke watumishi wa uma ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekua na kilio kikubwa cha subira kwenye ongezeko la mishahara (annual increments) kwa miaka kadhaa sasa, na ukweli ni kwamba watumishi wengi wamepoteza furaha kazini ilkhali wanasemea pembeni kwa hofu ya kuto kuwajibishwa. Kama itakupendeza Mh Rais, ebu tia neno ili basi uwabariki watumishi siku ya May mosi.
Mh Rais, kama ikikupendeza nivyema ukaangaza mifuko ya hifadhi ya jamii hasa upande wa mafao ya uzazi/kujifungua, pamoja na mafao ya kuachishwa kazi. Kwahili pamekua na vilio vingi vya wanachama kutokupewa mafao yao huku wakikosa majibu sahihi ya lini watalipwa ama nini kinacho endelea.
Mh Rais, kwa heshima na taadhima naomb kuwasilisha haya machache na ikiwa itakupendeza nivyema ukayafanyia kazi na pengine ikawa umerudisha nuru na imani kubwa kutoka kwa wananchi, watumishi na wahitimu wa vyuo.
 
Huyu mama watu wasimchukulie poa. Anaonekana mpole kwa kuongea lakini kwa vitendo ni sindano inayochoma. Shauri enu mnaomchulia poa mwenzenu tayari katumbuliwa.
Tumpe mitano tenaaaaa au ?[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mama akipiga kama miaka mingine kumi Tanzania itafika mbali sana.
 
Mama anaanza vizuri zama za ubabe zinaelekea ukingoni
Lets wait and see. Wewe ndiye utakuwa wa mwanzo kumnang'a hasa atakapoanza kutoa vibali vya watu wa JK wasilipe kodi. Ni uungwana kuweka akiba ya maneno si kukurupuka
 
Kikawaida nyumba haitakiwi kuongozwa na mwanamke ila kwa ubovu wa mifumo yetu Leo tunaongozwa na mwanamke
 
Nimemsikia Rais akitumia neno naomba mara nyingi katika maongezi yake.

Nafahamu watu wa mwambao huwa na lugha ya kiuungwana sana katika mazungumzo yao lakini hii lugha haijakaa kimamlaka sana kuweka mkazo kwa watu ambao hawajazoea lugha kama hiyo kutoka kwa viongozi wao. Hivyo ni vizuri atumie maneno "Nataka" "Naagiza" "Naelekeza" "Nahitaji" "Naamuru"
 
Kikawaida nyumba haitakiwi kuongozwa na mwanamke ila kwa ubovu wa mifumo yetu Leo tunaongozwa na mwanamke
Pia nakukumbusha kwakuwa mamlaka imeshikiliwa na mwanamke basi tuchague maneno ya kutumia/heshima kwa viongozi wetu,

Neno la kiswahili yaani KONGOLE hutumika kuwapongeza watu jinsia ya kiume baada ya kufanya jambo fulani kwa upande wa mwanamke, kiswahili sanifu cha kumpa sifa/kumpongeza huwa tunatumia neno HONGERA, hivyo kwenye uzi wako ungetumia neno hili kumpongeza Rais wetu kipenzi mama la mama Mama Samia Suluhu kuwa HONGERA SANA MADAM PRESIDENT.
 
Mh Raisi mama Samia anasema takukuru waangalie Kama kuna kesi za kubumba bumba wasizipeleke mahakamani

Zinaichafua serekali hongera mama kwa kutambua"wanyonge walikuwa Wana nyongwa kweli"

Kesi nyingi ni zao la kujipendekeza so dhani hata Kama hayati alikuwa anafurahia
Mama ni mtu wa haki. Serikali ya mwenda zake ilikuwa ya masifa na uonevu. Kila kesi ni uhujumu uchumi ili ukae mahabusu. Asante Mh. Rais kwa kuona hili. Wengi sasa wata toka.
 
Back
Top Bottom