Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mshahara hapana asiongeze, unatosha kabisa. Na ajira asitoe maana vyuo sikuhizi vinatoa watu wengi kuliko uwezo wa serikali kuajiri, akisema aendane na kasi ya wasomi kuzalishwa atakwama. Cha msingi afanye mazingira ya watu kujiajiri kupitia biashara, tehama na kilimo hasa watu kufanya biashara za nje ya nchi kuwe rahisi(vibali na passport virahisishwe).

Naunga mkono kupunguza makato na kutoa riba kwenye mkopo wa Elimu ya juu.
 
Wakuu Salaam..

Imependezwa tena kwa siku ya leo kuanza kupata mwanga kidogo kuhusiana na masuala yanayoendelea katika nchi yetu ikiwemo uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye shirika la ndege la ATCL... Pia kule bandari napo tumeona hali siyo shwari.


Hatujui kesho maeneo mengine hali itakuwaje kwenye miradi mikubwa ya SGR,Bwawa la kufua umeme la Mwl Nyerere, mabasi ya mwendokasi, madaraja na barabara.

Itoshe tu kusema Mh Rais kachagua njia sahihi ya kuwaonesha watanzania hali halisi ya nchi yetu ili tujue wapi tulipotoka, tulipo na kule tunapotaka kuelekea.


Kipindi cha aliyekuwa mtangulizi wake mara nyingi haya mambo tulifichwa na hawahawa ambao leo wameanza kusema kweli ya hali halisi, hatujui ni kwamba mambo yamebadilika ghafla au wamesoma upepo.

Tunakuomba Mh Rais kwa sasa usimuhakikishie mtu yeyote kuendelea na wadhaifa wake serikalini wala usimtumbue yeyote. Cha kufanya wape muda waweke mambo yote hadharani, baada ya hapo wewe sasa ndio uchuje nani wa kwenda nae.

Kila la kheir.
 
Kuna ubadhilifu mkubwa sana unatendeka pale kiwanda cha nguo urafiki.

Kuanzia naibu meneja mkuu wa kiwanda na wenzake wamegeuza kama kiwanda chao binafsi, wafanyakazi hatupati haki zetu, wamepangisha wafanyabiashara, kodi kidogo wanapeleka bank lakini pesa nyingine nyingine zaidi hawatoi risiti za kielektroniki kwa wanaolipa kodi.

Ili kuuhadaa umma wanatoa risiti chache tu kama ushahidi. Lakini pia kuna rushwa iliyokithiri, hususani kwa meneja nkelebe na wenzake, tunaiomba serikali itubadilishie watu Hawa ili na sisi wafanyakazi tupate haki zetu.

Sikia kilio chetu mheshimiwa Rais
 
Mheshimiwa Rais,

Vijana tuliohitimu vyuo toka mwaka 2015 tuna hali ngumu sana mtaani.

Hima, tunaomba utuangalie(sana) sisi vijana tuliohitimu vyuo toka mwaka 2015 kwani tunateseka katika nchi yetu wenyewe.

Kumbuka tumeandaliwa katika mazingira ya kutegemea kuajiriwa.
Lakini toka mwaka 2015 tumewekwa kando kwa sababu lukuki zikiwemo;
UHAKIKI WA WATUMISHI,KUJENGA MIUNDOMBINU KWANZA na KUUNDA UPYA MFUMO WA AJIRA.

Sasa mama,tunaomba katika utawala wako utupe jicho la kulia.
Halafu pia uone kama ni watoto wako hawa wanaohangaika.

Mungu amekuweka wewe kwenye urais kwa makusudi mengi likiwemo hili suala la ajira.

Basi tunaomba uteekeleze mipango ya Mungu.


NB: Ukimaliza hili, fumuafumua kitu kiitwacho "HESLB". Ni chukizo.
 
Ishu ya ATCL mama kaonesha ukomavu. Anakwenda kuifanyia maamuzi makini tunaita 'Rational decision' Hajakurupuka nayo, ile ishu atasikilizia bunge linasemaje.

Ndugai na Tulia wanatakiwa wafanye maamuzi ya busara sana. CAG kishavua msalaba kawatwika wabunge kazi kwao kuamua kupiga porojo au kutetea wananchi.
 
Mishahara duni, vyeo havipandi.

Mkiajiriwa na mikopo yenu hiyo si mtaishia kazini siku ya kuripoti tu
 
Back
Top Bottom