R.i.P John
Hili nalo limepita.
Rais Mama Samia Hassan Suluhu, kwanza napenda nikupongeze kwa jukumu jipya ulilo nalo mbele yako, ambalo ni kuongoza taifa la Tanzania na hasa jukumu kubwa la kurudisha imani ya wananchi hasa Vijana ambao hawajatengenezewa ajira kwa miaka kadhaa tangu walipo hitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati. Kwahakika vijana wengi wamepoteza nuru na imani ndani ya nchi yao.
Mh Rais, nakukumbusha uwakumbuke watumishi wa uma ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekua na kilio kikubwa cha subira kwenye ongezeko la mishahara (annual increments) kwa miaka kadhaa sasa, na ukweli ni kwamba watumishi wengi wamepoteza furaha kazini ilkhali wanasemea pembeni kwa hofu ya kuto kuwajibishwa. Kama itakupendeza Mh Rais, ebu tia neno ili basi uwabariki watumishi siku ya May mosi.
Mh Rais, kama ikikupendeza nivyema ukaangaza mifuko ya hifadhi ya jamii hasa upande wa mafao ya uzazi/kujifungua, pamoja na mafao ya kuachishwa kazi. Kwahili pamekua na vilio vingi vya wanachama kutokupewa mafao yao huku wakikosa majibu sahihi ya lini watalipwa ama nini kinacho endelea.
Mh Rais, kwa heshima na taadhima naomb kuwasilisha haya machache na ikiwa itakupendeza nivyema ukayafanyia kazi na pengine ikawa umerudisha nuru na imani kubwa kutoka kwa wananchi, watumishi na wahitimu wa vyuo.